Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Twende taratibu

1. Wakati unajibu hoja yangu umeijibu kwa free will au ulikuwa preprogrammed kuijibu?

Kwa ninichoices ziishie kwenye freewill na pre programmed tu?

Why is this a binary question? Where does the mutual exclusivity come from?

Sikujibu kwa freewill, sikuchagua muda wa kujibu. Sikuchagua level ya education ya anayeniuliza.

Ningekuwa na freewill kweli, ningekuwa najadiliana na watu wenye elimu nzuri wanaoweza kuuliza maswali mazuri.

Sasa wewe leo unaniuliza maswali ambayo nilishayapita mwaka 1996 wakati nasoma kitabu kinaitwa "The Philosophy of Religion: An Anthology".

Trust me, ningekuwa na freewill nisingekuwa najadiliana na wewe, ningejadiliana na Alvin Plantinga.

 
Not only hime many scientist wanaweza kusema chochote basi kwasababu wananplatform za kuongelea mitakwimu hakuna wa kuwakatalia maana ilinukatae unaTakiwa ukafanye tafiti... hata hapa wako wengi tu watuache na imani zetu

Sidhani kama ni lazima sana kufanya utafiti ili uweze kuwakatalia hao wanasayansi.

Kama unajiamini na kama unaona wanachoongea haki make sense, unawakatalia tu.

Mfano, mimi bado sijashawishika na maelezo ya theory ya evolution.
 
Sidhani kama ni lazima sana kufanya utafiti ili uweze kuwakatalia hao wanasayansi.

Kama unajiamini na kama unaona wanachoongea haki make sense, unawakatalia tu.

Mfano, mimi bado sijashawishika na maelezo ya theory ya evolution.
Kukatalia mbona unaweza kuwakatalia bila hata research kabisa.

Kuna watu wa flat earth society wanakataa kwamba dunia ni tufe, tunao hata hapa, wanasema dunia ni bapa.

Kwangu mimi, uzuri wa sayansi si kwamba ina majibu yote, au inahodhi ukweli wote, au haiwezi kushindwa.

La hasha. Sayansi haina majibu yote, haihodhi ukweli wote na inaweza kushindwa.

Uzuri wa sayansi ni kwamba, ni mfumo unaokubali kwamba, hauna majibu yote, hauhodhi ukweli wote na unaweza kushindwa.

Kukubali huku ndiko kunakoipa nguvu sayansi kujiongeza kuwa mfumo bora zaidi, kwa maana kama watu wanasema kitabu fulani ni cha Mungu na hakina makosa (dini) basi hawawezi kutafuta majibu zaidi ya yaliyomo kwenye kitabu hicho. Na kama kitabu kina makosa, watayapamba na kuyasheherekea kama ukweli mzuri sana. Matokeo yake wanadumaa.

Zamani watu waliamini kuwa kuna ether, magwiji wakawa hawana shaka kabisa kuhusu hili, wakaanza kufanya majaribio huku wakijua tu hapa tunathibitisha tulichosema, wengine wajue.

Wakaja kupata matokeo tofauti na mategemeo yao. Lakini kile kitendo cha kufanya majaribio, sehemu ya sayansi, kiliwashurutisha kuujua ukweli.

Kwa zaidi soma hapa chini kwenye Wiki.


Kwenye sayansi, leo hii ukigundua makosa ya msingi katika Darwin's evolution, au katika Einstein's Relativity, ni rahisi sana mwakani ukapata nishani ya Nobel, unazawadiwa na kusheherekewa na jumuiya ya wanasayansi kwa kuwaonesha makosa yao.

Kwenye dini ukienda Saudi Arabia, ukasema Mtume Muhammad alikosea hapa na pale, utapigwa jambia ufe haraka sana.

Hii tofauti, mfumo mmoja (sayansi) uko wazi na unakumbatia kukosolewa, mfumo mwingine (dini) uko kihafidhina na hautaki kukosolewa, ndiyo inayonifanya nione mfumo wa sayansi ni bora, hata kama kuna mambo haujapatia sawa.

Kwa maana, with time, mfumo wa sayansi umejijengea utaratibu wa self correction na convergence towards a more accurate truth.

Kwa upande mwingine, dini inadumaza maendeleo ya kutafuta ukweli.

So, tukifuata sayansi, kama kuna aspects za evolution zina makosa, with time, makosa yataanikwa tu. Watu wanatoa ma Ph.D kwa watakaoonesha makosa.

Kwenye dini, makosa yanakubalika, ukiyaanika, unaambiwa unakufuru na unatengwa na jamii nzima inayokubali dini hiyo, unaweza hata kuuawa.
 

Nayakubali maelezo yako.

Pia, si ni wewe ambaye umewahi kusema humu kuwa si lazima mtu ujue square root ya 2 ni nini ili kukataa kwamba siyo 9 [i’m paraphrasing]....?
 
Upo sahihi mkuu

Kudos
 
Nayakubali maelezo yako.

Pia, si ni wewe ambaye umewahi kusema humu kuwa si lazima mtu ujue square root ya 2 ni nini ili kukataa kwamba siyo 9 [i’m paraphrasing]....?
Exactly.

Ukishajua square root ya mbili ni ndogo kuliko mbili, jibu lolote lililo zaidi ya mbili utajua si la kweli, hata kama hujui square root ya mbili ni nini.

Sasa dini inatuambia square root ya 2 ni 9 (contradiction). Tukiuliza imepatikanaje? Mbona hesabu zimeharibiwa hapa? Tunaambiwa akili ya Mungu huwezi kuijua wewe.

Ukiuliza, mnajuaje huyo Mungu yupo na si hadithi tu? Hakuna anayeweza kuthibitisha Mungu yupo.

I look at the search for truth as either diverging from truth or converging to truth.

Dini ina contradictions zinazoonesha ina diverge kutoka ukweli. Sayansi, hata kama haina picha kamili ya ukweli leo, inaelekea kwenye direction ya ukweli na ina narrow down on that.

Ndiyo unakuta kwamba, Isaac Newtons equations are still true, all non relativistic speed/mass objects can use Newtonian equations and function just fine.

Lakini akaja mwamba mwingine Einstein akatuonesha kwamba, tukikaribia speed of light in a vacuum, au tukiwa kwenye regions za heavy gravity, Newtonian equations zinakuwa hazitoshi, inabidi tutumie Einsteinian Relativistic equations.

Tumekuja kupata uelewa zaidi unaochimba deep zaidi. Sina tatizo na mfumo unaojiongeza hivyo.
 

Tatizo la waumini wengi, hususan hawa wanaochangia humu, ni wanaonekana kama hawajui 'imani' ni nini katika muktadha wa dini.

Kwa sababu, kama wangekuwa wanajua 'imani' ni nini katika muktadha wa dini zao, sidhani kama hii mijadala ingekuwa inajirudia rudia hivi.

Binafsi naliona ni jambo jepesi sana lakini kwa wengine linaonekana kama ni jambo gumu sana.
 
Mkuu,hapa umeua kila kitu.

Hata hivyo wanywa bendera za dini najua Cognitive dissonance haitawaacha salama, kama huyu hapa chini.

Pangua hizo contradiçtions hata kama ni kwa tafsiri unayoitaka wewe na si kujichekelesha.
MI NADHANI SWALA LA MUNGU HAYUPO MNEGENZA KUHUBIRIA FAMILIA ZENU KWANZA NA WATOTO WENU.... MANA UMMA HAUPOTOSHWIKI KWA HILO.. GOD IS ONE.
 
Ni uwezo gani ambao unahitajika katika kufanya uovu? Kwa sababu wewe umesema ukifanya ambalo ni zuri kwako lakini baya kwa mwengine huo ndio uovu,sasa hapo ni uwezo gani unaohitajika kufanya uovu? Sijui kama unanielewa.
Swali langu mpaka sasa hujalitolea majibu!.Naomba nisikujibu chochote mpaka wewe unijibu.
 
Have those who disbelieved not considered that the heavens and the earth were a joined entity, and We separated them and made from water every living thing? Then will they not believe?
— Quran 21:30
Here is your Big Bang from Holly Quran 1400 yrs ago......so now u know. Atheists na Materialists tunawaangalia kwa jicho la huruma sana kwa upotevu wao juu ya uwepo wa ALLAH muumba wa mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo..muweza wa yote, mjuzi wa yote mwenye khabari na kila jambo ulijualo na usilolijua...ama hakika sifa zake ni nyingi.
 
Huyo hata swali hajalielewa.

Hajaona contradiction

Amekubali contradiction.

Na hajaelewa kwamba, kukubali contradiction kunavunja msingi mzima wa dhana ya kuwepo Mungu.
"contradiction" Ndiyo nini?.
Ukianacho wewe kuwa ni contradiction, kwangu mimi siyo contradiction.
Unawezaje sasa kunifanyia maamuzi ya kwamba hiki kipo hivi ili hali kwangu mimi hakipo hivyo?.
 
Mkuu majibu yake yana contradictions tele vile tu hamuelewi...
Usomi wenu mi unanishangaza sana.Yaani mtu anajua kuwa mahindi ni chakula kikuu Tz, lakini mahindi hayo hayo ni chakula kikuu cha mifugo huko ulaya!

Alafu anashindwa kujua kuwa kilicho contradiction kwake, siyo contradiction kwa mtu mwingine!. Ajabu sana.
 
Nianze kwa kusema nitafafanua hoja zako unazobainisha kama uongo na contradiction ya biblia.
Hapa nataka ufahamu jambo moja, ambalo kimsingi wengi hatulielewi vizuri kuhusu Mungu.
Ni vigumu kuzungumza dini bila kuhusisha, ama Mungu au miungu. Dini inafungamana moja kwa moja na Mungu au miungu. Ieleweke wazi kuwa miungu ni uongo, udanganyifu na upofu.
Kwa sababu hii ya dini, yaani Mungu, tumekuwa na biblia. Kwa kifupi, biblia ni tauhidi ya dini.
Kwahivyo, siyo sahihi kuelewa kwamba, biblia ndiyo dini. Siyo sahihi kabisa. Inayofanya dini ni liturujia ya sadaka. Liturujia ndiyo dini, ambapo liturujia ya sadaka(tambiko) ndiyo hufanya dini. Kama hakuna ibada ya sadaka hakuna dini.
Kwahiyo, biblia ni mafundisho ,ambayo hatahivyo, uhai wake umo katika liturujia ya kufanya ibada ya sadaka.
Tukijenga msingi wa dini katika biblia hatuwezi kuwa sahihi kwa kuwa kinachofanya dini siyo biblia bali taratibu za liturujia ya sadaka.
Tufahamu wazi kuwa, dini imekiwepo tangu mwanadamu alipoanza kuwepo. Dini ndiyo ilianza kisha mtu. Biblia ambayo tunayo hii leo imeandikwa miaka ya hivi karibuni. Lakini kwa maelfu ya miaka mtu amekuwa akifanya ibada ya sadaka-amekuwa na dini.
Kwahiyo, biblia haiwezi kwa kiasi chote kuwa ndiyo ukweli wote wa Mungu. Lakini ukweli wote wa Mungu unadhihirika katika taratibu za liturujia ya sadaka. Na hivyo hutuwezi kujenga dini katika msingi wa biblia.
 
Usitake kunitoa katika reli ya mjadala.

Nimekuuliza kama biblia ina contradictions, ukabisha.

Nimekuwekea contradictions unarukaruka kama kuku aliyechinjwa kichwa na kuachwa ajirushe.

Unakubali biblia ina contradictions?
 
Usitake kunitoa katika reli ya mjadala.

Nimekuuliza kama biblia ina contradictions, ukabisha.

Nimekuwekea contradictions unarukaruka kama kuku aliyechinjwa kichwa na kuachwa ajirushe.

Unakubali biblia ina contradictions?
Umebainisha ambazo kwako unaita contradiction ya biblia. Na mimi nimesema hapo kwenye post kwamba nitakujibu. Hivyo, sijakutoa kwenye reli. Nitajibu hizo unazodai contradiction ya biblia.
Lakini hapo nime-post msingi wa ambao unatufahamisha kuelewa ukweli wa dini.
 
Hujaweka msingi wowote zaidi ya kuweka madubwasha na mazingaombwe ya abracadabra.

Ungejibu contradictions zote, moja baada ya nyingine, kwa ufasaha na ufanisi, ungeweza kusema umweka msingi.

Sasa biblia mara unaitetea haina contradiction, mara unaikana kwa kusema si dini, inaonekana hata wewe mwenyewe hujui umesimamia wapi.

Sasa huo ndio msingi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…