Stephen Keshi kuinoa Azam FC

Stephen Keshi kuinoa Azam FC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
http://thesheet.ng/wp-content/uploads/2015/02/stephen_keshi-520x245.jpg

Kocha ambaye Yuko nje ya mkataba na timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi anaorodheshwa na club ya Azam ili kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa zamani wa timu hiyo yaani Joseph Omog .

http://jamboleo.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/OMOG.jpg

Mkameruni Omog pamoja na Kocha wake msaidizi yaani Ibrahim shikanda walitumuliwa jumatatu hii kutokana na matokeo mabovu katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.

Katibu Mkuu wa Azam Football club Idrissa Nassoro amesema club ya azamfc iko kwenye mazungumzo na makocha mbalimbali akiwamo Stephen Keshi ...alisema ,kitu ambacho azam inakiangalia ni cv za kocha na mafanikio yake katika michuano iliyopita.

http://timbuktoo.org/wp-content/uploads/2014/12/keshi116-300x200.jpg

Aliendelea kwa kusema " Bado tuko kwenye mazungumzo na makocha mbalimbali ila kuna nafasi kubwa ya kumpata kocha Stephen Keshi, kwa kuwa mazungumzo baina yeti sisi na yeye yanaendelea vizuri ....na mafanikio yake yaliyopita ni kitu ambacho kimetuvutia zaidi.
 
Atasaidia kulete uzoufumpya hapa kwetu japo atafukuzwa naye make Azam nao wameonekana kutompa kocha mda was kuisuka timu,kama wanaweza wakampata wakaa naye kwa misimu kama miwili liwe jua ama mvua naamini anaweza kuwasaidia
 
Ivi jamaa yukoje katika ngazi ya club, maana kwa upande wangu nimemshuhudia tu kwa super eagle.
 
Hivi CV yake at club level iko vipi? Kunoa National teams na clubs ni mitihani tofauti sana. Atafika hapa na kuanza kumlalamikia viwanja na waamuzi wetu wa Bongo. Na ataleiletea Azam wanaigeria wenzie. By the time wanamtimua atawachia zigo la wanaigeria!
 
Tatizo kubwa la virabu vya bongo huwa wanadhani hata uwe na wachezaji wa kuunga kunga madam unakocha mzuri tu, timu itakwenda vizuri!!! Ni ngumu azamu bwana hawana wachezaji wazuri wengi ni wale wale tu, sasa hapo huyo keshi atafanya nini? labda wampe pesa aingie sokoni, hiwezi kuchukulia kufundisha timu ya taifa ya Nigeria ambayo wachezajo wake wengi wanacheza ligi za zinazoeleweke na zenye ushindani, utegemee same results hapa kwetu. Ni SAWA NA MTU UNATAKA KWENDA PEPONI LAKINI KWENYE KUFA MUOGA.
 
Back
Top Bottom