Pre GE2025 Stephen Wassira aihakikishia Marekani kwamba Uchaguzi ujao utakuwa ni wa huru na wa haki. CCM wanaogopa vikwazo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Tunaposema kuwa CCM inawaogopa zaidi wazungu kuliko wananchi na vyama upinzani tunamaanisha mambo kama haya.

Swali la kujiuliza, ni kwanini Wasira "anaihakikishia" Marekani Uchaguzi kuwa huru na wa haki?

Shotocan Lucas Mwashambwa naomba msaada kwenye swali langu

=============================================================

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, ameiambia Marekani kuwa uchaguzi mkuu wa 2025 utakuwa huru na wa haki.

Akizungumza Februari 20, 2025, na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Andrew Lentz, Wasira alisisitiza kuwa CCM inaendelea kujiandaa kwa uchaguzi huo huku ikizingatia amani na utulivu wa taifa.

Soma pia: Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Alimweleza Lentz kuwa CCM inatarajia kushinda kwa sababu imetekeleza ahadi zake za maendeleo kulingana na Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025.

Kuhusu mazungumzo na vyama vya upinzani, Wasira alisema chama kiko tayari, likiwa ni sehemu ya falsafa ya R4 ya Rais Samia Suluhu Hassan inayohimiza majadiliano ya kisiasa.

Your browser is not able to display this video.

Source: Azam News
 
Tume ileile????Leo nimeona Kwa macho yangu mkoa wa pwani wakiandikishwa wanafunzi wa form one na form two yaani miaka 12 ,13,14 CCM ni hatariiiiiiiiii
 
Kwa hiyo ulitaka asema kuwa uchaguzi utakuwa wa vurugu .na kwamba watu wajiandae kupigwa virungu mpaka wavunjwe miguu na kutegua viungo?😄😄
 
Hata Trump alipata kwa uchaguzi wa haki 😄
Dunia hii wanasiasa wote wanaelewa lugha moja tu likija suala la Kura
 


Huyo mzungu na akili zote haoni hiyo body language kuwa ina udanganyifu mwingi tu!
 
Hajasimzia?
Yaani Chama kimachoshiriki Uchaguzi kina toa uhakika wa uchaguzi huru na wabaki badala ya tume ya uchaguzi kusema hayo.

Mbombo ngafu.
 
Hajasimzia?
Yaani Chama kimachoshiriki Uchaguzi kina toa uhakika wa uchaguzi huru na wabaki badala ya tume ya uchaguzi kusema hayo.

Mbombo ngafu.
Ameshamgutukia hapo anamchora tu

Hizi ni Ghiriba za kisiasa
 

Attachments

  • 5811771-84b12f6d5ff81d807821a183416ac2ed.mp4
    648.4 KB
WanaCCM kwa UONGO ..bi Chura nae alisema vivyo hivyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024...HADAA
 
Balozi kafanya utalii wa fursa.......!!!?
 
Kwa tume hii hii? Uwepo uchaguzi wa huru na haki? Hapo alikuwa anamfurahisha Kwa maneno mazuri ndugu kaimu balozi lakini CCM hii ninavyoifahamu haiwezi kuruhusu uchaguzi huru na haki Kwa kuwa kamwe hawawezi kushinda bila makando kando
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…