Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Nishati Azindua Mpango wa Miaka Minne wa Masuala ya Jinsia wa TANESCO

Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Nishati Azindua Mpango wa Miaka Minne wa Masuala ya Jinsia wa TANESCO

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
STEPHEN BYABATO NAIBU WAZIRI WA NISHATI AZINDUA MPANGO WA MIAKA MINNE WA MASUALA YA JINSIA WA TANESCO

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amezindua Mpango wa miaka minne wa masuala wa jinsia wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao utawezesha masuala mbalimbali ikiwemo kuboresha mfumo wa upatikanaji na utoaji wa takwimu za jinsia katika Shirika hilo

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 30/3/2023 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Mhe. Balozi Mwanaidi Majaar na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande.[/HEADING]

“Tumezindua programu hii ambayo itahamasisha na kusimamia haki na usawa wa watu wote katika eneo la kazi na mwisho wa siku tunataka TANESCO iwe mfano wa mashirika mengine katika kusimamia na kutekeleza masuala ya jinsia.”amesema Byabato

Amesema kuwa, katika mpango huo masuala mbalimbali yatakayofanyika ni pamoja na kuwa na sera ya Taasisi ambayo itaelekeza mambo mengi ikiwemo utaratibu kuwajengea uwezo vijana wa kike ili waweze kuingia katika kazi za kitaalam ambapo utaratibu huo utahusisha kuwatoa vijana katika vyuo na kuwapeleka kwenye Shirika na kuwapa mafunzo na baadaye kupewa ajira.

Jitihada nyingine zitakazofanyika ni kuhakikisha nafasi mbalimbali katika shirika zina wanawake na vijana wa kike sawa na wanaume sambamba na kuwapeleka shule ili waongeze uelewa na ujuzi utakaowawezesha kumudu nafasi mbalimbali shirikani.

Ili mpango huo wa jinsia ufanyike kwa ufanisi, Naibu Waziri ameiagiza TANESCO kuanzisha kitengo maalum kitakachokuwa kikishughulikia masuala ya jinsia katika Shirika hilo ikiwemo malalamiko yanayohusu jinsia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande amesema kuwa, suala la usawa wa kijinsia linapewa kipaumbele na TANESCO na tayari Shirika hilo limeshaweka mikakati ya kuhakikisha wanaongeza viongozi na wafanyakazi wanawake katika Shirika na kwamba Bodi pamoja na Wizara ya Nishati inawaunga mkono katika suala hilo.

WhatsApp Image 2023-03-31 at 12.52.25(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-31 at 12.52.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-31 at 12.52.24.jpeg

 
Hii Project yake, wmepanga Kula Billion ngapi ?. Maana sahizi ma Waziri Kila Wizara wanakuja na tuprogram uchwara twa kula Hela.

Sasa Hawa wameona Mama anajificha kwenye uanamke, nao wamekuja na kaprogram ka uanaumke.

Kazi yoyote Ile ya kiutendaji/kiuongozi inahitaji UBORA WA MTU na sio Jinsia, mambo ya Jinsia matokeo yake ndio yametuletea kitu inaitwa Wabunge wa viti maalumu ambao kiuhalisia HAWANA UMUHIMU ZAIDI YA KULA HELA TU, nyie wenyewe ni mashahidi, katika wale Viti Maalum, ni wachache Sanaa ambao wanajitutumua kuonyesha Uwezo wao !!.

Watu wanahitaji Umeme, hawataki porojoporojo za ohoooo sahizi tuna wafanyakazi 49% Wanawake .

Raia wanataka Umeme wa uhakika

Kwahiyo TANESCO mmekua tawi Dogo la Wizara ya Jinsia ?.

Shame on you TANESCO
 
Hiyo picha moja hapo juu, ina uhusiano wowote na mpango mkakati wa kutekeleza agenda hiyo?

Naona kivuli cha mtu mme mmoja, upande wa pili watu wake wawili, ndo uwiano unavyopaswa kuwa kwenye agenda yao?

Kila la kheri na ujinga wao!
 
STEPHEN BYABATO NAIBU WAZIRI WA NISHATI AZINDUA MPANGO WA MIAKA MINNE WA MASUALA YA JINSIA WA TANESCO

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amezindua Mpango wa miaka minne wa masuala wa jinsia wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao utawezesha masuala mbalimbali ikiwemo kuboresha mfumo wa upatikanaji na utoaji wa takwimu za jinsia katika Shirika hilo

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 30/3/2023 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Mhe. Balozi Mwanaidi Majaar na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande.[/HEADING]

“Tumezindua programu hii ambayo itahamasisha na kusimamia haki na usawa wa watu wote katika eneo la kazi na mwisho wa siku tunataka TANESCO iwe mfano wa mashirika mengine katika kusimamia na kutekeleza masuala ya jinsia.”amesema Byabato​

Amesema kuwa, katika mpango huo masuala mbalimbali yatakayofanyika ni pamoja na kuwa na sera ya Taasisi ambayo itaelekeza mambo mengi ikiwemo utaratibu kuwajengea uwezo vijana wa kike ili waweze kuingia katika kazi za kitaalam ambapo utaratibu huo utahusisha kuwatoa vijana katika vyuo na kuwapeleka kwenye Shirika na kuwapa mafunzo na baadaye kupewa ajira.​

Jitihada nyingine zitakazofanyika ni kuhakikisha nafasi mbalimbali katika shirika zina wanawake na vijana wa kike sawa na wanaume sambamba na kuwapeleka shule ili waongeze uelewa na ujuzi utakaowawezesha kumudu nafasi mbalimbali shirikani.​

Ili mpango huo wa jinsia ufanyike kwa ufanisi, Naibu Waziri ameiagiza TANESCO kuanzisha kitengo maalum kitakachokuwa kikishughulikia masuala ya jinsia katika Shirika hilo ikiwemo malalamiko yanayohusu jinsia.​

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande amesema kuwa, suala la usawa wa kijinsia linapewa kipaumbele na TANESCO na tayari Shirika hilo limeshaweka mikakati ya kuhakikisha wanaongeza viongozi na wafanyakazi wanawake katika Shirika na kwamba Bodi pamoja na Wizara ya Nishati inawaunga mkono katika suala hilo.​

View attachment 2571988View attachment 2571989View attachment 2571990

Mh...!!!
Kuna ka harufu ka yale mambo pingwa yale
 
Wanaacha Mambo ya msingi wanaelemea kwenye upuuzi tu , hao wataalam mlio nao kupatiwa haki Yao ya kupandishwa baada ya kumaliza masomo imekuwa shida mwaka na nusu sasa. Mnategemea walio nyuma Yao watapata hamasa ya kujiendeleza kweli kielimu ? pale wajinga wanapojadili ujinga Kwa maslahi yao inakuwa shida sana.
 
Sasa badala wajishughulishe na dhima kuu ya nishati, hasa umeme, wanavamia mambo ya ushoga. Hii nchi ina tatizo gani hasa?
 
Kila Wizara inatafuta kichaka Cha kupiga. Jinsia kwenye umeme ndio Nini?. Mambo ya jinsia peleka kwa Dr Gwajima waziri wa jinsia na watoto.
 
Back
Top Bottom