Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Unafikiri mimi ndiye hakimu!.Mahakimu wapo hapa Jf. Ila kwa kukusaidia tu,rudi kwa mwanao wa chekechea akupe tofauti uliyoshidwa kuiona wewe.
Mkuu mtu mwenye upendo kwa wote automatically ana upendo wote. Na kuhusu mtoto kwa bahati mbaya sina bado...
 
Mkuu mtu mwenye upendo kwa wote automatically ana upendo wote. Na kuhusu mtoto kwa bahati mbaya sina bado...
Huyo ana assume tu kwamba kila mtu ana mtoto.

Kama anavyo assume Mungu yupo.
 
Huyo ana assume tu kwamba kila mtu ana mtoto.

Kama anavyo assume Mungu yupo.
Ajabu mkuu!! Mtu anakubali mungu wake anawapenda watu wote lakini anakataa hana upendo wote. Matokeo yake anakimbilia mambo ambayo hata siyo msingi wa hoja husika..
 
Ajabu mkuu!! Mtu anakubali mungu wake anawapenda watu wote lakini anakataa hana upendo wote. Matokeo yake anakimbilia mambo ambayo hata siyo msingi wa hoja husika..
Hawajui kwamba manyota waliyompa huyo Mungu wa kutungwa ndiyo yanayomuelemea na kumuangusha.
 
MI NADHANI SWALA LA MUNGU HAYUPO MNEGENZA KUHUBIRIA FAMILIA ZENU KWANZA NA WATOTO WENU.... MANA UMMA HAUPOTOSHWIKI KWA HILO.. GOD IS ONE.
Huna mamlaka ya kutupangia pa kuanza kuwaelimisha watu juu ya uongo wa dini, kama ambavyo hatukuwapangia nyie pa kuanzia kupotoshea watu juu ya uwepo wa Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na mwenye upendo mkuu.

After all huwezi kuzipangua contradictions alizowawekea mkuu Kiranga hapo juu.

Na zaidi ya yote huwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu "hewa" wenu.

Kama unadhani unaweza tiririka ili nzengo yote ikucheke kwa namna unavyojiharishia huku unaenda!.
 
HAHAHH KWANZA UKIWAAMBIA UMMA LIVE SWALA HILO ..LAZMA WATILIE SHAKA IQ YAKO KAMA MIMI NILIVO NA SHAKA NA IQ ZENU..

AFTER ALL MUNGU ANAJIDHIRISHA KILA SIKU SIO KWENYE BIBLIA TU..HATA MTU ASIE WAI SIKIA HABARI ZA DINI..MOYON MWAKE ANAFAHAM KUNA KMUNGU..SIO NYIE WALEVI MNAFAHAM FIKA YUPO ILA KIBURI TU ..HAHAHAHH
 
HAHAHH KWANZA UKIWAAMBIA UMMA LIVE SWALA HILO ..LAZMA WATILIE SHAKA IQ YAKO KAMA MIMI NILIVO NA SHAKA NA IQ ZENU..
Siku zote mwehu huwa ana mashaka na IQ za walio wazima.

Yaani anajiona yeye na matendo yake ndiyo sahihi kuzidi wengine sababu ya kuchunguza appearance za watu badala ya hoja zao.

Huna tofauti na watu wa dizaini hiyo,sababu umeshindwa kujadili hoja,umehamia kujadili IQ za watu,huna lolote.

Pangua hizo contradictions kwanza iwapo kweli una uelewa japo kidogo.

AFTER ALL MUNGU ANAJIDHIRISHA KILA SIKU SIO KWENYE BIBLIA TU..
Wapi huko kwingine?

Unaweza kupataja?

HATA MTU ASIE WAI SIKIA HABARI ZA DINI..MOYON MWAKE ANAFAHAM KUNA KMUNGU..
Ni kwa watu wasiojua kufikiri sawasawa kama ulivyo wewe.

Hata hivyo hakuzifanyi fikira zenu kuwa ndiyo sahihi.

Mnahitaji elimu ya msingi ktk kujitambua.

Unajua watu wengi pia kabla ya kupata elimu ya msingi (formal or informal) huwa wanadhani dunia ni bapa.

Pamoja na hayo mawazo ya wengi, hawaifanyi dunia iwe bapa kweli.

Dunia ni duara regardless wengi wanafikiri kinyume chake.

SIO NYIE WALEVI MNAFAHAM FIKA YUPO ILA KIBURI TU ..HAHAHAHH
Sisi kuwa walevi ni ushahidi mwingine wa kutokuwepo Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Maana angekuwepo asingeumba Ulimwengu ambao walevi kama Mimi naweza kuwepo halafu na wengine kama nyie mkawa si walevi.

Huo ni upendeleo, kitu ambacho kinakwenda kinyume na sifa ya Mungu ya kuwa na upendo mkuu kwa wote.

Unaweza ukaniambia kwa nini Mungu aliumba dunia hii yenye uwezo wa kuwepo walevi wakati alikuwa na uwezo wa kuumba iliyo bora zaidi kiasi cha walevi kutowezekana kuwepo?
 
Mtu anakulazimisha uwe unafahamu kitu ambacho siyo tu umesema hukifahamu, bali pia umetoa sababu za kuonesha kwa nini hakikubaliki ambazo ameshindwa kuzijibu.

Yani maana yake mtu kashindwa arguments, anataka kutumia "brute force" kwenye mjadala.

Unaanzaje kumlazimisha mtu kwamba anafahamu kitu ambacho sio tu kasema hakifahamu wala hakikubali, bali pia kina contradictions ambazo hazijatatuliwa?
 

MUNGU KAMPA MWANADAMU FREE WILL... YAAN ANAWEZA KUCHAGUA ATAKAVYO...

KUACHA WALEVI NI KWAMBA ANAUPENDO NAO NDIO MANA HAJAWAFANYA CHOCHOTE ILA ANATAKA WAMGEUKIE YEYE..

..IVI USHAWAI KUJIULIZA KWANN WATOTP WADOGO WOTE WANAFAHAM MUNGU YUPO..YAAAN WOTE UNDER 18 WANAPJITAMBUA WANAFAHAM MUNGU YUPO DUNIAN KOTE... WEWE UNADHANI NI NADHARIA GAN HII YENYE NGUVU KIASI HIKI???? GOD ID REAL BRO
 
Ajabu mkuu!! Mtu anakubali mungu wake anawapenda watu wote lakini anakataa hana upendo wote. Matokeo yake anakimbilia mambo ambayo hata siyo msingi wa hoja husika..
Mkuu! Kuongeza au kupunguza katika neno la Mungu ni kosa.
Sasa narudia tena kwamba, andiko lisemalo UPENDO WOTE halipo.
 
MUNGU KAMPA MWANADAMU FREE WILL... YAAN ANAWEZA KUCHAGUA ATAKAVYO...
Wewe ulipewa free will ya kuchagua uzaliwe wapi,mwenye jinsia gani,na wazazi gani,wenye uwezo gani kimaisha,wenye magonjwa ya kurithi au laa,wakati gani na uwe na kipaji kipi?

Watu wanaozaliwa vilema nao walipewa free will na Mungu ya kuzaliwa na ulemavu huo ama walilazimishwa wawe hivyo kabla hata ya kuzaliwa?.

Unafikiri wanaozaliwa vipofu,viwete,viziwi wenye mitindio ya ubongo na waliopungukiwa viungo vya mwili huku wengi wao wakija kuishi maisha ya tabu, wangekuwa na free will wangechagua kuzaliwa hivyo?

Kama kweli free will ipo kwa nini tunatishiana mamoto na kuzamishana kwenye magharika ya Nuhu?

Kwa nini hiyo free will iwe ktk mema na mabaya tu na si kwenye kuchagua nizaliwe wapi na bila magonjwa ya kurithi kama ualbino,sickle cell,night blindness na ma kansa ambacho ndicho kitu cha muhimu zaidi?

Unaelewa hata maana halisi ya free will wewe?


KUACHA WALEVI NI KWAMBA ANAUPENDO NAO NDIO MANA HAJAWAFANYA CHOCHOTE ILA ANATAKA WAMGEUKIE YEYE
Kwa nini hakuumba dunia ambayo mlevi atamtii automatic na hasa kwa kuwa uwezo huo anao badala ya kusubiri huruma za mlevi?

Kwani angepungukiwa nini kwa kufanya hivyo?

..IVI USHAWAI KUJIULIZA KWANN WATOTP WADOGO WOTE WANAFAHAM MUNGU YUPO..YAAAN WOTE UNDER 18 WANAPJITAMBUA WANAFAHAM MUNGU YUPO DUNIAN KOTE... WEWE UNADHANI NI NADHARIA GAN HII YENYE NGUVU KIASI HIKI????
The same question apply to you,

Kwa nini watoto wadogo wengi kabla ya kuelimishwa wanafikiri jua ni dogo kiukubwa kulinganisha na dunia na si dunia kuwa ndogo kulinganisha na jua?

Ni nadharia gani hii yenye nguvu hivi kiasi cha kuwaaminishà watoto kwamba dunia ni kubwa kuliko jua?

Kupitia fikira hizo za kitoto ndivyo ukweli ulivyo kuhusu ukubwa wa jua na dunia?

GOD ID REAL BRO
Can you prove that The God exist real, and not just the products of your imagination only!?
 
Nimekuwekea contradictions unarukaruka kama kuku aliyechinjwa kichwa na kuachwa ajirushe.


Hii sentensi yako ina makosa ya kisarufi,uwe una hariri kwanza kabla ya kutuma.

".....kuku aliyechinjwa kichwa na ....". Ndio nini ? Hakuna Kiswahili cha namna hii.
 
Kwa hiyo nisubirie kwenda motoni siyo?
Yani Mungu mwenye uwezo wote, uwezo wote na upendo wote.

Anaweza kuumba ulimwengu wowote anaoutaka.

Ikiwamo na ulimwengu ambao mtu hawezi kwenda motoni.

Lakini Mungu akaamua kuumba ulimwengu ambao mtu anaweza kwenda motoni.

Kwa nini kaamua kuumba ulimwengu ambao watu wengi sana wataenda motoni na hakuamua kuumba ulimwengu ambao hakuna mtu atakayeenda motoni?

Sijapata jibu la swali hili.
 
Mtu anapinga uwepo wa Mungu anasema kabisa hakuna Mungu ila ajabu hoja anazotumia kutetea msimamo wake huo ni zile ambazo zinatumika na wapingaji wa vitabu vya dini ila wanaamini Mungu,na ndiyo maana utaona wakanaji Mungu na wapingaji wa vitabu vya dini huwa pamoja kushambulia waamini Mungu.
 
Inaweza kuwa huyu mungu ni Sadist..
 

Utakapokuja kuujua ukweli utaona ni kiasi gani hoja zako hizi za square root zilikua za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…