ksjdhhehbdb
New Member
- Jul 3, 2024
- 1
- 1
Ukiingia katika Stendi ya Magufuli unakutana na changamoto kubwa ya ukosefu wa maelekezo na mifumo bora ya kuwaongoza abiria.
Hakuna mabango au michoro ya kuelekeza watu wanapofika, hivyo inakuwa vigumu kujua sehemu ya kukatia tiketi, jengo la abiria lilipo au maeneo muhimu ndani ya stendi. Hata zile lifti zilizopo hazifanyi kazi, hali inayoongeza usumbufu hasa kwa wasafiri wenye mizigo au wenye changamoto za kutembea.
Abiria wanaposhuka kwenye mabasi mara nyingi wanabaki njia panda bila kufahamu wanapaswa kuelekea wapi kutokana na ukosefu wa alama na maelekezo ya kutosha.
Inashangaza kuona kuwa pamoja na changamoto hizi, kuna taarifa za mapato makubwa yanayokusanywa kila siku. Tunaomba uongozi husika uzingatie kuboresha huduma za msingi, kuweka alama za maelekezo na kuhakikisha miundombinu iliyopo inafanya kazi ili abiria wapate huduma inayolingana na hadhi ya stendi hiyo.