Pre GE2025 Steve Nyerere adokeza kuwa Rais Samia amekuwa akimuulizia mchekeshaji Asha Boko. Asha Boko alia machozi baada ya kupokea zawadi

Pre GE2025 Steve Nyerere adokeza kuwa Rais Samia amekuwa akimuulizia mchekeshaji Asha Boko. Asha Boko alia machozi baada ya kupokea zawadi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Akiwa anatoa "zawadi" ya bodaboda hivi karibuni kwa mchekeshaji Asha Boko, Steve Nyerere amesema kuwa kuna kipindi alikuwa na Rais Samia na kwamba Rais Samia alimuuliza yeye kuhusu wapi alipo Asha Boko.

Binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa hizi zawadi zinatoka kwenye mfuko wa hiyo "organization" ya Steve Nyere

There is a lot at play here!

=======================================================

Mwigizaji na mchekeshaji maarufu Bongo, Asha Boko hapo jana, Januari 11, 2025 aliwavunja watu mbavu baada ya kuangua kilio wakati akikabidhiwa pikipiki mpya aliyopewa kama zawadi.

Asha Boko alikabidhiwa pikipiki hiyo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere aliyemzawadia kama shukrani kwa mchango wake na namna anavyojitoa kwa nafasi yake katika taasisi hiyo kwenye matukio mbalimbali.

Asha Boko alikabidhiwa pikipiki hiyo makao makuu ya ofisi ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya wanataasisi hiyo iliyohudhuriwa na mkongwe wa muziki kutokea DR Congo, Bozi Boziana na wadau wengine kutoka katika tasnia mbalimbali.

 
Back
Top Bottom