Kuna kitu sikielewi..sawa yawezekana MUNGU hayupo ila kuna kitu nataka kuelewesha kama sio kufundishwa
Tunaenda kanisani ghafla katika maombi anatokea dada/kaka anapaza sauti anaruka juu anaongea maneno ya ajabu ajabu saingine analala chini na kuanza kutambaa kama nyoka..
Ghafla mchungaji/shekh akapofika hufanya maombi na kumtaja MUNGU na kila neno MUNGU likitamkwa inakua kama moto unachochewa lakini hadi mwisho muhusika huinuka na kuwa mzima.
Kama si MUNGU ni nani anaefanya mauponyaji ya namna hiyo?
Kiranga
Ushasoma kuhusu kitu kinaitwa "hypnotism"? Kama hujasoma, tafuta habari hizi zaidi.
Hypnosis is a mental state of increased awareness, suggestibility, and concentration that can be used as a therapeutic tool for many conditions.
www.verywellmind.com
Kimsingi, bado hatuelewi vizuri ubongo wa mtu unavyofanya kazi. Kwenye hypnotism, mtu mmoja anaweza kuwa controlled na mtu mwingine, bila hata kutumia habari za Mungu. Ni saikolojia tu.
Saikolojia ya watu wanavyofanya mambo katika crowd inaonesha kwamba ku control watu katika crowd ni rahisi, watu wana conform.
Nilikuwa naangalia comedy moja, comedian katunga habari ya uongo, anahadithia kama imetokea, akamuuliza mtu mmoja kwenye hadhara, uliisoma ile habari? Jamaa akakubali kaisoma. Akamuuliza uliisoma Washington Post au New York Times, jamaa akajibu Washington Post. Yani jamaa hakutaka kuonekana mshamba hajui habari mpya zinazoendelea. Hapo hapo yule comedian akamzodoa, akamwambia hiyo habari hujaisoma, acha uongo. Hujaisoma kwa sababu nimeitunga mwenyewe hapahapa sasa hivi. Mob psychology inamfanya mtu afanye mambo ya kijinga, ya uongo, akubali asichojua.
Pia kuna watu wanataka kuwa sehemu ya kitu kikubwa zaidi yao, wanajiaminisha kabisa kwamba wana mapepo (kwa kweli hatujui vizuri magonjwa ya akili, huenda pia wana magonjwa ya akili wasiyoyaelewa wanayaita mapepo). Kuna watu wametokea kuongea kwa lahaja tofauti kabisa (mfano Mmarekani aanze kuongea Kingereza kwa accent ya Uingereza). Hii hali inaitwa "Foreign Accent Syndrome". Soma zaidi hapa
https://en.wikipedia.org/wiki/Foreign_accent_syndrome
Kwenye sayansi kuna watu wanapona kwa kile kinachoitwa "placebo effect". Yani unaweza kugundua dawa ya ugonjwa leo, ukawa na group la watu 300, ukawapa dawa watu 150 kila siku (namba si za kitaalamu, angalia dhana na hoja tu) halafu watu wengine 150 ukawapa vidonge vinaonekana kama dawa, lakini ni vidonge vya geresha tu, havina dawa. Wwanasayansi wameona mara nyingi kati ya wale waliopewa vidonge visivyo na dawa, wakiamini ni dawa, kuna wanaopona nao. Kwa sababu ya imani tu.
Huwa natania kwa kusema Yesu aliposema "imani yako itakuponya" alikuwa anasema kweli, alikuwa anazungumzia "placebo effect"
pla·ce·bo ef·fect
/pləˈsēbō əˈfekt,ēˈfekt/
noun
- a beneficial effect produced by a placebo drug or treatment, which cannot be attributed to the properties of the placebo itself, and must therefore be due to the patient's belief in that treatment.
"orthodox doctors dismiss the positive results as a result of the placebo effect"
The mind can trick you into believing that a fake treatment has real results, a phenomenon known as the placebo effect. It's a real response to a fake treatment.
www.verywellmind.com
1.Kwa kweli, hatuelewi ubongo unavyofanya kazi.
2. Mimi sijawahi kukataa kwamba inawezekana Mungu yupo na ndiye chanzo cha haya
3. Mimi ninataka ushahidi wa kuonesha haya yanatokana na Mungu
4. Ushahidi huu haujatolewa
5. Watu wakiona kitu wasichokielewa, wanakimbilia kusema Mungu ndiye sababu, hata kabla uchunguzi wa kina
6. Kukimbilia huku kusema jibu ni Mungu, bila uchunguzi wa kina, ndiyo ninakukataa
7. Ulimwengu wenye magonjwa ya akili, mapepo, watu wanaopagawa etc una contradict dhana ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote mwenye uwezo wote na upendo wote
8. Tutafute maelezo na uthibitisho kuhusu vitu tusivyovielewa bila kuhusisha uchawi, mujiza, Mungu kwanza.
9. Si lazima ujue jibu sahihi ili ujue jibu fulani si sahihi. Ukijua square root ya mbili ni ndogo kuliko mbili, huhitaji kujua square root ya mbili ni nini ili kujua kwamba kumi si square root ya mbili.
10.Tusome zaidi historia, saikolojia, baiolojia, kemia, jiografia, fizikia na hisabati kutafuta majibu ya maswali magumu yanayotukabili.