Kuna mdau hapo kaongelea ubunifu. Inaelekea yuko sawa. Hatuna ubunifu nchi hii.
Mtu mmoja akijenga fremu za maduka akafanikiwa inageuka fasheni nchi nzima wote wanafanya hivyo hivyo.
Issue ya stand pia iko hivyyo hivyo, kila halmashauri inasjibdana na nyingine kujenga stand! Na nyingi zimegeuka white elephant.
Stand zinajengwa mbali na wananchi ambao wanalazimika kiingia gharama za biila sababu na yakitokea mabadiliko tuna shangaa.
Yanayotokea Nyamhongolo hayana tofauti ya yalitoko Nyegezi, vyumba vingi vya biashara vimefungwa kwa kuwa hakuna watu..
Na hata wenye guest house maeneo ya kuzunguka stand nyingi zinafungwa kwa kukosa wateja ambao walilengwa abiria.
Na sababu kubwa ya anguko la hizi stand ni uamuzi wa kuruhusu mabasi kusafiri wakati wote. Hivyo hakuna haja ya kulala guest, kula vyajula visivyo na ladha na kuandaliwa katika mazingira machafu n.k.
Kwa wenyeji wa Mwanza watakumbuka jinsjibiashara ya kupangisha wanafinzi wa saut ilihuokufa kifo vha asili licha ya baadhi ya watu kuwekeza mamilioni ya fedha na au nyumba za makazi kugeuzwa za kupanga wanafunzi, yote hii ni baada ya Uongozi wa chuo kujenga hosteli zake.