GE2025 Stephen Wasira: Ni jambo la aibu kwamba tunaishi na maji lakini hatuna maji

GE2025 Stephen Wasira: Ni jambo la aibu kwamba tunaishi na maji lakini hatuna maji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katika kampeni zinazoendelea, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, alisisitiza Sera ya Maji, akizungumza mbele ya wananchi wa Musoma Mjini.

Akitoa kauli yake, alisema: "Ni jambo la aibu kwamba tunaishi na maji lakini hatuna maji," kauli iliyolenga kuibua mjadala kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika eneo hilo.

Serikali kuu chini ya CCM, ambayo imeongoza nchi hii tangu uhuru, ilikuwa na jukumu la kuhakikisha usimamizi na upatikanaji wa maji kwa wananchi lakini Mzee Wasira ni kama alikuwa nje ya Chama hivi. Je, nani anahusika na usimamizi huo?

 
Mzee wa hovyo.
Amekuwa kiongozi kwenye chama na serikali chaajabu hata huko anakotokea hakuna cha maana.
Leo anajitukna kupitia maneno yake maana yake chama chake hakijafanya lolote for more than 60yrs.
Hivyo hakipaswi kushika dola
 
Eti kukamata "dora"

Unaikamata dola tena unaishi na maji na huna maji!

Hebu mpeni huyo dawa halafu apumzike.
 
Katika kampeni zinazoendelea, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, alizungumzia kwa msisitizo Sera ya maji, akitoa kauli hiyo mbele ya wananchi wa Musoma Mjini akisema "Ni jambo la aibu kwamba tunaishi na maji lakini hatuna maji"

Hayo maneno akamueleze mwenyekiti wake asituletee kelele. Hovyo sana hawa ccm
 
Back
Top Bottom