Tatizo hao mawakala wengine bei zao zipo juu sana yaani ni bora tuendelee kuvumilia tu hizo siku kwakweli.sasa kuliko utumie aliexpress, si unaorder kitu kwa agents kama bashley, exa etc wapo wengi tu na mzigo unachukua siku tatu hadi dar, electronics kama simu ni siku tisa, mi siwezi tumia aliexpress or ebay nk.. kwasababu ya muda, unaagiza kitu kinakufikia ushasahau.. yan miezi miwili niwe nasubiri kitu,, mmmh hapana
Mkuu unaweza kuniagizia display ya Samsung A50 Bei ganiVodacom Tanzania : Welcome
Vodacom Tanzania Public Limited Company is Tanzania's leading mobile operator and mobile financial services provider, with the fastest nationwide data network and the largest mobile money network in the country. We provide various communication services to more than 12.6 million customers.vodacom.co.tz
Mzigo Dsm lazima utapitia tu,maana mizigo yote inapokelewa hapo kisha wanaichambua na kuipeleka katika masanduku ya barua yanayohusika pamoja na mizigo yote ya mikoani. Kwa wewe wa Iringa maana yake mzigo wako utaletwa posta Iringa halafu posta ya mahali ulipo. Kama upo mkoani hapohapo utauchukulia posta kama upo wilayani utakuja katika posta ya wilaya yako. Hauna haja ya kwenda Dsm kufuata mzigo wako.Mkuu kwa sisi wa mikoani mfano iringa tufanyaje ili kuagiza mizigo njee na itufikie salama bila kuja dar
Usumbufu, labda usema unachelewa kukufikia. Mfano kama upo wilayani,mzigo unatrack na unaona umeshafika Dsm. Sasa kutoka Dsm kuja ulipo unachelewa sana. Halafu hata kutrack kwa kutumia mtandao wa posta inakuwa taabu hata ukiingiza ile namba uliyopewa ni majanga hakuna utakachojibiwa. Hapo utapata taabu ya kwendakwenda posta kuangalia sanduku lako kama kuna ujumbe. Wakati mwingine posta wenyewe wanakupigia simu kukupa taarifa ya kifurushi chako.Mkuu unaweza ukawa na ufahamu kidogo kuhusu watu wenye masanduku ya posta mikoa mingine tofauti na Dar, je kuna usumbufu wowote wa mzigo kufika au?
sasa kuliko utumie aliexpress, si unaorder kitu kwa agents kama bashley, exa etc wapo wengi tu na mzigo unachukua siku tatu hadi dar, electronics kama simu ni siku tisa, mi siwezi tumia aliexpress or ebay nk.. kwasababu ya muda, unaagiza kitu kinakufikia ushasahau.. yan miezi miwili niwe nasubiri kitu,, mmmh hapana
Mkuu naomba unijulishe njia za kufanya malipo aliexpress na ebay unazozitumia.Watanzania tuache uoga mimi nimesha agiza simu zaidi ya tano kwa kupitia alixpress tena sina sanduku la posta natumia posta makao makuu Mzigo ukifika naenda kuchukua
Nimeagiza vitu vingi sana na vimefika bila shida yoyote
Muhimu ujue ku track mizigo yako ili ikifika posta utambue mapema na kuifuatilia
Maana ukitegemea kupata msg kutoka posta mara nyingine msg hazifiki
Hizo ni baadhi ya simu nilizo agiza na zikafika bila shida yoyote
Kuna item zaidi ya 30 nimeagiza na zimefika
View attachment 1144110View attachment 1144111
Mkuu naomba msaada wa kufahamu naona ya kufanya malipo kununua bidhaa ebay. Nilijaribu kuorder bila kufanya malipo nikaambiwa nchi yangu haipo miongoni nchi zinatakiwa kutumwa mzigo.Elimu nzuri sana hii, binafsi natumia M-pesa mastercard. Ni rahisi sana na haina usumbufu wa aina yoyote. Changamoto ya kuagiza vitu Aliexpress zipo, kwa mfano binafsi nilishatumiwa mzigo feki kama mara 2. Hivi sasa naagiza Amazon na Ebay tu baada ya hizo changamoto.
hapa ndipo nilipokuwa najiuliza kwa nini watu wasitumie m pesa master card mpaka wasumbuke na makadi ya bankUlizwa swali lolote kuhusu M-pesa master card nitakujibu.
Ninakaribia mwaka sasa toka nianzw kutumia M-pesa master card na hususan Aliexpress.
Ebay kuna baadhi ya wauzaji huwa hawaleti kwenye baadh ya nchi kama east africa so njia nzur ni kutumia forwading agents kama myus, shipito or stacry wapo wengi sana ila hzo ni chache.Mkuu naomba msaada wa kufahamu naona ya kufanya malipo kununua bidhaa ebay. Nilijaribu kuorder bila kufanya malipo nikaambiwa nchi yangu haipo miongoni nchi zinatakiwa kutumwa mzigo.
mkuu,hv format ya shipping addess ipoje,msaada tafadhali.Mkuu soma hapa utapata picha ya swali lako pia hii itawasaidia na wengine pia
*Kwanza download application ya alixpress kwenye simu yako
* application ikifunguka jisajili kwa kuweka email yako and password zako kumbuka kuhifadhi password vyema ili ikitokea ume unistall hiyo application ukija ku download upya irudi account yako ileile ya awali
*Ingia kwenye application yako ya alixpress kwenye setting tafuta sehem pameandikwa
Shipping adresse hapo ingiza Adress yako
Kwamba unaitwa nani, unakaa wapi, Namba zako za simu zilizopo hewani, post code yako. N.k kisha save
* Tafuta kitu unachotaka kununua ukipata fuata process za kununua hapo hapo kwenye ulipoonea hicho kifaa itakuonyesha pia na shipping cost
Fuata maelekezo hayo ya kununua yatakupeleka mpaka kwenye namna ya kununua hapo utatumia credit card yako ya Visa au Master card au M pesa master card
salio lako litatumwa kwa alixpress baada malipo yako kuwa confirmed
Seller ataanza ku process mzigo wako
Mara nyingi ni 5days then atautuma kwa shipping company
* mzigo wako utatumwa na selller kwa kupitia shipping company uliyo chagua
Kazi yako hapo ww itakuwa ni kungojea mzigo ufike posta kulingana na estimate period iliyowekwa ...
Kumbuka seller atakutumia tracking number hvyo utakuwa una u track mzigo wako kujua maendeleo yake mara nyingi baada ya seller kutuma mzigo huwa inachukua siku 21 au zaidi
Huwa na tumia track24.net hii huwa inanionyesha maendeleo yote ya mzigo wangu mpaka unapo fika posta
* Mm nachukuliaga mizigo yangu posta mpya hapa dar es salaam
Kwahiyo ww utaenda makao makuu ya posta ya mkoa uliopo
Au unaweza kutumia sanduku lako la posta kama unalo ni muhimu kufuatilia mapema mzigo wako posta usingojee mapaka wakutumie msg maana mara nyingi msg zao hazifiki kwa wakati hii inaweza kupelekea mzigo kupotea au kupatataabu kuupata
* kwa mizigo midogo huwa hamna charge zozote ila pale posta mara nyingine huwa wana tukata 1500tsh hata kwa mizigo midogo midogo hii sijajua ni ya nini wajuzi wata dadavua
Vile vile mzogo ukiwa mkubwa zaid ya 0.5kg jamaa TRA wanatakaga 20% ya bei uliyonunulia mzigo hii nazungumzia kwa mizigo midogo dogo
Ila kwenye simu sijawah kukatwa pesa huwa na chukua free
*kumbuka Jina utakaloandika kwenye shipping address liwe ndio hilo hilo lililopo kwenye kitambulisho chako
Maana siku ya kwenda kuchukua mzigo lazima uende na kitambulisho chako cha kura, taifa, au driving license..
Kama una swali karibu