Muigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania, Steven Nyerere, ameonyesha kutoridhishwa na hatua ya mfanyabiashara Niffer kumjibu Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kupitia mitandao ya kijamii. Hii ilitokea baada ya Niffer kuitwa kituo cha polisi kwa mahojiano kufuatia kampeni yake ya kuchangisha pesa mtandaoni kwa waathirika wa ajali ya jengo lililoporomoka Kariakoo.
Pia, Soma:
Steven amesema hatua ya Niffer ni ishara ya ukosefu wa heshima, akidai kuwa kitendo hicho hakipaswi kufumbiwa macho. Aidha, alitoa lawama kwa marafiki wa karibu wa Niffer, akisema wameshindwa kumshauri vema na kumwongoza kuepuka mgongano na viongozi wa serikali.
"Naona kama Niffer anazungukwa na marafiki wasiomtakia mema, kwani ni jambo lisilo la hekima kumjibu Waziri Mkuu hadharani,"