Stephen Wassira: Kada mkongwe wa CCM asiye na kashfa

Stephen Wassira: Kada mkongwe wa CCM asiye na kashfa

Wasira hana Kashfa?

Muulizeni alimfanya nini mama yake huyu jamaa:

16.jpg

Huyu ni nani?
Ni MC wa harusi gani?
 
Stephen Masato Wasira si jina geni kwa Watanzania, ni jina maarufu. Umaarufu wa Wasira ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu unatokana na mambo mengi.


Haya ndio yamenifanya nianzishe mpango maalum wa kumchunguza kihabari ili niwaoneshe Watanzania upande mwingine wa shilingi kuhusu Mwanasiasa huyo, lakini nakiri kuwa “nimeshindwa kumpata” Wasira katika hilo.

Huyu ndiye Wasira ambaye Mwaka jana aliwatahadharisha Vijana wasomi wa Vyuo Vikuu kutumia taaluma zao kupambanua ukweli na uwongo wa vyama vya siasa ili wasiendelee kuwa wateja wa siasa uchwara na “wachumia matumbo”


Nimeshindwa kumpata WASIRA aliyeyasema hayo katika kongamano lililofanyika mkoani Mwanza na kushirikisha vyuo mbalimbali mkoani humo kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania(SAUT).
Nimeshindwa kumpata kwani kati ya watu niliobahatika kuzungumza nao au niliosoma mandishi yao, hakuna aliyenipa kashfa hata moja inayomgusa Wasira tofauti na upungufu wa kawaida ambao hakuna mtu wa kawaida duniani anayeweza kuukosa.


Baada ya juhudi zangu kushindikana kumpata Wasira ndipo najiuliza “HUYU WASIRA NI MTU WA NAMNA GANI?”
Katika kumtafuta Wasira na dosari zake, nakumbana na Gazeti la Raia Mwema Toleo la 2677 la November ,2013 likiwa na kichwa cha habari kisemacho “Nani ni nani CCM?”


Katika Habari hiyo Gazeti linasema “Stephen Wasira anatajwa kuwa ni mwanasiasa mwenye uwezo wa kuendesha siasa za jukwaani, lakini pia ni mwanasiasa mwenye kupenda siasa za suluhu miongoni mwa wanachama wa CCM, akiwa pia mwiba kwa upande wa vyama vya upinzani kwa wepesi wake wa kujibu mapigo”


Linaongeza”Ingawa CCM haijawahi kuonja historia ya kuwa chama cha Upinzani lakini Wasira amewahi kuingia upinzani na kushinda uchaguzi wa ubunge kupitia NCCR-Mageuzi, akimbwaga aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba”.


Christopher Gamaina, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri , anamtaja Wasira akisema “Sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Wasira ni usafi wa kimaadili ndani na nje ya Chama chake (CCM) kwa maneno na matendo ya maisha yake”.
Gamaina anasema ,“ Pia Wasira anatajwa na watu wengi kwamba ni mtu mwenye msimamo imara katika vita dhidi ya Ufisadi ndiyo maana hana doa wala kashfa ya ufisadi, lakini kubwa zaidi anatajwa kama mmoja wa makada wenye utashi na ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani ya CCM na mwenye upeo mpana wa kuona mbali”.



Mmoja wa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam aliyetoa maoni yake kwa sharti la kutotajwa jina wala cheo, anasema “Ukiachia nafasi walizopata kuwa nazo wenzake, kati ya wanaosemwa (anamaanisha kuutaka Urais mwaka 2015), Wasira ni msafi kuliko wote kwasababu sijawahi kusikia kashfa yake ni mtu mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya siasa na utawala.


Kwa mujibu wa uchunguzi wa uchunguzi wa makala haya, WASIRA amepata kuwa Mbunge wa Mwibara (mwaka 1970-1975), Bunda (1985-1990),(1995-1996) na (2005-2010). Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,Wasira alichaguliwa tena kuliwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Bunda.

Taarifa zilizopatikana katika mtandao zinasema Wasira pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara (mwaka 1975 hadi 1982) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990 hadi 1991.


Habari hizo za kimtandao zinafahamisha kuwa kati ya mwaka 1982 na 1985, Wasira alikuwa Waziri Mwambata katika Ubalozi wa Tanzania Washngton DC, Marekani na kisha akawa Naibu Waziri wa Kilimo mwaka 1972-1975, na Serikali za Mitaa mwaka 1987-1989.


Kwasasa Wasira ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) na Mbunge wa Bunda mkoani Mara.
November Mwaka jana , mmoja wa wachangiaji katika mtandao wa Jamii Forum(JF) aliandika kuhusu Wasira akisema “Huyu mzee namkubali sana ,kwanza hana makundi katika chama na mzee huyu namkubali pia katika hotuba zake zenye nguvu na ushawishi. Namkubali sana..”


Alipoulizwa kuhusu anavyowajua makada watatu wa CCM wanaotajwa kuhusu kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwaka 2015, yaani mawaziri wakuu wazamani, Frederick Sumaye, Edward Lowasa na Wasira, Mratibu wa ULINGO ambayo ni ASASI ya Umoja wa Wanawake katika vyama vya siasa vyenye Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Ave Semakafu, amesema, “Sijaona yeyote kati ya hao anayejali na kuhudumia kwa dhati makundi ya watu walio pembezoni”.


“Wengi wanafanya siasa kavu tu za kuwapa vijana mipira na jezi, wakati wana matatizo magumu yanayowakabili kimaisha. Mipira sio tatizo la Watanzania . Wengine wanasema vijana wamekalia bomu la ajira, lakini hawaoi jawabu la tatizo hilo”.
Anaongeza, “Rais Jakaya Kikwete ndiye amekuwa Mfano bora kwa kuyajali makundi yote ya Watanznia. Amejitahidi hata kuwa karibu na watu na kuweka usawa wa kijinsia.Mfano amejitahidi kuteua majaji wanawake ; ameonesha mfano wa kuinua vijana na wanawake hata katika ule mfuko ulioitwa “Mabilioni ya Kikwete” na kusidia Vijana kupitia mifuko mbalimbali hadi ngazi ya wilaya.”


“Natamani kumpata Mwanasiasa huyu nayetajwa kuwa jasiri asiyeogopa wala kusita kufanya uamuzi mugumu kwa maslahi ya umma” Na nimwambie kimoja wanachosema watu wanaomsema vizuri kwamba zile chagamoto ambazo hajazishughulikia jimboni kwake Bunda, azifanyie kazi.


Nimejitahidi kumtafuta Wasira kwa siku tatu mfululizo nikabahatika “kumpata” kwenye dosari moja waliyonayo Mawaziri karibu wote wa Kikwete kuwa, hawapendi kupokea simu. Hapo nimempata na kumweka kwenye kundi la wabunge na mawaziri wenzake .


Tuachane na hayo; Nimemtafuta Wasira sikumpata, maana nilitaka nimjulishe kuwa kuna mmoja ameshauri afanye juhudi kubwa n haraka ili kukamilisha ‘juhudi zake’ za kuondoa shida ya maji katika maeneo ya Nyamakokoto,Bunda stoo,Nyasura,Migungani na sehemu nyingine.


Bado naendelea “kumtafuta” Stephen Masato Wasira ili nijiridhishe iwapo kweli hana hata kashfa moja kama wanavyosema watu wengi. BADO NAENDELEA KUMTAFUTA.


Makala kwa Hisani ya Gazeti la Pata Habari.
Ni kada mkongwe kivipi maana Wassira alihama CCm na kwenda akihamahama kama vyama vinne hivi, mwishowe aliunda chake, hicho hata hakikuwa na ofisi. Nauliza hivi ukiwa CCM miaka 20, ukahamia chamakingine ukirudi CCM umri wako chamani unakuwa upi au unaunganishiwa? Nijibuni wajameni.

Pili, kuhusu kashfa hilo ni kweli. HANA KASHFA ya ufisadi hata chembe. Tumseme mengine lakini siyo ufisadi.

Tatu, kifamilia kidogo ana kadoa. Mara kesi za hapana pale na wanafamilia na hadi watoto wake wa kuzaa. Hilo linaweza kusemwa ni la binafsi, vinginevyo Wassira hana doa.
 
Wasira hana Kashfa?

Muulizeni alimfanya nini mama yake huyu jamaa:

16.jpg

Baada ya CCM kuamua kuwa mgombea ubunge jimbo la Bunda awe Waziri Mkuu Joseph Warioba, Wasira akazila. Akajitoa CCM akajiunga na NCCR ya Mrema.

Hivyo Wasira aligombea ubunge mwaka 1995 kwa tiketi ya NCCR na akashinda na kuwa mbunge wa UPINZANI.

Bwana Warioba alipinga ushindi huo mahakamani na Wasira akaondolewa kwenye ubunge na AKAFUNGIWA KUGOMBEA KWA MIAKA 10. Kipindi hiki kilikuwa kigumu sana kwa Wasira maana muda alikuwa anakula hapa IFMSo canteen akiwa amevaa KANDAMBILI! Ni ngumu kuamini!

Tuanzie hapo sasa. Uchagizi wa 2005 akagombea kwa tiketi ya CCM tena! Sasa utuambie, mtu wa aina hii anaaminika? Je itikadi yake iko wapi? Huyu ndiyo Wasira Tyson Mr. White.



Angejifunza kwa Mrema ambaye aligoma kurudi CCM pamoja na misukosuko yote aliyopata japo alikua anaipenda CCM.
Vijana waanze kuisoma historia ya huyu Shujaa Mrema aliyepoteza uwaziri kwa kupinga Ufisadi tofauti na hawa wanaojinadi kwmb niwapambanaji wa ufisadi huku waking'ang ania madaraka.
 
Wassira alirudishwa CCM-Mtandao na Rostam. Akapewa na hela nzuri za kwenda kugombea Ubunge na Rostam. Akafanya kazi nzuri sana ya uana-mtandao kati ya 1995-2005 kanda ya Ziwa.

Akapewa Uwaziri katika wizara mbalimbali. Ni fundi sana wa kuzitafuna kwa siri taasisi zilizo chini ya wizara anazoziongoza. Waulizeni TASAF wanavyohangaika naye sasa.

Anaandaliwa kuwa chaguo la pili endapo Lowasa atakwama.
 
Comment zako huwa zina upande mmoja tu, na Tatizo kubwa ni ushabiki wa kiitikadi ulionao.

Jaribu kutazama makala ya huyo bwana with 'Sober brain' yawezekana kuna jambo jema utaliona.

Oh wow --- NACHANGANYIKIWA... Naambiwa kuwa COMMENTs ZANGU hazieleweki -- Kwasababu Haijulikani kama niko UPANDE wa CHAMA TAWALA au UPINZANI naelemea CHADEMA... wewe unanipa KIITIKADI ni SHABIKI

Sasa Ni SHABIKI wa nani ? Kwani kweli hakuondoka CCM ? NYERERE hakumkandia ? Sasa hiyo TUITE NINI kwenye Demokrasia ya NCHI HII... KULINDANA ???
 
Yaania acha tu kaka...

Ni kwa sababu tumekosa UZALENDO.Kibaya kwetu kizuri na kizuri kwetu kibaya.Atakachosema mpinzani hata kama ni kizuri kitatafsiriwa ubaya na kitakachosemwa na CCM hata kama ni kibaya kitapewa uzuri.Inasikitisha sana.
 
Wassira alirudishwa CCM-Mtandao na Rostam. Akapewa na hela nzuri za kwenda kugombea Ubunge na Rostam. Akafanya kazi nzuri sana ya uana-mtandao kati ya 1995-2005 kanda ya Ziwa.

Akapewa Uwaziri katika wizara mbalimbali. Ni fundi sana wa kuzitafuna kwa siri taasisi zilizo chini ya wizara anazoziongoza. Waulizeni TASAF wanavyohangaika naye sasa.

Anaandaliwa kuwa chaguo la pili endapo Lowasa atakwama.

Haya mambo ya mtandao ndio yanaipeleka nchi yetu pabaya. Hawa wana mtandao wanatuamulia rais kutokana na ujinga wetu.
 

Mleta mada nimesoma makala yako mwanzo hadi mwisho kwa utulivu, hakika ujumbe wako ni mzuri nilitamani uendelee kutoa story ya Ndugu Wasira.

Katika siasa kuna bahati na vipaji katika watu, kuna baadhi ya watu wanalazimisha siasa labda kwa sababu ya fedha zao au kwakuwa wao walikuwa watoto wa fulani au ukoo fulani.

Lakini tangu naanza kufuatilia siasa hizi za Tanzania nimegundua kuna watu wana mvuto sana na wamebarikiwa na Mungu kuwa na vipaji vya kuendesha siasa, Mmoja wao katika kundi hili ni Stephen Wasira.

Siwezi kusema sana lakini hotuba zake majukwaani na harakati zimekuwa zenye mafanikio sana, ukimsikiliza huwezi kuchoka, utacheka,utafurahi na utaelewa ujumbe anaokusudia kuufikisha.

Wasira anaweza kutoa hotuba according to level of listeners, kulingana na aina ya watu anaowahutubia na ujumbe unafika.
 
Acha kutudanganya! Umesahau kashfa ya kuuchapa usingizi bungeni?
 
UPOFU MWINGINE BHANA NI MBAYA SANA... yani wassira naye ni safi? Hv Tunasahau Au Tuajisahaulisha? Si Ni Huyuhuyu Aliyefungiwa Kugombea Ubunge Na Mahakama Kwa Miaka Mitano Kutokea 1997 Mpaka 2002 Kwa Kutoa Rushwa Kwenye Uchaguzi Aliomshinda Warioba??nzishe mpango maalum wa kumchunguza kihabari ili niwaoneshe Watanzania upande mwingine wa shilingi kuhusu Mwanasiasa huyo, lakini nakiri kuwa £¿nimeshindwa kumpata£¿ Wasira katika hilo.

Huyu ndiye Wasira ambaye Mwaka jana aliwatahadharisha Vijana wasomi wa Vyuo Vikuu kutumia taaluma zao kupambanua ukweli na uwongo wa vyama vya siasa ili wasiendelee kuwa wateja wa siasa uchwara na £¿wachumia matumbo£¿


Nimeshindwa kumpata WASIRA aliyeyasema hayo katika kongamano lililofanyika mkoani Mwanza na kushirikisha vyuo mbalimbali mkoani humo kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania(SAUT).
Nimeshindwa kumpata kwani kati ya watu niliobahatika kuzungumza nao au niliosoma mandishi yao, hakuna aliyenipa kashfa hata moja inayomgusa Wasira tofauti
 
Kweli Watanzania mna AKILI ZA SAMAKI na WAVIVU WA KUUTAFUTA UKWELI?! Leo mwanaume mzima na ma****nde yake anakuja JF na kuuambia umma wa wa-Tanzania kwamba Wassira ni msafi hana doa lolote! Please give us a break. Wassira huyu alishawahi kupatikana na hatia ya kutoa RUSHWA mbele ya mahakama na kufungiwa kutogombea nfasi ya uongozi wowote katika Taifa hili kwa kipindi cha miaka 5. Watanzania wachache wanaopenda kuutafuta ukweli wanaweza kupata reference ya kesi hii (Warioba V Wassira) mahakama kuu. Wassira huyu huyu alishawahi kupatikana hatia before the court of law for a violence conduct baada ya kumpiga magumi hadharani mtu. hence JK kumbatiza jina la TYSON.
 
Usimtafute sana ngoja nikusaidie mahali pa kuanzia. Mulize akueleze na kisha utuambie kuhusu ile kashfa aliyopata pale aliposhitakiwa na Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba na kumshinda katika kesi ya uchaguzi kwa kosa la kutoa rushwa kwenye uchaguzi na hivyo kufungiwa na Mahakama Kuu kushiriki masuala ya siasa kwa muda wa miaka mitano. Je, unalijua hili au hulijui. Kama unalijua basi tueleze! Vinginevyo yeye analijua na kama ni mkweli atakueleza na wewe utatueleza.
 
Wassira alirudishwa CCM-Mtandao na Rostam. Akapewa na hela nzuri za kwenda kugombea Ubunge na Rostam. Akafanya kazi nzuri sana ya uana-mtandao kati ya 1995-2005 kanda ya Ziwa.

Akapewa Uwaziri katika wizara mbalimbali. Ni fundi sana wa kuzitafuna kwa siri taasisi zilizo chini ya wizara anazoziongoza. Waulizeni TASAF wanavyohangaika naye sasa.

Anaandaliwa kuwa chaguo la pili endapo Lowasa atakwama.

Ooh! Mungu atuepushe na BALAAA HILI.
 
Ana umri gani huyu mzee maana amekuwa mtawala tangu sijazaliwa hadi sasa nina zaidi ya miaka 40. Ndo maana taifa hili haliendelei akili zile zile miaka nenda rudi
 
Ana umri gani huyu mzee maana amekuwa mtawala tangu sijazaliwa hadi sasa nina zaidi ya miaka 40. Ndo maana taifa hili haliendelei akili zile zile miaka nenda rudi

Ana miaka 68, mwenye nguvu, Afya njema, heima na Busara.


9k=
 
Back
Top Bottom