KERO Stendi ya Mbezi Chini yazidi kuwa kero, Barabara yavamiwa na wafanyabishara. Mamlaka ziingilie kati

KERO Stendi ya Mbezi Chini yazidi kuwa kero, Barabara yavamiwa na wafanyabishara. Mamlaka ziingilie kati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Stendi ya Mbezi Chini kumekuwa kero kiukweli, sio magari au watembea kwa miguu yaani wafanyabiashara wamepanga bidhaa zao hadi kwenye barabara kabisa. Wengine wameegesha kabisa mabanda sasa hivi hata magari kupishana imekuwa shida

Kiukweli Serikali kama wa napita na kuangalia hali hiyo na kuacha kuna hatari sana kiukweli inaenda kutokea pale tunaomba sana serikali iweke jicho lake pale hasa wakati wa jioni ndio balaa.
 
Huu uchaguzi unaacha wapiga kura wasibughudhiwe. Ngoja ifike Novemba humuoni mtu kakaa bila mzigo hapo
 
Ni kero sana sana, hata kama ni kutafuta ila hatuwezi kuishi bila utaratibu.
 
Habari,

Stendi ya Mbezi Chini kumekuwa kero kiukweli, sio magari au watembea kwa miguu yaani wafanyabiashara wamepanga bidhaa zao hadi kwenye barabara kabisa. Wengine wameegesha kabisa mabanda sasa hivi hata magari kupishana imekuwa shida

Kiukweli Serikali kama wa napita na kuangalia hali hiyo na kuacha kuna hatari sana kiukweli inaenda kutokea pale tunaomba sana serikali iweke jicho lake pale hasa wakati wa jioni ndio balaa.
Nilishapita hii njia kwa bahati mbaya jioni, ni kero sana sanaaaaa.
 
Kiukweli hali ni ya kusikitisha. Serikali iingilie mapema kabla madhara hayajatokea, badala ya kusubiri yatokee halafu baadae waanze kuunda tume za uchunguzi wakati wangeweza kuweka mazingira sawa na kudhibiti hali mapema.
 
Tatizo hilo ni la karibu nchi nzima, binafsi nazishauri mamlaka ziyatambue majukumu yao, na ingependeza kama tutatenganisha taaluma na siasa, Kuna vitengo kama bibi na bwana Afya, ni kwamba mimea ya kijani huchukuwa hewa chafu na kutoa hewa safi, hivyo basi kwa bidhaa kama mbogamboga ambazo ni kijani zinapopokea hewa chafu ikiwemo vumbi na Moshi wa magari uwezekano wa kupumua haiwezekani kwani ilishatenganishwa na shina, hivyo kumfanya mlaji kula sumu ambayo itakuwa imefyonzwa na hiyo mimea

Pili, watu wa mazingira, nao wangesimamia Sheria ya Uchafuzi wa mazingira kwa kuwakamata na kuwatoza faini wale wote wanapanga bidhaa kandokando mwa barabara, Tatu, Tarura/Tanroad, vitengo hivi Nina hakika havikujenga barabara ili kuwa masoko, nao wangezisimamia Sheria zao siamini kama Kuna yeyote angelithubutu kufanya biashara barabarani, nne, Polisi, Kuna Sheria kama mtu akinywa sumu au kujinyonga na akanusurika Jamuhuri humshitaki kwa kosa la kutaka kujiua, Sasa ni kwanini Sheria hiyohiyo isitumike kwa wale wote wanapanga barabarani kwa kufunga kwa makusudi ili magari na vyombo vingine viavyotumia barabara viwagonge?.

Mwisho ni halmashauri/mipango miji, kwamba sura ya mji au mitaa ni pamoja na muonekano wake halisi, Leo hii ukipita barabarani na hata kwa wenye fremu za maduka utakuta bidhaa zimepangwa mpaka maeneo ya watembea Kwa miguu, kwanini wasiwakamate na kuwashitaka kwa kosa la kufunga njia/barabara bila kibali na kuwatoza faini?

Nina Imani kama vitengo vyote hivi vikisimamia Sheria zao na wanasiasa kutoshabikia uvunjaji huu wa Sheria hatutawaona watu hao barabarani Tena.
 
Kabisa, na wale wanaochoma nyama za usiku pale za buku buku na mishkaki ya mia mbili, mamlaka iangalie kama zinafaa kwa binadamu baadae tusije kusababisha watu kuingia kwenye gharama za matibabu yasiyo ya lazima
 
Habari,

Stendi ya Mbezi Chini kumekuwa kero kiukweli, sio magari au watembea kwa miguu yaani wafanyabiashara wamepanga bidhaa zao hadi kwenye barabara kabisa. Wengine wameegesha kabisa mabanda sasa hivi hata magari kupishana imekuwa shida

Kiukweli Serikali kama wa napita na kuangalia hali hiyo na kuacha kuna hatari sana kiukweli inaenda kutokea pale tunaomba sana serikali iweke jicho lake pale hasa wakati wa jioni ndio balaa.
Wanachalamila hao ukiwagusa analiwasha
 
Back
Top Bottom