Steve Nyerere astaafu kuwa kiongozi misibani

Steve Nyerere astaafu kuwa kiongozi misibani

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
MSANII maarufu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema amekoma kuwa kiongozi misibani kwa sababu ya matusi anayovuna akishika nafasi hiyo. Steve aliiambia Za Motomoto News wikiendi iliyopita kuwa, amekuwa akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake. “Unajua mimi nina watoto, sasa wanapoona yanayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo watanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nitashiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve
 
Atulie kama una akili iliyokomaa huwez kusumbuliwa na Watu wa mitandaoni tena mtandao wenyewe Instagram
 
Kwenye msiba wa mtoto Pati hakupiga picha akiwa makaburini?
 
umaarufu ni harufu ""..yeye atulie " dawa imuingie "".. kama angekuwa hali hizo Pesa za michango "" basi angekuwa anapata sifa njema toka kwa watu "na kuuheshimu mchango wako ""..kwakujitolea "kwake"" asisahu kuwa wahenga hawakuwa wajinga "" pale waliposema kwamba ...Lisemwalo lipo ...............na panapofuka moshi ................
 
Kwani lazima yeye kuwa kiongozi?

Hata hivyo amechelewa sana Maana nilikua nashangaa hizi tuhuma zote inakuwaje Jamaa bado anang'ang'ana na misiba ya Watu!
 
Kwani na msiba huu pia amepiga vihela kidogo..?
 
Sasa yeye ambaye ameshaota ngozi ngumu akikimbia nani tena ataweza hilo jukumu
 
Back
Top Bottom