Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Kumradhi kidogo.. usije kuchanganya Steve Walsh yule mchezaji na Steve Walsh huyu Scout tunaemzungumzia hapa Leo, Walsh ni mtu asiyeimbwa sana nyuma ya mafanikio ya Chelsea na Leicester City yeye akiwa kama Msaka vipaji wao.
Wakati Billionea wa Chelsea Roman Abramovich akianza kuisuka Chelsea upya alihitaji jicho la kuona mbali kama la Walsh, ni huyu Bwana aliwaletea pale Gianfranco Zola ambaye ni Legend pale darajani, ni huyu Bwana aliesafiri mpaka Ufaransa na kurejea na jina la Didier Drogba kwa Jose Mourinho.
Nani asiejua kuhusu majina hayo mawili makubwa pale Stamford Bridge, huyu ndie binadamu aliefanya ile kazi, baadae alisepa zake mpaka Newcastle United, Kule ndipo alikutana na Kocha Nigel Pearson, na ndio maana Magpies wanadai Leicester is made in Newcastle, Walsh alikuwa scout mkuu pale St James Park.
Wakati Pearson anaelekea Leicester City 2008 aliondoka na Walsh, kwenda kwao King Power ilikuwa ni mwanzo wa historia kubwa kwa The Foxes, Walsh alikuwa mtu muhimu nyuma ya mafanikio ya kutwaa ubingwa wa England.
Walsh alihusika na usajili wa Jammie Vardy kutoka Fleetwood Town mpaka Leicester City, Walsh alipaa mpaka Ufaransa kuchukua jina la Rihyad Mahrez kwenye klabu ya AC Le Havre ule msimu wa 2013/14 ni huyu bwana alietuletea Ngolo Kante kutoka SM Caen, ilikuwa jicho kubwa mno, ni miwani ya bundi hii, Walsh with binocular eyes.
Nani asiyejua kwa pamoja Kante, Mahrez na Vardy ni nini walichofanya pale King Power msimu ule wa 2015/16, nyuma ya mafanikio ya Claudio Ranieri ni Steve Walsh, msaka vipaji bora kuwahi kutokea kwa upande wangu.
Walsh baadae alitimkia Everton baada ya kuhitajika na Boss Farhad Moshiri, lakini 2018 aliacha kazi kutokana na matokeo mabovu na kufeli kwa Everton kwenye dirisha la usajili, ila ana legacy kubwa sana.
Ila nyuma ya stori ya Ngolo Kante kulikuwa na mtu anaitwa David Abbot, shabiki la kutupwa la Middlesbrough, jamaa aliwahi kutweet 2011, miaka miwili kabla Walsh hajamleta Kante pale Leicester, Abbot aliwaomba klabu yake wamsajili Kante, ila walimpa kalenda tu.