Jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi kasi ya siasa ya mzee huyu wasira inavyozidi kushika kasi mzee huyu sasa amekuwa tishio ndani ya chama na nje ya chama kutokana na kuzungumziwa kwa mapana wahenga walisema mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.. ni kweli huyu mzee kwa sasa amekuwa akipasua akili za watu kwa umakini wake katika kazi.
Katika suala la urais idadi ya watu wanaomuunga mkono inazidi kuongezeka siku hadi siku ukitembelea group lake la facebuk lenye wafuasi zaidi ya 13000 ambao wanafuatilia na kumuunga mkono huyu mzee hivi majuzi akiwa na mkutano jijini mwanza kuhusiana na mambo ya kilimo cha pamba baadhi ya wadau walionesha nia ya kumsapot na kumuomba achukue fomu ya urais.