Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Huo ni mfano tu nilikupa rejea ile post utaelewa ,huwezi read between the lines basi siwezi kukusaidia.

Ndio mawazo yangu,yako si ya Hawkings.
Ipo nini? Na unajuaje ipo haionekani na si mawazo yako tu?
 
SOMA VIZURI UELEWE UMEKIMBIA MASWALI KIBAO,UNAJAZA TU THREAD BILA MISINGI YEYOTE.
 
Siyo mimi nimejiweka.

Kwa dhana ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, viumbe wake wote ni viumbe wapendwa.

Akiwepo kiumbe mmoja tu ambaye si mpendwa, hata shetani, basi huyo Mungu hana upendo wote.
Sasa nilipokuuliza kuwa wewe nae ni mpendwa wa Mungu ulikuwa unakataa nini?
 
Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Ndiyo maana unakimbilia kuwa mwanamazingaombwe ya kulazimisha mambo.
Ili kitu kiwepo siyo lazima ukithibitishe. Mfano, hata wewe huwezi kuthibitisha Big Bang ilitoka wapi na kwa nini ilitokea kama ilivyotokea na si vinginevyo na huwezi kuthibitisha pia kama waasisi wa Big Bang theory kuna eneo walikosea au la maana hujui na mimi sijui. Hivyo, kuna mambo mengi hatuwezi kuyathibitisha, lakini kutoyathibisha kwetu siyo ushahidi kuwa hayapo. Whether tuthibitishe au la, kama yapo, yapo na kama hayapo, hayapo.
 
Sawa.

Lakini kuna vitu havithibitishiki kwa sababu si kweli, havipo.

Kwa mfano, mtoto aliyezaliwa na mama hawezi kuthibitisha kwamba yeye (mtoto) ni mama mzazi wa mama yake.

Sasa tutajuaje huwezi kuthibitisha Mungu yupo, ila yupo, na si kwamba huwezi kuthibitisha Mungu yupo, kwa sababu hayupo?

Hususan kwa sababu habari nzima ya Mungu kuwepo ina contradiction, kama habari ya mtoto aliyemzaa mama yake mzazi mwenyewe?
 
Hakuna anayeamini kwa sababu ya uthibitisho.
Kuamini unaweza kuamini uongo wowote ule.

Ndiyo maana kwangu si jambo la muhimu.

Swali la muhimu ni, je, unaweza kuthibitisha?

Hujaweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha.
 
Nimemfuatilia sana kiranga kwa kina nikabaini kuwa ni mgonjwa wa akili,anaumwa "Schizophrenia Paranoid", ni ugonjwa mbaya sana,anaweza akabeba mawe na kupiga watu na kisha akakana na kudai waliomwona wathibitishe hata kama alionwa na halaiki ya watu.
Hapa tunahangaika na kichaa kabisa
 
Ikiwa ulichoandika hapa ni kweli, na mimi kweli nina ugonjwa wa akili, huo pia utakuwa ni ushahidi zaidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao viumbe wake wangeweza kuumwa ugonjwa wowote.

Habari zako za kunipa mimi ugonjwa, zinaongeza ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Hazioneshi kwamba Mungu huyo yupo.

Unaelewa hilo?

Pia,

Unaelewa kwamba watu wenye utaalamu wa kuagua ugonjwa wa "Schizophrenia Paranoid" maadili yao ya kazi yanawakataza kuagua watu mitandaoni na kuwasema mitandaoni, na hivyo, wewe hata hujakaribia utaalamu unaotakiwa kujua kuagua ugonjwa huu na maadili ya kazi za watu wenye mafunzo na uwezo wa kuagua ugonjwa huu?
 
Kama kuamini si jambo muhimu kwako basi pia masuala yote yenye kuhusu imani sio muhimu pia,sasa ajabu unajadili suala la Mungu ambalo ni suala lenye kuhusu kuamini kitu ambacho sio muhimu kwako.

Sio kuamini tu ndio unaweza kuamini uongo wowote bali hata mahakami huko watu wanatoa ushahidi wa uongo na kukubalika.
 
Sina tatizo na yeyote anayeaema anaam8ni Mungu yupo.

Hiyo ana haki ya kikatiba kuamini hivyo, hata mimi nitatetea haki yake ya kuamini anavyotaka.

Nina tatizo na anayesema anajua, kweli, kwa fact, kwamba Mungu yupo.

Wewe unaamini tu au unajua kweli kabisa kwa fact Mungu yupo?
 
Suala la uwepo wa Mungu linajulikana ni suala la imani kwa maana watu wanaamini Mungu yupo,sasa kwani kuna mtu anayesema suala la kuwepo Mungu si imani? Maana wewe umesema hauna tatizo na wenye kuamini kwa hivyo wote unajadiliana nao humu ni wale wasiochukulia hili suala ni imani.
 
Kwa hiyo wewe huna hakika Mungu yupo, unaamini tu?
 
Kwa hiyobwewe huna hakika Mungu yupo, unaamini tu?
Mimi hakika ninayo kwa maana sina mashaka ila suala la uwepo wa Mungu ni la imani na hivyo linahitaji kuamini,ndio maana nakuuliza kwani kuna mtu anayesema hili suala la uwepo wa Mungu sio imani?
 
Mimi hakika ninayo kwa maana sina mashaka ila suala la uwepo wa Mungu ni la imani na hivyo linahitaji kuamini,ndio maana nakuuliza kwani kuna mtu anayesema hili suala la uwepo wa sio imani?
Huwezi kuwa na hakika, halafu hapo hapo ukawa una imani, imani ni kutokuwa na hakika, unaelewa hilo?
 
Upepo hatujawahi kuuona ila tunasema upo kwa kuwa tunaona tu matendo yake kama kupuliza kupeperusha n.k
Vipi wewe unayesema MUNGU hayupo kwa kuwa tu eti hajawahi kuonekana ijapokuwa tunayaona matendo yake
Hapana anasema kama tunajua kisayansi jinsi upepo unavyotengenezwa, kiasi kwamba tunaweza tengeneza upepo artificial kwa science ya kibinadamu.

Au mvua, ambayo inanyesha kiasili tukiamini ni Mungu amefanya, leo kwa science iliyopo hata wewe ukifundishwa unaweza ukaitengeneza na hakuna nguvu nyingine inayoweza kuizuia mvua yako isinyeshe.

Tsunami,tetemeko,ukame,miamba tunajua kisayansi inavyotengenezwa au jinsi ya kuibomoa.

Kama hayo yanafanyika kibinadamu na kwa kufuata science principles, kwanini tuendelee kuamini uwepo wa Mungu mwenye uweza?
It is a matter of time Wanasayansi wapo karibu zaidi na ukweli kuliko fumbo la uwepo wa Mungu, ambalo tunakatazwa kuhoji baadhi ya maswali juu yake.
Mfano Nani alimuumba Mungu
 
Yapo maswali mengi tu

Mfano

Wanasema hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na nchi

swali,: huyo mungu alikua anaishi wapi wakati anaziumba mbingu na nchi?
 

1. Kama hivyo ndivyo, naomba uthibitishe kwa nini Big Bang ilitokea na ilitokana na nini.
2. Naomba uthibitishe pia kabla ya kutokea Big Bang, kulikuwa na nini.
 
Yapo maswali mengi tu

Mfano

Wanasema hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na nchi

swali,: huyo mungu alikua anaishi wapi wakati anaziumba mbingu na nchi?
Ukiwa na mwaka mmoja tarehe 6 December SAA 8 na nusu unajua ulikuwa wapi?
 
Unajua kuwajibu mkuu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…