PreGE2025 Stepehen Wasira: Rais Samia amejenga hospitali na zahanati, mkombozi mkubwa kwa wanawake

PreGE2025 Stepehen Wasira: Rais Samia amejenga hospitali na zahanati, mkombozi mkubwa kwa wanawake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mzee Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2024
Posts
234
Reaction score
284
IMG-20250330-WA0003.jpg

==
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa hususan ujenzi wa hospitali na zahanati ambazo ni mkombozi mkubwa kwa wanawake.

Wasira amesema hayo jana Machi 29, 2025 Itilima mkoani Simiyu alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na CCM wilayani humo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tunataka na akina mama mchangamkie zile zahanati ili mtokane na mambo yaliyopita ya nyuma, mambo ya wakoloni ambapo kulikuwa hakuna zahanati na hospitali, leo tuna hospitali, leo tuna zahanati na kwa kweli vipimo vipo, kwa hiyo akina mama na ninyi mna deni na Rais ambaye ni wa kwanza mwanamke katika Tanzania. Jitokezeni muongoze kutoa kura nyingi utakapofika wakati wa uchaguzi," amesema.

== ==
 
...ukikutana na wale jamaa wana drive zile boda za kijan zmeandikwa SSH ...wanasema tunakula na kipofu...ivi kati ya samia na wao nani kipofu....
 
Mbona kuna heading mbili kama mnataka kuongelea nyomi za bila kubebwa na Mafuso angalieni Iringa leo.
 
wanadai wamefanya yote hayo lakini bado wanaogopa uchaguzi HURU na wa HAKI
 
Back
Top Bottom