Huyo Kiranga amekuwa muoga sana siku hizi,unatakiwa umshajiishe aache uoga na asiwe anakimbia maswali.
Kitu cha pili fikiria hichi kitu
Tupo watu takribani , let us say kama ishirini kwenye majadiliano
Ni watu wa dini tofauti tofauti lakini katikati yetu kuna watu wawili hawaamini Mungu yupo
Kwa umoja wetu sisi watu kumi na nane wa dini tofaut tofaut si mwislamu si mkristo si mbudha si mnani yaan wote tukashirikiana kupinga wale watu wawili
Wale watu wawili wakaona isiwe tabu wakajitenga na sisi , tuliobaki tukaanza kuondoka kwenda sehemu
Katika maongezi yetu tukaanza kuwaponda wale jamaa , aah mafala sana wale hawaamini uwepo wa Mungu , kwa kweli tukawasema sana
Lakini mbudha akaibua hoja , hivi nyie wakristo na waislamu mungu wenu sio wa kweli ,, teh
Tukajitenga nae
Tukabaki wakristo na waislam , tukaanza kumponda mbudha , aaah yule jamaa ni multi orse jinga kabisa
Mara teh , sheikh akaibuka nyie mnaamini Allah
Wakristo wakaja juu , "we fala unasemaje
Kilichofuata ni mapigano ambayo hata hapa jukwaa la dini huwa tunayaona matusi kejeli , kati ya hizi dini mbili
Mara wakristo wakaenda njia yao huko walijitenga kinoma
Yaanu tukamkuta
Msabato
Mlokole
Mroma
Muanglican
Mpentecost
Mmoravian
Mluthet
Na wwngine wengi , ambao hawakuaminiana kabsa kuhusu mungu wanayemuabudu
Mara huku waislam nao wakajitenga
Nadhan unajua kuna makundi mangapi ya waislamu
Je unadhani , hilo la kujitenga linathababishwa na nini , kwa nini Mungu hakuamua kuwe na njia moja ya kumjua yeye
Usibishe hapa , unawakosoa sana wakristo jukwaa la dini
Je Mungu wao ni wauongo ?
Je wako ni wa kweli ?
Je tumwamini Mungu yupi ?
Kwa nini anajicontradict hivi
Kuna sehemu wanakula kitimoto
Mara huku hawali
Hapo ni kwa wakristo huku
Unadhani sababu ni ipi
Huo mtengano uliotokea kwa watu ishirini , je unaweza kuwa uthibitisho wa kwamba mungu yupo au hayupo ?!