Steve Nyerere kaidhalilisha CCM

Steve Nyerere kaidhalilisha CCM

MtuHabari

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
321
Reaction score
1,019
STEVE NYERERE KAKIDHALILISHA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), BUNGE na TUME YA UCHAGUZI WAOMBE RADHI

Anaandika Reuben Mchome

0655331933.

Kwani kuna wabunge waliopo Bungeni kwa VIMEMO?

Kwani kuna wabunge waliopo Bungeni na ushindi wao ukiwa ni wa MASHAKA?

Mshindi wa SITA kuongoza Jimbo (MBUNGE) ni kosa au ni dhambi?

Na kama mshindi wa SITA kuongoza Jimbo ni kosa au ni dhambi, hilo kosa au hiyo dhambi ni ya mbunge au Chama (CCM) kilichompitisha?

Baadhi ya Vitabu Vitakatifu vinasema kila jambo duniani lina majira yake na nyakati zake, kuna wakati wa kunena na kuna wakati wa kunyamaza, kuna wakati wa kupandana na kuna wakati wa kuvuna, kuna wakati wa kucheka na kuna wakati wa kulia, kuna wakati wa kuzaliwa na kuna wakati wa kufa, kuna wakati wa kuomboleza na kuna wakati wa kucheza, kuna wakati wa kutupa mawe na kuna wakati wa kuyakusanya mawe.

Ukiangalia maana halisi ya mistari hii kwenye Vitabu Vitakatifu ni moja tuu, kutukumbusha ama kutufundisha sisi wanadamu kufanya mambo yetu kwa usahihi wa majira husika, ukifanya jambo kwenye majira yasiyo sahihi basi kilio chake kitakuwa kikubwa.

Wataalamu wa kupanda majukwaani ni kufungua vinywa vyao na kuwasha vipaza sauti na kupiga maneno mbele za watu wanasema kila neno linalotoka kinywani mwa mwanadamu lina HASI au CHANYA yake. (Epuka sana HASI)

Kwa takribani wiki moja sasa, mitandao ya kijamii imetawaliwa na kelele, mizaha, kejeli, vibweka, majigambo, kukosoana na kuvurugana juu ya msemaji wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania.

Baada ya kufuatilia swaga za hapa na pale tangu sakata hili lilipoanza pale Bodi ya Shirikisho hilo lilipomtangaza Steve Nyerere (Steve Akeeee) kuwa Msemaji wa Shirikisho hilo, tumeshuhudia mengi kutoka kwa wanamuziki wa Tanzania ikiwa ni pamoja na wengine kuunga mkono uteuzi wake huku wengine wakipinga vikali uteuzi huo.

Steve Nyerere amekuwa ni mtu wa kuzungumza sana hata pale ambapo hapaswi kuzungumza (haangalii majira wala nyakati) leo nimemsikia akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari akiwajibu wanamuziki ambao wameonyesha kutomkubali au kutokuunga mkono uteuzi wake wa kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

Leo Steve Nyerere umeongea bila kuangalia MAJIRA na NYAKATI, leo ulipaswa kuzungumza KIMUZIKI zaidi na sio KISIASA kama ulivyofanya, na mbaya zaidi umemshambulia mtu lakini kupitia kwenye chama, chama ambacho wewe ni mwanachama wake na ndicho chama tawala na chama chenye wabunge wengi Bungeni.

Mimi sitazungumzia zaidi Muziki, mimi nitazungumzia kauli zako kwenye maslahi mapana ya Taifa.

Mwaka 2020 Steve Nyerere uligombea Ubunge kupitia Chama Tawala CCM lakini kura zako hazikutosha kwenye ngazi za kura za maoni, Steve Nyerere wewe unajua taratibu na kanuni za chama chako kuhusu mwanachama mwenye dukuduku juu ya maamuzi yoyote yaliyofanywa na chama juu ya mwanachama yoyote, Steve Nyerere unajua majukwaa halali ya kuzungumzia mambo ya chama chako.

Steve Nyerere, leo hii kuhoji kama mbunge halali wa CCM alishinda au hakushinda wakati Chama kinatambua kwamba ameshinda, Tume ya Uchaguzi imemtangaza na kumtambua kama mshindi wa Uchaguzi, Bunge likampokea na kumuapisha kama Mbunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku ni kukikosea chama chako na viongozi wake lakini pia kulikosea Bunge pamoja na Tume ya Uchaguzi, WAOMBE RADHI.

Steve Nyerere, leo hii kusema hamtaki wabunge wa vimemo, unataka kuiambia nini dunia? Unataka kusema kuna wabunge wapo Bungeni kwa vimemo? Na kama ni kweli, hivyo vimemo vilitoka wapi kwenda kwa nani? Wanaotangaza mshindi wa kiti cha Ubunge ni Tume ya Uchaguzi, Je unataka kusema Tume ya Uchaguzi ilipokea vimemo kutangaza washindi wa viti vya ubunge? Hapa umeikosea sana Tume ya Uchaguzi, WAOMBE RADHI.

Steve Nyerere, leo unahoji mshindi wa SITA wa CCM kuongoza jimbo? Ni wanachama wangapi wa CCM walioongoza kwenye kura za maoni na hawakupitishwa na chama? Kwahiyo unataka kutuambia kwamba viongozi wa CCM walifanya makosa katika hili? Hapa umekikosea sana CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) na Mwenyekiti wake pamoja na uongozi mzima wa chama. WAOMBE RADHI.

Wahenga walisema mdomo uliponza kichwa.

Mimi kazi yangu ni Uandishi wa Habari, pamoja na majukumu na kazi zingine zote nilizonazo kwa mujibu wa sheria na katiba kama muandishi wa habari ni pamoja na Kuielimisha jamii na Kuikosoa jamii, nimetimiza majukumu yangu ya kisheria na kikatiba.

MY TAKE: Chama hiki kimekubuhu katika kulea mbumbumbu na kuwapa platform za kuzungumza juu ya wapinzani wao kwa vile hawana aibu mfano pia ni Kibajaj na Msukuma. Lakini hayo ni mabomu kwani hayana uwezo wa kujitambua nilipukie wapi yanaweza kujilipua hata ndani mwao.
 
instagram.jpg
 
STEVE NYERERE KAKIDHALILISHA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), BUNGE na TUME YA UCHAGUZI..WAOMBE RADHI.

Anaandika Reuben Mchome.
0655331933.

Kwani kuna wabunge waliopo Bungeni kwa VIMEMO?
Kama unaharaka Anza kusoma paragraph ya pili kutoka mwisho[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23]
 
MY TAKE;
Chama hiki kimekubuhu katika kulea mbumbumbu na kuwapa platform za kuzungumza juu ya wapinzani wao kwa vile hawana aibu mfano pia ni Kibajaj na Msukuma. Lakini hayo ni mabomu kwani hayana uwezo wa kujitambua nilipukie wapi yanaweza kujilipua hata ndani mwao.
Huyu kijana baada ya kutupwa huko Iringa ambako yeye slianza kujipa ushindi kabla ya kupitishwa na CCM kwa kutumia kigezo cha unyerere!

Alibaki na kinyogo ila sasa amepata uwanja wa kuitema nyongo.
 
Kuwadi wa ngono hajawahi kufanikiwa na hatafanikiwa kamwe kuwa ni kuwadi wa Kisiasa. Tanzania tunao Wabunge wa CCM wa vimemo kwa mujibu wa Stefu na anaye mtumia.
 
Back
Top Bottom