Stephen Wassira: Kada mkongwe wa CCM asiye na kashfa

Uchaguzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
914
Reaction score
171
Stephen Masato Wasira si jina geni kwa Watanzania, ni jina maarufu. Umaarufu wa Wasira ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu unatokana na mambo mengi.

Haya ndio yamenifanya nianzishe mpango maalum wa kumchunguza kihabari ili niwaoneshe Watanzania upande mwingine wa shilingi kuhusu Mwanasiasa huyo, lakini nakiri kuwa "nimeshindwa kumpata" Wasira katika hilo.

Huyu ndiye Wasira ambaye Mwaka jana aliwatahadharisha Vijana wasomi wa Vyuo Vikuu kutumia taaluma zao kupambanua ukweli na uwongo wa vyama vya siasa ili wasiendelee kuwa wateja wa siasa uchwara na "wachumia matumbo"

Nimeshindwa kumpata WASIRA aliyeyasema hayo katika kongamano lililofanyika mkoani Mwanza na kushirikisha vyuo mbalimbali mkoani humo kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania(SAUT).
Nimeshindwa kumpata kwani kati ya watu niliobahatika kuzungumza nao au niliosoma mandishi yao, hakuna aliyenipa kashfa hata moja inayomgusa Wasira tofauti na upungufu wa kawaida ambao hakuna mtu wa kawaida duniani anayeweza kuukosa.

Baada ya juhudi zangu kushindikana kumpata Wasira ndipo najiuliza "HUYU WASIRA NI MTU WA NAMNA GANI?"
Katika kumtafuta Wasira na dosari zake, nakumbana na Gazeti la Raia Mwema Toleo la 2677 la November ,2013 likiwa na kichwa cha habari kisemacho "Nani ni nani CCM?"

Katika Habari hiyo Gazeti linasema "Stephen Wasira anatajwa kuwa ni mwanasiasa mwenye uwezo wa kuendesha siasa za jukwaani, lakini pia ni mwanasiasa mwenye kupenda siasa za suluhu miongoni mwa wanachama wa CCM, akiwa pia mwiba kwa upande wa vyama vya upinzani kwa wepesi wake wa kujibu mapigo"

Linaongeza"Ingawa CCM haijawahi kuonja historia ya kuwa chama cha Upinzani lakini Wasira amewahi kuingia upinzani na kushinda uchaguzi wa ubunge kupitia NCCR-Mageuzi, akimbwaga aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba".

Christopher Gamaina, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri , anamtaja Wasira akisema "Sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Wasira ni usafi wa kimaadili ndani na nje ya Chama chake (CCM) kwa maneno na matendo ya maisha yake".
Gamaina anasema ," Pia Wasira anatajwa na watu wengi kwamba ni mtu mwenye msimamo imara katika vita dhidi ya Ufisadi ndiyo maana hana doa wala kashfa ya ufisadi, lakini kubwa zaidi anatajwa kama mmoja wa makada wenye utashi na ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani ya CCM na mwenye upeo mpana wa kuona mbali".

Mmoja wa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam aliyetoa maoni yake kwa sharti la kutotajwa jina wala cheo, anasema "Ukiachia nafasi walizopata kuwa nazo wenzake, kati ya wanaosemwa (anamaanisha kuutaka Urais mwaka 2015), Wasira ni msafi kuliko wote kwasababu sijawahi kusikia kashfa yake ni mtu mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya siasa na utawala.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa uchunguzi wa makala haya, WASIRA amepata kuwa Mbunge wa Mwibara (mwaka 1970-1975), Bunda (1985-1990),(1995-1996) na (2005-2010). Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,Wasira alichaguliwa tena kuliwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Bunda.

Taarifa zilizopatikana katika mtandao zinasema Wasira pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara (mwaka 1975 hadi 1982) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990 hadi 1991.

Habari hizo za kimtandao zinafahamisha kuwa kati ya mwaka 1982 na 1985, Wasira alikuwa Waziri Mwambata katika Ubalozi wa Tanzania Washngton DC, Marekani na kisha akawa Naibu Waziri wa Kilimo mwaka 1972-1975, na Serikali za Mitaa mwaka 1987-1989.

Kwasasa Wasira ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Mbunge wa Bunda mkoani Mara
November Mwaka jana , mmoja wa wachangiaji katika mtandao wa Jamii Forum(JF) aliandika kuhusu Wasira akisema "Huyu mzee namkubali sana ,kwanza hana makundi katika chama na mzee huyu namkubali pia katika hotuba zake zenye nguvu na ushawishi. Namkubali sana.."

Alipoulizwa kuhusu anavyowajua makada watatu wa CCM wanaotajwa kuhusu kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwaka 2015, yaani mawaziri wakuu wazamani, Frederick Sumaye, Edward Lowasa na Wasira, Mratibu wa ULINGO ambayo ni ASASI ya Umoja wa Wanawake katika vyama vya siasa vyenye Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Ave Semakafu, amesema, "Sijaona yeyote kati ya hao anayejali na kuhudumia kwa dhati makundi ya watu walio pembezoni".

"Wengi wanafanya siasa kavu tu za kuwapa vijana mipira na jezi, wakati wana matatizo magumu yanayowakabili kimaisha. Mipira sio tatizo la Watanzania . Wengine wanasema vijana wamekalia bomu la ajira, lakini hawaoi jawabu la tatizo hilo".

Anaongeza, "Rais Jakaya Kikwete ndiye amekuwa Mfano bora kwa kuyajali makundi yote ya Watanznia. Amejitahidi hata kuwa karibu na watu na kuweka usawa wa kijinsia.Mfano amejitahidi kuteua majaji wanawake ; ameonesha mfano wa kuinua vijana na wanawake hata katika ule mfuko ulioitwa "Mabilioni ya Kikwete" na kusidia Vijana kupitia mifuko mbalimbali hadi ngazi ya wilaya."

"Natamani kumpata Mwanasiasa huyu nayetajwa kuwa jasiri asiyeogopa wala kusita kufanya uamuzi mugumu kwa maslahi ya umma" Na nimwambie kimoja wanachosema watu wanaomsema vizuri kwamba zile chagamoto ambazo hajazishughulikia jimboni kwake Bunda, azifanyie kazi.

Nimejitahidi kumtafuta Wasira kwa siku tatu mfululizo nikabahatika "kumpata" kwenye dosari moja waliyonayo Mawaziri karibu wote wa Kikwete kuwa, hawapendi kupokea simu. Hapo nimempata na kumweka kwenye kundi la wabunge na mawaziri wenzake .

Tuachane na hayo; Nimemtafuta Wasira sikumpata, maana nilitaka nimjulishe kuwa kuna mmoja ameshauri afanye juhudi kubwa n haraka ili kukamilisha ‘juhudi zake' za kuondoa shida ya maji katika maeneo ya Nyamakokoto,Bunda stoo,Nyasura,Migungani na sehemu nyingine.

Bado naendelea "kumtafuta" Stephen Masato Wasira ili nijiridhishe iwapo kweli hana hata kashfa moja kama wanavyosema watu wengi. BADO NAENDELEA KUMTAFUTA.

Makala kwa Hisani ya Gazeti la Pata Habari.
 
Mhh mbona una mashairi kama ya mjomba? Amekupa copyright?
 
Issue haikuwa kuhama chama bali ajenda ilikuwa ni uwakilishi wa wananchi,wananchi wa Bunda walimhitaji na hakuwa na namna isipokuwa kwenda upinzani, anyway suala hili wanalifahamu zaidi wananchi wa Bunda ambao hawakuona uhaini wake, instead walimtema waziri mkuu "warioba" na kumchagua yeye hadi leo
kuwahi kutoka ccm na kujiunga upinzani ni kashfa kubwa kuriko zote ni zaidi ya kuuza utu,kusaliti nchi ni uhain
 
Tony, tofautisha maana ya Nchi na Chama cha siasa na shughuli zake zinavyoendeshwa.
Ukiwa na mtazao huo finyu walioko upinzani leo asilimia kubwa walianza wapi? nadhani hapo ukijitafakari utaona jinsi usivyotumia neno uhaini na maana yake halisi.

Hapa Maslahi ya nchi na Wananchi yanatazamwa kwa utumishi wa Mwanasiasa.

Wasira deserves credit for being faithful and royal to his country, since the first Mwalimu Nyerere Regime to the forth Regime of Jakaya Kikwete.
 
Stephen Masato Wasira si jina geni kwa Watanzania, ni jina maarufu. Umaarufu wa Wasira ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu unatokana na mambo mengi.

Haya ndio yamenifanya nianzishe mpango maalum wa kumchunguza kihabari ili niwaoneshe Watanzania upande mwingine wa shilingi kuhusu Mwanasiasa huyo, lakini nakiri kuwa "nimeshindwa kumpata" Wasira katika hilo.

Huyu ndiye Wasira ambaye Mwaka jana aliwatahadharisha Vijana wasomi wa Vyuo Vikuu kutumia taaluma zao kupambanua ukweli na uwongo wa vyama vya siasa ili wasiendelee kuwa wateja wa siasa uchwara na "wachumia matumbo"

Nimeshindwa kumpata WASIRA aliyeyasema hayo katika kongamano lililofanyika mkoani Mwanza na kushirikisha vyuo mbalimbali mkoani humo kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania(SAUT).
Nimeshindwa kumpata kwani kati ya watu niliobahatika kuzungumza nao au niliosoma mandishi yao, hakuna aliyenipa kashfa hata moja inayomgusa Wasira tofauti na upungufu wa kawaida ambao hakuna mtu wa kawaida duniani anayeweza kuukosa.

Baada ya juhudi zangu kushindikana kumpata Wasira ndipo najiuliza "HUYU WASIRA NI MTU WA NAMNA GANI?"
Katika kumtafuta Wasira na dosari zake, nakumbana na Gazeti la Raia Mwema Toleo la 2677 la November ,2013 likiwa na kichwa cha habari kisemacho "Nani ni nani CCM?"

Katika Habari hiyo Gazeti linasema "Stephen Wasira anatajwa kuwa ni mwanasiasa mwenye uwezo wa kuendesha siasa za jukwaani, lakini pia ni mwanasiasa mwenye kupenda siasa za suluhu miongoni mwa wanachama wa CCM, akiwa pia mwiba kwa upande wa vyama vya upinzani kwa wepesi wake wa kujibu mapigo"

Linaongeza"Ingawa CCM haijawahi kuonja historia ya kuwa chama cha Upinzani lakini Wasira amewahi kuingia upinzani na kushinda uchaguzi wa ubunge kupitia NCCR-Mageuzi, akimbwaga aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba".

Christopher Gamaina, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri , anamtaja Wasira akisema "Sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Wasira ni usafi wa kimaadili ndani na nje ya Chama chake (CCM) kwa maneno na matendo ya maisha yake".
Gamaina anasema ," Pia Wasira anatajwa na watu wengi kwamba ni mtu mwenye msimamo imara katika vita dhidi ya Ufisadi ndiyo maana hana doa wala kashfa ya ufisadi, lakini kubwa zaidi anatajwa kama mmoja wa makada wenye utashi na ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani ya CCM na mwenye upeo mpana wa kuona mbali".

Mmoja wa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam aliyetoa maoni yake kwa sharti la kutotajwa jina wala cheo, anasema "Ukiachia nafasi walizopata kuwa nazo wenzake, kati ya wanaosemwa (anamaanisha kuutaka Urais mwaka 2015), Wasira ni msafi kuliko wote kwasababu sijawahi kusikia kashfa yake ni mtu mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya siasa na utawala.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa uchunguzi wa makala haya, WASIRA amepata kuwa Mbunge wa Mwibara (mwaka 1970-1975), Bunda (1985-1990),(1995-1996) na (2005-2010). Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,Wasira alichaguliwa tena kuliwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Bunda.

Taarifa zilizopatikana katika mtandao zinasema Wasira pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara (mwaka 1975 hadi 1982) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990 hadi 1991.

Habari hizo za kimtandao zinafahamisha kuwa kati ya mwaka 1982 na 1985, Wasira alikuwa Waziri Mwambata katika Ubalozi wa Tanzania Washngton DC, Marekani na kisha akawa Naibu Waziri wa Kilimo mwaka 1972-1975, na Serikali za Mitaa mwaka 1987-1989.

Kwasasa Wasira ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Mbunge wa Bunda mkoani Mara.
November Mwaka jana , mmoja wa wachangiaji katika mtandao wa Jamii Forum(JF) aliandika kuhusu Wasira akisema "Huyu mzee namkubali sana ,kwanza hana makundi katika chama na mzee huyu namkubali pia katika hotuba zake zenye nguvu na ushawishi. Namkubali sana.."

Alipoulizwa kuhusu anavyowajua makada watatu wa CCM wanaotajwa kuhusu kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwaka 2015, yaani mawaziri wakuu wazamani, Frederick Sumaye, Edward Lowasa na Wasira, Mratibu wa ULINGO ambayo ni ASASI ya Umoja wa Wanawake katika vyama vya siasa vyenye Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Ave Semakafu, amesema, "Sijaona yeyote kati ya hao anayejali na kuhudumia kwa dhati makundi ya watu walio pembezoni".

"Wengi wanafanya siasa kavu tu za kuwapa vijana mipira na jezi, wakati wana matatizo magumu yanayowakabili kimaisha. Mipira sio tatizo la Watanzania . Wengine wanasema vijana wamekalia bomu la ajira, lakini hawaoi jawabu la tatizo hilo".
Anaongeza, "Rais Jakaya Kikwete ndiye amekuwa Mfano bora kwa kuyajali makundi yote ya Watanznia. Amejitahidi hata kuwa karibu na watu na kuweka usawa wa kijinsia.Mfano amejitahidi kuteua majaji wanawake ; ameonesha mfano wa kuinua vijana na wanawake hata katika ule mfuko ulioitwa "Mabilioni ya Kikwete" na kusidia Vijana kupitia mifuko mbalimbali hadi ngazi ya wilaya."

"Natamani kumpata Mwanasiasa huyu nayetajwa kuwa jasiri asiyeogopa wala kusita kufanya uamuzi mugumu kwa maslahi ya umma" Na nimwambie kimoja wanachosema watu wanaomsema vizuri kwamba zile chagamoto ambazo hajazishughulikia jimboni kwake Bunda, azifanyie kazi.

Nimejitahidi kumtafuta Wasira kwa siku tatu mfululizo nikabahatika "kumpata" kwenye dosari moja waliyonayo Mawaziri karibu wote wa Kikwete kuwa, hawapendi kupokea simu. Hapo nimempata na kumweka kwenye kundi la wabunge na mawaziri wenzake .

Tuachane na hayo; Nimemtafuta Wasira sikumpata, maana nilitaka nimjulishe kuwa kuna mmoja ameshauri afanye juhudi kubwa n haraka ili kukamilisha ‘juhudi zake' za kuondoa shida ya maji katika maeneo ya Nyamakokoto,Bunda stoo,Nyasura,Migungani na sehemu nyingine.

Bado naendelea "kumtafuta" Stephen Masato Wasira ili nijiridhishe iwapo kweli hana hata kashfa moja kama wanavyosema watu wengi. BADO NAENDELEA KUMTAFUTA.

Makala kwa Hisani ya Gazeti la Pata Habari.

Asiye na KASHFA ?? wewe Umezaliwa 1999? kwasababu haujui ya kuwa alikikimbia CCM kwa MATUSI kwa kukosa nafasi kugombea huo UBUNGE na kuhamia NCCR MAGEUZI na kushinda kama Mpinzani wa CCM;

Ina Maana KATIBA ya CCM inataka Wabunge wawe na 3 TERM LIMITS baada ya hapo wanaachia NGAZI kupisha DAMU SAFI MPYA na kuondoa ULIMBUKENI na KUONDOA UMAFIA wa KURUDISHA WANASIASA walewale ndani ya HICHO CHOMBO nakukifanya kama ni FAMILY ORIENTED CULT COMMITEE.. Kwahiyo angehama na kukimbilia chama kingine???

Sababu Soma hotuba zake za CHUKi DHIDI ya CCM... Inaonyesha kweli Wanaosoma JAMII FORUMS wasema Ukweli WOOOTE Wamekimbia au wamekwenda in the DL...

ANOTHER PAIN in Our True Democracy
 
Tony, tofautisha maana ya Nchi na Chama cha siasa na shughuli zake zinavyoendeshwa.
Ukiwa na mtazao huo finyu walioko upinzani leo asilimia kubwa walianza wapi? nadhani hapo ukijitafakari utaona jinsi usivyotumia neno uhaini na maana yake halisi.

Hapa Maslahi ya nchi na Wananchi yanatazamwa kwa utumishi wa Mwanasiasa.

Wasira deserves credit for being faithful and royal to his country, since the first Mwalimu Nyerere Regime to the forth Regime of Jakaya Kikwete.

Ataturudisha enzi za Mwalimu na kuifanya nchi ya politic badala ya watu kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Ni mzuri kwenye siasa lakini sio mbunifu. Kanda ya ziwa ns bunda kwa ujumla ina wachapakazi lakini hatujaona jinsi ambavyo Wassira alivyotumia ushawishi wake kuleta maendeleo badala yake anatumia muda mwingi kujenga chama anachokipenda kwa sababu ya madaraka ,akikosa anahama na kwenda upinzani.Yule ni CCM madaraka.
Hanatofauti na enzi za Mzee Malecela,naye alitumia Muda mwingi kupigania Chama badala ya kupigania maendeleo ya wananchi wa mtera na Dodoma kwa ujumla.
 
Huyu mzee anafaa kuwa Rais wa Tanzania. Naamini ndiye pekee kama kweli tunataka CCM iendelee kushika madaraka. Zaidi ya hapo hakuna mtu pale Lumumba.
 
Ishu ya kuchinja kule Geita tukumbushane kidogo alikuwa msuluhishi huyu....
 
Huyu mzee anafaa kuwa Rais wa Tanzania. Naamini ndiye pekee kama kweli tunataka CCM iendelee kushika madaraka. Zaidi ya hapo hakuna mtu pale Lumumba.
kama kigezo cha urais ni kutokuwa na kashfa basi anafaa, lakini kiutendaji bado hajanishawishi kuwa anaweza kuipeleka nchi kule tunakotaka.
 
Mkuu hujalala wewe?
 
Exactly, sasa sijui wanatafuta nini zaid. He is an epitome of QUESTIONABLE LOYALTY, kwa lugha ya CDM ni msaliti.

Mhh mbona una mashairi kama ya mjomba? Amekupa copyright?
 
  • Thanks
Reactions: bdo
kuwahi kutoka ccm na kujiunga upinzani ni kashfa kubwa kuriko zote ni zaidi ya kuuza utu,kusaliti nchi ni uhain

Baada ya CCM kuamua kuwa mgombea ubunge jimbo la Bunda awe Waziri Mkuu Joseph Warioba, Wasira akazila. Akajitoa CCM akajiunga na NCCR ya Mrema.

Hivyo Wasira aligombea ubunge mwaka 1995 kwa tiketi ya NCCR na akashinda na kuwa mbunge wa UPINZANI.

Bwana Warioba alipinga ushindi huo mahakamani na Wasira akaondolewa kwenye ubunge na AKAFUNGIWA KUGOMBEA KWA MIAKA 10. Kipindi hiki kilikuwa kigumu sana kwa Wasira maana muda alikuwa anakula hapa IFMSo canteen akiwa amevaa KANDAMBILI! Ni ngumu kuamini!

Tuanzie hapo sasa. Uchagizi wa 2005 akagombea kwa tiketi ya CCM tena! Sasa utuambie, mtu wa aina hii anaaminika? Je itikadi yake iko wapi? Huyu ndiyo Wasira Tyson Mr. White.
 
Eti hana kashfa! Ebu nenda Musoma ukawaulize pesa za ujenzi wa hospitali ya rufaa zilitafunwa na nani? Alitafuna mamilioni, tena enzi hizo, kutoka kwenye makato ya wakulima wa pamba na hospitali imebaki gofu mpaka leo.
Nyie vijana muwe mnafanya utafiti kwanza kabla ya kukimbilia kuandika.
 
Wasira hana Kashfa?

Muulizeni alimfanya nini mama yake huyu jamaa:

16.jpg
 
Eti hana kashfa! Ebu nenda Musoma ukawaulize pesa za ujenzi wa hospitali ya rufaa zilitafunwa na nani? Alitafuna mamilioni, tena enzi hizo, kutoka kwenye makato ya wakulima wa pamba na hospitali imebaki gofu mpaka leo.
Nyie vijana muwe mnafanya utafiti kwanza kabla ya kukimbilia kuandika.
Hebu tupe mchanganuo wa hiyo kashfa,alikula shilingi ngapi na nani?
Mnakosa cha kuongea na sasa Unabuni tu lolote unaloona linafanana na huko alikotoka,
Najua ni vigumu sana kwa mtu mwanasiasa kuwa Karina siasa kwa kipindi kirefu namna hiyo halafu akakosa doa, lakini kuhusu Wassira na uadilifu hawezi kutenganishwa.

Natamani nimpate mtu aliye na kashfa dhidi yake iliyo wazi na inayoeleweka tumjue kiundani.

Otherwise Hongera Mzalendo Wassira.
 
Asiye na KASHFA ?? wewe Umezaliwa 1999? kwasababu haujui ya kuwa alikikimbia CCM kwa MATUSI kwa kukosa nafasi kugombea huo UBUNGE na kuhamia NCCR MAGEUZI na kushinda kama Mpinzani wa CCM;

Ina Maana KATIBA ya CCM inataka Wabunge wawe na 3 TERM LIMITS baada ya hapo wanaachia NGAZI kupisha DAMU SAFI MPYA na kuondoa ULIMBUKENI na KUONDOA UMAFIA wa KURUDISHA WANASIASA walewale ndani ya HICHO CHOMBO nakukifanya kama ni FAMILY ORIENTED CULT COMMITEE.. Kwahiyo angehama na kukimbilia chama kingine???

Sababu Soma hotuba zake za CHUKi DHIDI ya CCM... Inaonyesha kweli Wanaosoma JAMII FORUMS wasema Ukweli WOOOTE Wamekimbia au wamekwenda in the DL...

ANOTHER PAIN in Our True Democracy
Comment zako huwa zina upande mmoja tu, na Tatizo kubwa ni ushabiki wa kiitikadi ulionao.

Jaribu kutazama makala ya huyo bwana with 'Sober brain' yawezekana kuna jambo jema utaliona.
 
Back
Top Bottom