Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania, Steven Nyerere, ameonyesha kutoridhishwa na hatua ya mfanyabiashara Niffer kumjibu Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kupitia mitandao ya kijamii. Hii ilitokea baada ya Niffer kuitwa kituo cha polisi kwa mahojiano kufuatia kampeni yake ya kuchangisha pesa mtandaoni kwa waathirika wa ajali ya jengo lililoporomoka Kariakoo.
Pia, Soma:
Steven amesema hatua ya Niffer ni ishara ya ukosefu wa heshima, akidai kuwa kitendo hicho hakipaswi kufumbiwa macho. Aidha, alitoa lawama kwa marafiki wa karibu wa Niffer, akisema wameshindwa kumshauri vema na kumwongoza kuepuka mgongano na viongozi wa serikali.
"Naona kama Niffer anazungukwa na marafiki wasiomtakia mema, kwani ni jambo lisilo la hekima kumjibu Waziri Mkuu hadharani,"
Pia, Soma:
- Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
- Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo
- Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa