Steve Nyerere amvaa tena Lulu

Steve Nyerere amvaa tena Lulu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta Lulu ya kutojumuika nawenzake kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera klabu ya Bongo Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya.

Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria shughuli za wenzie kama misiba au hata sherehe zilianza tangu alipotoka gerezani. Ilisemekana kwamba kilichosababisha viongozi wa Bongo Muvi kukasirishwa na kuamua kumweka kikao ili kumsema, ni kwamba ipo sikunaye yatamfika.

Baada ya kuzinyaka, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie Steven Mengere, Steve Nyerere ambaye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo ili kumuonya kwa tabia yake hiyo kwa kuwa yeye bado mdogo.

Alisema Lulu anatakiwa afuate nyayo za wakubwa zake ambao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali kwa kuwa ipo sikunaye yatamfika.
Lulu ni mtoto mdogo, hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda.

Sisi kama Bongo Movie tuna kawaida yakuhudhuria shughuli za wenzetu pale inapobidi lakini kama mtu anakuwa na udhuru huwa anatoa taarifa lakini yeye hana kawaida hiyo,anajiona amekamilika.

Naaamini ipo siku na yeye yatamfika kwa kuwa mitihani ni kawaida kwa binadamu, sidhani kama mtu atajitokeza na kumuunga mkono kwa tabia hiyo na siyo yeye tu anayejitenga, wapo nawengine wengi lakini yeye bado ni mdogo kwetu huenda hajui alitendalo ndiyo maana tunataka tumfunze jinsi ya kuishi na watu," alisema Steve.

Kwa upande wake Lulu alipotafutwa na kuulizwa juu ya jambo hilo hakuonesha mshtuko bali aliwaka: "Huyo aliyesema hivyo atajijua mwenyewe mimi sina shughuli na mtu, aachanena mimi.
 
Huyu naye yatamshinda, mfyuuuuuuu.
Janaume zima kutwa kusimanga watoto wa wenzie.
 
Hiv huyu ndio baba ushauri si ashauri watoto wake pambaff steve
 
Mtu halazimishwi kwenda shughulini bana, yakimfika atajibeba mwenyewe....
 
Mtu halazimishwi kwenda shughulini bana, yakimfika atajibeba mwenyewe....

Apo sasa , maneno mengi ya nn ?? Kwan walivyomfanyia wema kwenye msiba wa baba ake walimuonya?? Si wali surprise madame had akapararaiz
 
Apo sasa , maneno mengi ya nn ?? Kwan walivyomfanyia wema kwenye msiba wa baba ake walimuonya?? Si wali surprise madame had akapararaiz

Dawa ndo hiyo, ni vitendo tu...
kama ye huwa anatuma hela zamu yake pia atumiwe tu hela kazi kwisha
 
Lulu ana ndugu zake sio lazima hao bongo muvie.

Watu wenyewe hata 20 hawafiki iweje wamshupalie mtu ajumuike nao?

Ningekuwa mimi nisingejiunga nao
 
Lulu ana ndugu zake sio lazima hao bongo muvie.

Watu wenyewe hata 20 hawafiki iweje wamshupalie mtu ajumuike nao?

Ningekuwa mimi nisingejiunga nao

Si umeona lulu alivyojibu , Kasema wamuache n maisha yake, naona kajifunza alivyoingia jela , maana hakuna aliyemsaidia kama Dr Chen n familia yake so hata wasipoudhuria kwenye matatizo yak anaona poa tu maana hat alipokuwa jela hawakujishughulisha
 
Hivi kwani kule Segerea hiyo unity walikuwa wanaendaga kule zaidi ya Dr. Cheni na Mama Lulu??
 
Kwanza alishajibeba kule Segerea alikuwa anaendaga Dr. Cheni na mama lulu tu... Wamuache ye alishaona familia yake inamtosha
Ila nilisikia mwenyewe alikataa watu, kwa madai kuwa wanaenda kumsanifu...
 
Nipe story binam walienda kumpeleleza kuhusu ilikuaje The great akadedi etii

Binamu nae umbea wote huo ukusikia kuhus kifo cha kanumba??

Yah familia ilikataa mtu yeyote kumsalimia wala kumpelekea chakula zaidi ya mama mzazi , cheni na muigizaji mmoja anaitwa muna basi , maana wasanii walikuwa wanamkashfu sana lulu , familia ikasikia na haikutak msanii au mt yeyote wa pemben ajihusishe na lulu kwenye lile tukio
 
Back
Top Bottom