Stendi ya Nyegezi ni ya pili kwa ukubwa hapa Mwanza baada ya ile ya Nyamohongolo, wakati wa ujenzi wake ilielezwa kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 15 zilitumika kwa mradi huo ikiwemo maegesho ya mabasi, magari madogo, vyumba maalumu za abiria na chumba cha Wanawake wanaohitaji kunyonyesha watoto.
Upande wa Stendi ya Nyamuhongolo imeelezwa imegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 26. 6 ambapo pia kuna eneo la kuegesha malori, stendi ya mabasi yenye uwezo wa kuingiza mabasi 120, jengo la hoteli, eneo la gereji, eneo la ghala pamoja na maduka.
Pamoja na mambo mazuri yote hayo lakini bado kuna changamoto ya uendeshaji na kusababisha vyumba vingi kukosa wateja katika stendi hizo;
Stendi ya Nyamuhongolo
Vyumba kutumika kwa matumizi binafsi
Baadhi ya Wafanyabiashara wanadai kuna vyumba vinatumika kama vyumba vya watu binafsi kutokana na uwepo wa magodoro lakini vingine vimekuwa stoo za kuhifadhia vitu mbalimbali.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Stendi ya Nyamuhongolo wamelazimika kujenga kibanda nje ya Stendi, wengi wao wamefanya hivyo kutokana na gharama ya upangaji kuwa juu na sio rafiki kabisa kwao, inaelezwa bei ni kuanzia Sh Laki 6 hadi Milioni.
Kuna baadhi ya Mawakala ofisi zao zipo jirani na maeneo ya Nyegezi ambapo wamepanga katika nyumba binafsi ili kupunguza gharama
Biashara ni ngumu pia
Licha ya mzunguko wa fedha lakini biashara zimekuwa ngumu kwa kuwa abiria wengi wanakwepa kununua vitu ndani ya stendi hizo kutokana na gharama kuwa juu, Wafanyabiashara wanapandisha bei ili angalau wakidhi mahitaji ya fedha walizotumia kuwekeza kwenye vituo hivyo.
Halmashauri zinatakiwa kuwapa watu au kampuni maalum kuendesha vituo hivyo kwa kuweka mikakati sahihi.
Serikali inatakiwa kuingilia kati kwa kuwa kuna uwepo wa kutupiana mpira katika upangishaji wa vyumba kiasi ya kwamba inaonekana si jambo la kawaida kama mradi wa watu wachache tu walioamua kukinufaisha wenyewe.
Chumba cha kunyonyeshea wengi hawakijui
Kuna huduma maalumu za abiria zinatolewa mfano katika Stendi ya Nyegezi kuna chumba cha Wanawake Wanaohitaji kunyonyesha watoto wao, swali ni kwamba abiria mmewafikiaje wafahamu kuna huduma hizo na wawe tayari kuzitumia?
Ni vyema ukubwa wa Stendi hizo uendane na hadhi ya Wafanyabishara waliopo ili Halmashauri na Mkoani wa Mwanza kupata mapato ya ndani.