Stendi ya Magufuli imefanya watu wa mikoani wengi kudhani Mbezi Luis ndio City Centre ya DSM na kuleta dharau

Stendi ya Magufuli imefanya watu wa mikoani wengi kudhani Mbezi Luis ndio City Centre ya DSM na kuleta dharau

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Kipindi niko mdogo stendi ya kwenda mikoani kutokea Dar ilikuwa Kisutu na nyingine ilikuwa Mnazi mmoja

Ni mpaka early 90s meya au mkurugenzi wa Jiji Bwana Keenja slipoihamishia Ubungo,jamaa alikuwa mbunifu sana.

John Pombe Magufuli akaisogeza mbezi Luis

Hii imepekekea wamikoani wengi wakidhani mbezi ndio City centre,niliwahi kuleta uzi humu jinsi nilivyompoteza ndugu yangu mitaa ya Congo Kariakoo baada ya kuliponda jiji letu, yule bwana alitembea kwa miguu kutoka kariakoo mpaka mbezi malamba mawili maana hakuwa na nauli, kuanzia siku hiyo akawa mpole.

Ni kama Morogoro Town hufanya watu wadhani pale Msamvu ndio city center,bila kujua mji uko ndani huko,zamani miaka ya 70 barabara ilikuwa ikipita katikati ya mji wa Morogoro

Hivi unajua jiji la Dar ed Salaam huenda linazidi jiji la Detroit nchini marekani kwa mambo mengi?najua kuna watu watabisha,nimefika Detroit na naijua Dar tofauti kama ipo ni kidogo sana.

Niliwahi kufika Kinshasa nikashangaa mji unaanzia kama posta mpaka Kibaha ni mji tu. Kinshasa ni kubwa zaidi ya mara tatu ya Dar Es salaam kwa size na population, nadhani wako milioni 17 kwa anayesikia habari za waasi wa Congo anaweza kudhani Congo yote ni magofu.

Naomba tuupe heshima jiji letu la DSM kama hulijui omba utembezwe,au kama umefikia Kitunda au Chanika,bado hujalijua jiji.

Hapo kariakoo tu uwe umezaliwa Dar au umeletwa na mwenge lazima kuna siku uliwahi kupotea.

Miji na majiji yote ya Tanzania nimeyatembelea Dodoma after 15 year atleast wanaweza kuanza kuleta battle za kujishindanisha na Dar, mikoa mingine subirini kwanza miaka 60 ijayo

Kipindi tunapata uhuru Tanga ilikuwa nambari mbili after Dar,miaka 60 mbele iko nyuma sana
 
Actually,to be sincerely honest in my humble opinion,without being sentimental and of course without offending anyone who thinks differently from my point of view, and without hiding any thoughts in my mind, and without lies to the actual truth, with my clear open mind and clean heart,expressing whatever is embedded inside me for a long time which I didn't say because I was nervous. But today, by gathering all the courage and motivation, I just want to say that I actually feel and think that I have absolutely nothing to say. Thank you!
 
Actually,to be sincerely honest in my humble opinion,without being sentimental and of course without offending anyone who thinks differently from my point of view...
Kwa kweli, kuwa mwaminifu wa dhati katika maoni yangu ya unyenyekevu, bila kuwa na hisia na bila shaka bila kumuudhi mtu yeyote ambaye anafikiri tofauti na maoni yangu, na bila kuficha mawazo yoyote katika akili yangu, na bila uongo kwa ukweli halisi, na wazi yangu wazi.

Akili na moyo safi, nikieleza chochote kilichowekwa ndani yangu kwa muda mrefu ambacho sikusema kwa sababu nilikuwa na wasiwasi. Lakini leo, kwa kukusanya ujasiri na motisha yote, nataka tu kusema kwamba kwa kweli ninahisi na kufikiria kuwa sina la kusema. Asante!
 
Miji yote duniani ina slums na vitongoji,downtown ya majiji yote wazungu hutumia ramani au GPS,ukiona mji hupotei ujue hicho ni kijiji,kariakoo imepimwa lakini lazima upotee,New York kupotea ni kugusa tu
Kabla ya GPS New York City nilipata tabu sana ya kupigiwa simu na wabongo wanaopotea njia kuuliza wapite wapi.

Siku hizi GPS imemaliza kabisa hizi simu watu hata hatutafutani.
 
Dah mada imejaa mambo mengi knoma kuliko main point.

1: Kumpoteza ndugu yako mitaa ya Congo
2: Habari za watu wa Morogoro
3: Kufananisha Dar na Detroit - USA
4: Kufananisha Dar na Kinshasa na watu wake
5: Umeidharau mikoa mingine dhidi ya Dar
 
Dah mada imejaa mambo mengi knoma kuliko main point.

1: Kumpoteza ndugu yako mitaa ya Congo
2: Habari za watu wa Morogoro
3: Kufananisha Dar na Detroit - USA
4: Kufananisha Dar na Kinshasa na watu wake
5: Umeidharau mikoa mingine dhidi ya Dar
The theme is Dar is underated na watu wasioijua,same applies to Morogoro and Kinshasa
 
Dah mada imejaa mambo mengi knoma kuliko main point.

1: Kumpoteza ndugu yako mitaa ya Congo
2: Habari za watu wa Morogoro
3: Kufananisha Dar na Detroit - USA
4: Kufananisha Dar na Kinshasa na watu wake
5: Umeidharau mikoa mingine dhidi ya Dar
Dar haifikii hata nusu ya KINSHASA,hata kwa idadi ya watu!
 
Back
Top Bottom