Stephen Masele: Kusimamia haki si utovu wa nidhamu

Stephen Masele: Kusimamia haki si utovu wa nidhamu

Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amesema kusimamia misingi ya haki za binadamu asitafsiriwe kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Alisema hayo jana baada ya kutoka katika mahojiano na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu.

Masele ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa Bunge la Afrika (PAP) alihojiwa kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 5.34 asubuhi hadi saa 9.18 alasiri na kamati hiyo inayongozwa na mwenyekiti wake, Emmanuel Mwakasaka.

Baada ya mahojiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la utawala bungeni, Masele alisema anaamini kamati itamtendea haki huku Mwenyekiti Mwakasaka akisema baada ya kumaliza kumhoji na kupitia mahojiano hayo Watanzania watajuzwa.

Kamati hiyo ilimhoji Masele ikitekeleza agizo la Spika Job Ndugai alilolitoa Mei 16 alipolitangazia Bunge akimtuhumu mbunge huyo kwa utovu wa nidhamu na kumtaka kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiendelea na vikao vya PAP.

Chanzo: Mwananchi
...
 
Back
Top Bottom