GE2025 Stephen Wasira: Ilani ijayo 2025 - 2030 CCM kuinua uchumi jumuishi kwa Watanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Mgombea Urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa Otoba 29, 2025, Dk. Samia Suluhu Hassan, atapigiwa kura nyingi kwa sababu wananchi wameiona kazi kubwa aliyoifanya kuleta maendeleo kwa miaka minne iliyopita.

Aidha, amesema Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-2030, imejikita kusimamia uchumi na kuhakikisha unawagusa wananchi katika kila sekta.

Wasira ameeleza hayo leo, Septemba 3, 2025, Simanjiro Mkoani Manyara akiwa katika ziara ya kuitafutia ushindi wa kishindo CCM kupitia Dk. Samia, wagombea ubunge na udiwani.
WhatsApp Image 2025-09-03 at 15.41.12_32ec3b9c.jpg
“Ndiyo maana tunaandika Ilani, ukitazama mafanikio yaliyopatikana wala sihitaji kutumia takwimu, maana Watanzania hata wa Simanjiro wanajua mafanikio yaliyofanyika hapa, wanajua kiwango cha vituo vya afya vilivyojengwa, wanajua madarasa yaliyojengwa hapa, wanajua majosho yaliyojengwa kwa ajili ya wafugaji, na juzi Mama Samia ametoa ruzuku kwa ajili ya kuchanja mifugo,” amesema.

Amesema wananchi wa Tanzania wanajua jitihada zilizofanywa na Chama, akitolea mfano Simanjiro alieleza kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya maji, lakini yanashughulikiwa kwa kiasi kikubwa.
WhatsApp Image 2025-09-03 at 15.41.13_e2799de2.jpg
“Kwa hiyo nimekuja kutoa wito kwa wananchi wa Simanjiro kuhakikisha wapigakura wote wanatoka kwenda kupiga kura, wasisahau, na wakumbuke kumpigia kura Daktari Samia Suluhu Hassan. Tukamilishe safu kwa mafiga matatu halafu tukimaliza tunawatuma kusikiliza Ilani.

“Ilani katika siku zinazokuja tunataka kusimamia uchumi wa watu wa Tanzania, kama ni wafugaji tunataka kuwasaidia wafugaji ili ufugaji wao uwalipe, kama ni wakulima tunataka kuwasaidia wakulima tuwape zana, tulete miradi ya umwagiliaji maji walime waondokane na umaskini, kama ni wavuvi tutawapa vifaa vya kuvua na tunaka kuanzisha viwanda kulingana na malighafi inayopatikana.

“Hapa Simanjiro malighafi yake ni mifugo, kwa hiyo ukitaka kuanzisha viwanda utaanzisha vya nyama,” alieleza.

Alisema kila wilaya itakuwa na viwanda vyake kutokana na mazao yanayozalishwa eneo husika, na kwamba hivyo ndivyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyosema shabaha ikiwa kuleta maendeleo kwa wote.

Alisisitiza kuwa, serikali inatumia fedha na gharama kubwa kwa wananchi wakiwemo wa vijijini kuhakikisha maisha yao yanazidi kuwa bora.

“Hivi hapa Simanjiro ambapo vijiji vyenu vipo kilometa 70 kutoka mjini nani alijua umeme utaenea mpaka ufike kijijini, lakini umefika vimebaki labda vitongoji tu. Vijiji vyote vya Tanzania vina umeme, tutaendelea kujenga vitu hivi kujenga uchumi lakini shabaha kubwa ni kusaidia uchumi wa mtu mmoja mmoja.

“Ndugu zangu nilitaka niyaseme hayo lakini kubwa kuliko yote ni kwamba lazima tushinde uchaguzi,” ameeleza.
 
Wako madarakani tokea miaka ya 70, kama wameshindwa miaka yote hiyo leo wataweza?
 
Yaani kama vile ndo wameingia Tanzania hivi karibuni kumbe wako tokea miaka 60+ iliyopita na yeye yumo serikalini 50+..
Vipi zile nyiuz za yeye na zile hela za mbegu waliishia wapi?
 
Miaka zaidi ya 60 madarakani leo ndio wamekuja na wazo la kuinua uchumi!!!? Yaani chama kile kile na bendera ile ile hata mwendo wao ni ule ule.
Hakuna uchaguzi ambao hakuwahi kuja na maneno matamu lakini mwisho wake ni mchungu sana. Bila mabadiliko oktoba 25 ni kukamilisha tu maelekezo.
 
Wako madarakani tokea miaka ya 70, kama wameshindwa miaka yote hiyo leo wataweza?
Vijana tupaswa kufanya kazi sio kulalamika Nasibu Diamond juzi kawaasa vijana..uko Ulaya pia wameanza mbali

China uchumi wake unategemea nguvu kazi ya vijana wake.!!
 
Back
Top Bottom