==
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa hususan ujenzi wa hospitali na zahanati ambazo ni mkombozi mkubwa kwa wanawake.
Wasira amesema hayo jana Machi 29, 2025 Itilima mkoani Simiyu alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na CCM wilayani humo.
"Tunataka na akina mama mchangamkie zile zahanati ili mtokane na mambo yaliyopita ya nyuma, mambo ya wakoloni ambapo kulikuwa hakuna zahanati na hospitali, leo tuna hospitali, leo tuna zahanati na kwa kweli vipimo vipo, kwa hiyo akina mama na ninyi mna deni na Rais ambaye ni wa kwanza mwanamke katika Tanzania. Jitokezeni muongoze kutoa kura nyingi utakapofika wakati wa uchaguzi," amesema.