Stendi ya Magufuli imefanya watu wa mikoani wengi kudhani Mbezi Luis ndio City Centre ya DSM na kuleta dharau

Hii kubishania miji huwa ni kwa maslahi ya nani? Maana kuna watu wapo dar wanaishi mazingira machafu na magumu kuliko panya na mende wanaokula mahindi na matunda kwenye maghala vijijini achilia mbali binadamu.
 
Mjini ni mjini tu.
 
Miji yote duniani ina slums na vitongoji,downtown ya majiji yote wazungu hutumia ramani au GPS,ukiona mji hupotei ujue hicho ni kijiji,kariakoo imepimwa lakini lazima upotee,New York kupotea ni kugusa tu
Kweli kabisa. Moja ya miji iliyopangiliwa vizuri ni jiji la Tanga lakini pamoja na kukaa jiji hilo miaka isiyopungua tisa nilishawahi potea mara moja maeneo ya Msambweni
( kwa wanaolijua jiji la Tanga ) japo ilikuwa usiku lakini kupotea ni kupotea tu hadi nikaanza kuwauliza watu njia ya kunifikisha Ngamiani.
 
Ni Kama wanaofika Mwanza wakafikia Nyegezi Bus Stand au Nyamong'oro bus stand, bado hawajalijua jiji 😁.
Ni mtazamo Tu😂
 
I just want to say that I actually feel and think that I have absolutely nothing to say. Thank you!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…