Ikiwa ulichoandika hapa ni kweli, na mimi kweli nina ugonjwa wa akili, huo pia utakuwa ni ushahidi zaidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.
Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao viumbe wake wangeweza kuumwa ugonjwa wowote.
Habari zako za kunipa mimi ugonjwa, zinaongeza ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Hazioneshi kwamba Mungu huyo yupo.
Unaelewa hilo?
Pia,
Unaelewa kwamba watu wenye utaalamu wa kuagua ugonjwa wa "Schizophrenia Paranoid" maadili yao ya kazi yanawakataza kuagua watu mitandaoni na kuwasema mitandaoni, na hivyo, wewe hata hujakaribia utaalamu unaotakiwa kujua kuagua ugonjwa huu na maadili ya kazi za watu wenye mafunzo na uwezo wa kuagua ugonjwa huu?