Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,641
- 4,457
“Nilifikia kilele cha mafanikio katika biashara duniani. Katika macho ya watu wengine, maisha yangu ni kielelezo cha mafanikio. Hata hivyo, mbali na kufanya kazi, nina furaha ndogo. Kwa jumla, utajiri ni uhalisia tu wa maisha ambayo nimeyazoea.
Wakati huu ambao nimelala kitandani nikiwa mgonjwa na kuyakumbuka maisha yangu yote, ninagundua kwamba ufahamu utajiri nilionao umefifia kwa kuwa hauna maana wakati kifo kinakaribia.
Nikiwa gizani, ninautazama mwanga wa kijani kutoka katika mashine zinazonisaidia kuendelea kuishi na kusikia sauti za muungurumo wake, ninasikia na kuhisia pumzi za Mungu na za kifo zikinikaribia…
Sasa nafahamu kwamba tunapolimbikiza utajiri wa kutosha maishani mwetu, inatupasa kufuatilia mambo mengine ambayo hayahusiani na utajiri…
Kiwe ni kitu fulani ambacho ni muhimu zaidi:
Labda ni uhusiano, labda ni sanaa, labda ni ndoto inayoanzia katika siku za ujana…
Kutafuta utajiri muda wote utamwingiza mtu katika maisha yasiyofahamika, kama mimi.
Mungu alitupa hisia za kutambua pendo katika kila moyo wa mtu, si mauzauza yanayoletwa na utajiri.
Utajiri nilioupata maishani mwangu siwezi kuondoka nao.
Ninachoweza kuondoka nacho ni kumbukumbu zilizojaa upendo.
Huo ndiyo utajiri wa kweli utakaokufuata, utakaoungana nawe, ukakupata nguvu na mwanga wa kusonga mbele.
Upendo unaweza kusafiri maelfu ya maili. Maisha hayana kikomo. Nenda unapotaka. Fika katika kilele unachotaka kufika. Yote yamo moyoni na mikononi mwako.
Ni kitanda gani chenye gharama zaidi duniani? Ni kitanda wanacholalia wagonjwa…
Unaweza kumwajiri mtu akaendesha gari lako, mtu akakuingizia fedha lakini huwezi kumpata mtu wa kubeba ugonjwa wako.
Vitu vilivyopotea vinaweza kupatikana. Lakini kuna kitu kimoja ambacho hakipatikani pindi kikipotea – ni Maisha.
Mtu anapokwenda katika chumba cha upasuaji, atagundua kwamba kuna kitabu kimoja ambacho bado hajamaliza kukisoma – “Kitabu cha Maisha ya Afya”.
Hata tukiwa katika daraja gani la maisha hivi sasa, muda ukifika, tutakabiliana na siku ambapo pazia la maisha litashuka
Thamini Upendo kwa familia yako, mpende mwenza (mke/mme) wako, wapende marafiki zako. Jitambue vyema. Wathamini watu wengine.”
Steve Jobs alikuwa akiugua ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu
Baada ya kuandika barua hiyo! Siku chache mbele akafariki!
Sent using Jamii Forums mobile app