Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Natumaini alikufa kifo chema.
Mungu awepo asiwepo bado watu wanahitaji kusali na kuabudu ili wawe na afya ya akili na mwili.

Tafiti zinaonyesha watu wanaoamini uwepo wa mungu wa afya njema zaidi kuliko wapagani
 
Kwanza kabla ya kuendelea nithibitishie kuwa anashindwa kuzuia mabaya?maana umetumia kauli kuwa Anashindwa kuzuia.

Mungu mnamsema mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Ameumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya.

Kwa nini?

Kama hajashindwa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya (na hivyo kuzuia mabaya kuwepo), kwa nini kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo?

Kataka tu?

Kama hajashindwa kuzuia mabaya, kataka tu mabaya yawepo, mtasemaje ana upendo wote? Mungu mwenye uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo, halafu asiumbe ulimwengu huo, akaumba huu wenye kuweza kuwa na mabaya, utasemaje ana upendo wote?

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo?
 
Natumaini alikufa kifo chema.
Mungu awepo asiwepo bado watu wanahitaji kusali na kuabudu ili wawe na afya ya akili na mwili.

Tafiti zinaonyesha watu wanaoamini uwepo wa mungu wa afya njema zaidi kuliko wapagani
Unaelewa kwamba hata Wapagani wanaamini Mungu, na kutoamini Mungu ni tofauti na upagani?
 
Unaelewa kwamba hata Wapagani wanaamini Mungu, na kutoamini Mungu ni tofauti na upagani?
Dah mkuu mimi nina hofu ya Mungu.Na nikienda kwa ibada napata amani na matumaini yanayotokana na hofu zangu za maisha.Katika maisha haya ni bora uwe mkristu, muislamu na hata budha kuliko kuwa mpagani.

Iwapo wewe unapata amani kwa kumsoma marehemu Hawkings ambaye alikuwa ni mpagani basi ni vizuri pia.
 
Hujajibu nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.
 
Sina nia ya malumbano mkuu.Naheshimu maamuzi yako ya kuwa mpagani.
Wewe ngumbaru hata maana ya neno mpagani hujui, halafu ukipewa darasa la bure hufundishiki.

Mpagani bibi yako.
 
Mbona haueleweki? Unazungumzia Ulimwengu kuruhusu mabaya au Mungu kuruhusu mabaya yatokee? Hoja yako hasa ipi kuhusu mabaya tatizo ni ulimwengu au Mungu?
 
Mbona haueleweki? Unazungumzia Ulimwengu kuruhusu mabaya au Mungu kuruhusu mabaya yatokee? Hoja yako hasa ipi kuhusu mabaya tatizo ni ulimwengu au Mungu?
Ulimwengu umekuwepo bila Mungu kuuruhusu uwepo?
 
Hilo neno asilani umelitoa wapi? Hebu nukuu niliposema hivyo.

Ila ni vizuri kuzungumzia imani.
Unajua kusoma habari kwa ufahamu na kuchambu sentensi kimantiki?
 
Ulimwengu umekuwepo bila Mungu kuuruhusu uwepo?
Haujajibu nilichouliza,hoja yako ni ulimwengu kuruhusu mabaya au Mungu kuruhusu mabaya kutokea ulimwenguni.

Halafu ukiniuliza kwamba ulimwengu unaweza kuwepo bila Mungu kuruhusu? Maana yake Mungu sio muumbaji au muundaji wa huo ulimwengu.
 
Tatizo watu mnabishana Mungu yupo mara hayupo lakini nadhani ilitakiwa kujua kwanza Mungu ni nini? Au Mungu ni nani? I'm sure kwenye maana ya Mungu ndo kuna contractions otherwise tungejua Mungu ni nini then Je, Mungu ndo chanzo cha yote au pengine tunaamini/tumetengeneza Mungu wetu mwingine ambaye siye cha vyote.
 
Haujajibu nilichouliza,hoja yako ni ulimwengu kuruhusu mabaya au Mungu kuruhusu mabaya kutokea ulimwenguni.

Halafu ukiniuliza kwamba ulimwengu unaweza kuwepo bila Mungu kuruhusu? Maana yake Mungu sio muumbaji au muundaji wa huo ulimwengu.
Mungu kauumba/ kauruhusu ulimwengu kuwapo? Au ulimwengu umetokea bila kuumbwa wala kuruhusiwa kuwepo na Mungu?
 
Karibu kila nikijibu habari za Mungu naeleza kwamba ninaongelea Mungu "Mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote".

Imekuwa kama mantra sasa.

Hujaona?

Ukiongelea Mungu tu bila definition, hata Beyonce kuna watu wanamuita Mungu.

Na Beyonce yupo, kwa hivyo katika ubishi wa Mungu Beyonce yupo au hayupo, kwa definition ya Mungu ambayoinamfanya Beyonce kuwa Mungu, siwezi kubisha.

Halafu tatizo si definition tu, kama hapa nime define mara kibao, lakini ama hujasoma, ama umesoma hujaelewa.

Kuna watu washakula kiapo, wao Mungu awepo,asiwepo, wanabisha kwa kusema yupo tu.

Sasa hao utasemaje tatizo ni definition?
 
Unajua kusoma habari kwa ufahamu na kuchambu sentensi kimantiki?
Neno asilani umelitoa wapi? Maana hakuna nilipotumia hilo neno wala hakuna nilichosema chenye kumaanisha hilo neno.

Hakuna niliposema kuwa wewe umesema kuwa hutozungumzia imani.
 
Karibu kila nikijibu habari za Mungu naeleza kwamba ninaongelea Mungu "Mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote".

Imekuwa kama mantra sasa.

Hujaona?
Umeulizwa Mungu ni nini unaeleza sifa za huyo Mungu badala ya kuelezea Mungu ni nini?

Ukiulizwa paka ni nini utaanza kutaja rangi ya paka na manyoa yake.
 
Neno asilani umelitoa wapi? Maana hakuna nilipotumia hilo neno wala hakuna nilichosema chenye kumaanisha hilo neno.

Hakuna niliposema kuwa wewe umesema kuwa hutozungumzia imani.
Kama sijasema sitaki kujadili imani asilani, utaanzaje kushangaa nikijadili imani popote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…