Watoza ushuru Stendi ya Magufuli wanatoa risiti za aina mbili, wana risiti za Sh 500 na za Sh 2,000, mtu wa Bajaj ukiingia kuchukua abiria wanakuomba Sh. 1,000 kisha wanakupa risiti ya Sh 500.
Ukigoma kuwapa wanakupa risiti ya Sh 2,000, risiti zote zina maelezo ya kufanana, ni parking fee per day. Tunashindwa kuelewa ipi ni tozo sahihi ya Bajaj kati ya risiti ya Sh 500 au ya Sh 2,000.