Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameitaka Wizara ya Kilimo kufanya uchunguzi wa umiliki wa ardhi inayoshikiliwa na Mohammed Enterprises Ltd wilayani Rungwe, Mbeya, ili kuona kama kampuni hiyo imeshindwa kuiendeleza na kurudisha ardhi hiyo serikalini kwa matumizi mengine.
Wananchi wa Tukuyu, Rungwe, wamelalamika kuwa Mohammed Enterprises Tanzania Ltd inamiliki mashamba makubwa ya chai ambayo yameachwa bila uzalishaji kwa muda mrefu, hali iliyosababisha ardhi hiyo kugeuka mapori yanayovutia nyoka na wanyama waharibifu, huku wakazi wakikosa maeneo ya kulima.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza na wananchi katika ziara yake mkoani Mbeya, Wasira amesema CCM inaiagiza serikali kupitia Waziri wa Kilimo kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua stahiki.
"Sheria ya umiliki wa ardhi inasema ukipewa ardhi lazima uizalishe. Mashamba haya ya chai yakiacha kuzalisha, viwanda vya chai haviwezi kufanya kazi, na matokeo yake ni kudidimia kwa uchumi wa wananchi," amesema Wasira.