Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Mtu mwenyewe mpaka anakufa alikuwa kama zombie, kitu kidogo sana kuhusu afya yake hajui mpaka ameparlyse then anakuja kuandika maujinga tumuelewe😅.

Kijana kujua kingereza usitafute loopholes na kujifanya unajua mambo mengi ,behind unaonekana zuzu kwa vile hauna elimu Wala factual informations za kuprove jambo ambalo huyo aliyetoa kashindwa kujitibu na kutafuta solution maana alikuwa kama zombie mpaka anakufa..😅
 
If you haven't read Hawking, and you are interested "A Brief History of Time: From The Big Bang To Black Holes" (attached) is a good start.
Mungu alimleta na sasa akamtwaa
 
Logical non sequitur.

Mtu kutokujua jibu la swali lolote si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Ni uthibitisho tu kwamba mtu hajui jibu la hilo swali.
 
Hii ni kauli ya imani, hujathibitisha Mungu yupo.
Big Bang ni mlipuko uliotokana na either joto ama msuguano. Na mlipuko wowote mkubwa ni deadly fire and. heat.

Inawezekanaje baada ya mlipuko wenye moto na joto kali kukaja kuibuka viumbe ambavyo haviwezi kumudu hata joto la nyuzi 90 vikaishi?

Theories za hawa wanasayansi hazina proof yeyote.

Mungu aliumba mfumo ambao umeweka uwiano ktk kila jambo. Mimi nimeona malaika na majini. Nao ni viumbe au hallusinations?
 
Logical non sequitur.

Mtu kutokujua jibu la swali lolote si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Ni uthibitisho tu kwamba mtu hajui jibu la hilo swali.
😅😅How comes are you arguing instead of learning?

Sikiliza ndugu yangu unatakiwa ujifunze kwanza ukianza kwa kubisha bila ya kujua jambo ,surely hautokuja kujua kitu chochote ...Jifunze utambue ukweli sehemu zote halafu chambua kwa kushirikisha ubongo wako.

"God has created the sun and the moon moving in precise circulation " rejea surah ar rahman. Unapata facts za maana kuliko porojo zq binadamu ambaye hata kesho yake haijui.😅
 
Hii logical fallacy inaitwa Logical non sequitur.

Hata kama Big Bang ni uongo na theories zote za wanasayansi hazina proof yoyote, hilo si proof ya kuwapo Mungu.

Unasema theories za wanasayansi hazina proof yoyote, halafu na wewe unatoa madai ya kuwapo Mungu bila proof yoyote.Huoni kwamba unarudi palepale pa kutoa madai bila proof?

Naweza kukubishia kwamba theories za wanasayansi zilizosema kwamba watatengeneza internet ya kukuwezesha wewe kutuma ujumbe huu hapa JF zina proof kwamba zipo sahihi, na proof ni huu ujumbe wako kunifikia, but that is another matter.

Hata kama nikikukubalia theories za wanasayansi hazina proof yoyote - for the sake of argument , huoni kwamba na wewe pia unadai Mungu yupo bila ya kuwa na proof yoyote na hivyo huna tofauti na hao wanasayansi unaowasema hawana proof yoyote?

Nimekuomba unipe proof Mungu yupo. Hujanipa proof.

Unatoa kauli za imani tu.
 

Kwa hiyo paragraph ya kwanza pekee tayari unamrudisha Kiranga palepale kwenye hoja yake ya msingi

"Mungu muweza wa yote angeweza kuumba ulimwengu ambao hauna magonjwa/mauaji wala mabaya hayawezekani kutokea. Kutokea Kwa hayo yote ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo"
 
Sasa kama unaamini hayo magonjwa yameumbwa na Mungu basi yupo.!!

Baadhi ya magonjwa binadamu wanayetengeneza maabara ila wanafuata mfumo ule ule wa magonjwa yaliyokuwepo enzi za zamani , hata sasa hao binadamu wanaweza kutengeneza jua lao .
Swali je ni nan alitengeneza lile juu la asili na akaliwekea ratiba ya kuchomoza na kuzama?

Magonjwa yapo kwa vile ni mfumo wa Mungu aliyoweka hapa dunian, ukichana na haya tunaoamini yanatengenezwa maabara yapo ya kihistoria miaka kibao nyuma je haya yalitokea wapi?
 

Wapi nmesema naamini magonjwa yameumbwa na Mungu!? Je kutojua aliyetengeneza jua na kuliwekea ratiba ya kuchomoza na kuzama inamthibitisha vipi mungu?
 
Wapi nmesema naamini magonjwa yameumbwa na Mungu!? Je kutojua aliyetengeneza jua na kuliwekea ratiba ya kuchomoza na kuzama inamthibitisha vipi mungu?
Kama sio yeye niambie nan ana ratibu kuzama na kuchomoza kwa jua ?

Nan analeta magonjwa?
 
Mr Kiranga, Mungu hakulazimika kuumba. Mungu kuumba uhai ni zawadi tu ambayo ameitoa. Wanaoikubali wanachukua jukumu wanaishi katika muda, wanaokataa wanakufa.

Uhai unahitaji uwepo, uwepo unahitaji muda na muda unahitaji mabadiliko. Mabadiliko ndiyo yanayohitaji utofauti wa hali zinazowezekana kuwepo.

Narudia hakulazimika kuumba ulimwengu. Ila alipoamua kwamba nitaumba(Super duper Freely Willingly) basi hicho kililazimisha 'uwepo' uhitajike na ndio muda ukahitajika na ndio mabadiliko yakahitajika na ndio utofauti ukahitajika. Ndio hali hizo tunaziita uzuri na ubaya relatively (kwa kuzilinganisha na kuzitofautisha). Ni kama tu jotoridi tunapokaa na kusema katika chumba negative to 5 celcius ni baridi na ni 'ubaya' af tukasema labda 27 to 32celcius ndio nzuri halafu 45 huko ni ubaya hozo ni relatives tu.

Amin amin nakuambia Muumbaji angeumba joto lililopo na linalowezekana kuwepo ni 27 celcius tu ili kuepusha hayo majoto mengine 'mabaya' basi ulimwenguni usingewahi kuja kusikia wazo/concept ya jotoridi popote! Wala ubaya wake, wala uzuri wake. In effective jotoridi, joto na baridi vingekuwa havipo.

Chukulia huo ni ukuaji wa nchi na mafunzo ya kuishi kama nchi. Katika ukuaji wa nchi na ustaarabu wa dunia nzima. Nchi na watu wake wanapitia hali ambazo zinawafundisha kuzitatua na kuufikia ustawi wake binafsi na wa dunia na ulimwengu kwa ujumla.

Labda Kiranga chukulia ukuaji wa mtoto. Je utoto na mambo yake ni mabaya ambayo hayatakiwi kuwepo? Yaani Mungu muweza yote ungemuamini kama tu ataumba mtu akiwa mzima tu labda wa miaka 32 tu. Na abakie hapohapo ndio utafurahi? Maana utoto una mabaya mengi;
Kubanwa mbavu kutoka nje
Kuumizwa na hewa oksijen inapotanua mapafu
Kuumizwa na misindano
Kutembelea magoti yanachubuka
Kutokujua mengi mara ujikate mara ujin'gate
Utasa na ugumba (mtoto hazai ujue)....
...
... Uzee nao una shida nyingi;
Kuna kushindwa kukojoa
Misuli kutokuwa na nguvu.
Mifupa na mvi
Udhaifu wa mishipa na viungo vya mwili.

Sasaa; mtu wa miaka 80 labda ni taabu, na wa miaka mitano pia ni taabu so unaweza kuargue watu wote wawe na miaka 32. Lakini ukiweza kuargue hivyo sasa itabidi huyo wa 32 asibadilike, so asiongezeke muda wala kupungua. Na ili kusiwe na mabadiliko ya hali na basi na muda (usiende) usiwepo dunia yote. Kwa kufanya hivyo my friend unakuwa umeuua uhai na uwepo as we know it!
 
Swali moja dogo unaliruka. Labda hulielewi vizuri. Swali hili linazaa mengine mengi.

Je, Mungu huyu unayemsema yupo, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na ubaya, maumivu etc, au hakuweza?

Kama aliweza kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya na maumivu, kwa nini kaamua kuumba ulimwengu huu ambao unaweza kuwa na mabaya na maumivu?

Kama hakuweza kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya na maumivu, je, ni kweli ana uwezo wote?

Unaposema mabadiliko ndiyo yanaleta uzuri na ubaya, unakuwa hujajibu swali la msingi. Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao una uwepo na mabadiliko, lakini hauna na hauwezi kuwa na ubaya na maumivu?

Kuhusu utoto, Mungu ameshindwa kuumba ulimwengu ambao una watu wakapitia utoto bila ya kupitia mabaya?

Kuhusu uzee, Mungu ameshindwa kuumba ulimwengu ambao una watu wakapitia uzee bila ya kupitia mabaya?
 
Je, Mungu huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na ubaya, maumivu etc, au hakuweza?
Sasa ninalijibu kila wakati na jibu ni hili hapa👇

Mungu angeweza kuamua kuumba, au kutoumba.

Na akishaumba anaweza kuamua kuweka humo viumbe wenye hekima na wasio na hekima. Wenye kuchagua na wasiochagua. Wote akawapa akili, wengine.... sorry vingine asivipe akili vyote anaweza na amefanya.

Sasa katika viumbe yule mwenye akili na hekima ndiyo ataamua kutenganisha vile anavyoona yeye vinafaa na atavyoona havifai, vizuri na vibaya.

Mwisho mwishoni tofauti zote hizi zipo kwako wewe mwenye kutumia akili kuamua kuwa huu ni UBAYA huu ni UZURI kwa hekima zako mwenyewe.
 
Kuhusu utoto, Mungu ameshindwa kuumba ulimwengu ambao una watu wakapitia utoto bila ya kupitia mabaya?
Chukulia huu mfano: mtoto akiambiwa 'we mchumba wangu' anaumia na analia. Mtu mzima analilia kuolewa na kuoa. Akikosa mchumba analia.

Je Mungu kwa kumfata mtoto aumbe ulimwengu ambao uchumba na ndoa haviwezekani kabisa?

Au Mungu kwa kumfuata mtu mzima aumbe ulimwengu ambao kila kiumbe mtoto kwa mtu mzima hadi mawe na miti iwe na wenza wake siku zote miaka yote?

Je hiyo siyo jehanaamu kwa wale timu KATAA NDOA?

Huoni kama ni akili kubwa kuweka uwezekano wa yote ili kila mmoja ajichagulie mazuri yake na mabaya yake kwa wakati wake na mwisho kwa yote aweze kuishi maisha?
 
Hujajibu swali.

Je, Mungu aliwea kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya wala maumivu?

Aliweza au hakuweza?
 
Hujajibu swali.

Je, Mungu aliwea kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya wala maumivu?

Aliweza au hakuweza?
Kiranga hiyo ni kitu rahisi saaaaaana kufanya.

Hata sasa asipobadilisha kingine chochote katika ulimwengu huu.

Kikafanyika kitu kimoja tu, kuondoa hekima na akili kwa kila kiumbe mwenye akili basi vuup, uzuri na ubaya unabakia kuwa myth ambayo hakuna mtu tena hata wa kuin'gamua anymore.

Wote tunakuwa kama mawe, lichomwe jua sawa, lisagwe na nyundo sawa, liyeyushwe na volcano sawa, liwepo sawa, lisiwepo sawa. In fact none of nothing makes any sense...... in fact even sense doesnt exist to begin with.
 
Kwa mujibu wako. Kati ya Mungu na mtoto, nani alianza kuwapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…