Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa ‘Mama Ongea na Mwanao,’ Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere, amempongeza Tundu Lissu kwa kutangaza nia yake ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA, akisisitiza kuwa ni haki yake kikatiba mradi anazingatia miko na katiba ya chama.
Kupitia ujumbe aliouandika, Steve alisema:
"Nimekusikiliza mara 100, nasema nimekuelewa. Ni haki yako kikatiba kugombea ilimradi huvunji katiba ya chama chako na miko ya chama chako. Ukijiona unatosha, basi muda wa kujipima kwa wanachama wenzako ni sasa kwa maslahi mapana ya umoja wenu."
Aliendelea kusema:
"Natamani hivi karibuni nimuone mgombea mwenza wako naye akijitokeza hadharani… Hongera Mwenyekiti."
Kwa utani, Steve akisema:
"Doo, tatizo mzigo ulikuwa unapita chumbani, sebuleni wakubwa mnakula upepo, wine, Hennessey kidogo… Lazima ubwage."
Pia, Soma:
• Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA
• Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA