The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Stephen Wasira ameeleza kuwa Chama cha Mapinduzi kimefanya maendeleo makubwa katika sekta nyingi nchini ikiwemo sekta ya elimu licha ya kuwa watu wengine wamekuwa
wakiyabeza.
“Jana niliwaambia wako wanaosema hatujafanya lolote nikawaambia nyie mnaota ndoto za mchana wakati tunajitawala hatukuwa na Chuo Kikuu, sasa leo tuna vyuo vikuu vya serikali 12 vyote vinatoa shahada” amesema Wasira
Wasira amesema hayo leo 18, April 2025 wakati akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Tabora akiwa katika eneo la kihistoria ya Sanamu la Mwalimu Nyerere lililopo Manispaa ya Tabora , mkoani Tabora , ikiwa ni tamati ya ziara yake ya ukaguzi wa uhai wa CCM na Jumuiya zake mkoani Tabora .
Wasira ameongeza kuwa kuna haja ya vijana nchini kufundishwa kuhusu historia ya amani ya taifa, ili wawe wazalendo na nchi yao licha ya kuwa baadhi ya watu hawataelewa kuhusu kuwa wazalendo.
"Nchi yetu lazima ianze kufundishwa vijana wajue historia yao, kwa sababu uzalendo unatokana na kujua, tuwafundishe wengi wajue wataelewa tutabaki na watu wachache" Wasira alisema.