Steven Kanumba's Death and Elizabeth Michael a.k.a Lulu's Involvement; The Guide at JF

Steven Kanumba's Death and Elizabeth Michael a.k.a Lulu's Involvement; The Guide at JF

... Lengo la hii thread ni kutengeneza kumbu kumbu ya Thread zote ambazo zimeguza hilo tukio La kusikitisha. Kwa wale ambao ni members hawapo, kwa wale ambao watakuja kua members, kwa wale ambao watataka kujikumbushia ama kusoama yote kuhusiana na shughuli nzima waweze pata kwa urahisi badala ya kutafuta randomly. Threads zipo nyingi sana hivo nimejaribu chukua baadhi ya Msingi. Kuna nyingine sijaziona Nitaomba fellow members wajaribu kuweka Links katika posts na nita update ..
AshaDii, realy wasn't in JF at that time! That means the thread realy have served its purpose!!

Honestly I never had all this informations and more important how it really touched you! I am gratefully how you had all concerns especially to Lulu and her future, realy genuine concern ... for a Mom to a daughter .. am again highly pleased, was a very nice article!!

You must know what pushed me all this way ..!The article of General Ulimwengu and "upuuzi" saga .. You should know that I went up and down .. I felt there must be something more/deeper than I could tell ... and here I got it!! all in this thread!!! ... You know how I love to know the real MEANING and deep UNDERSTANDING of issues in nature!! Lots of beauty in the process!! Lot of creativity goes along with it Lol!!

Professionally am taught never to judge but to discern ... in life issues!! But honestly I don't think m that good.

BUT The way you calmly approached and discern your views in that thread ...hii !!! .. What Can I say?!! so perfect!!

NOTE] Key world .. To be able to Discern so nicely, calmly, with penitence and so carefully ... and not to judge .. you must be able to operate above "IQ intelligence" ... Because that must be the function of ... The true Conscience ... which is the function of "Consciousness Intelligence" AND we all know that to be the home/the fountain of Pure Love, Meaning, True understanding and Passion!! The source of humanity and life itself!!!!
 
Last edited by a moderator:
Azimio Jipya huishi kunishangaza, ukatoka kwa mzee Dark City na Ulimwengu wake kutafuta pusher ya depth? lol... On a serious note your post has overwhelmed me... I am more than humbled. Pamoja saana buddy!
 
Last edited by a moderator:
Azimio Jipya huishi kunishangaza, ukatoka kwa mzee Dark City na Ulimwengu wake kutafuta pusher ya depth? lol... On a serious note your post has overwhelmed me... I am more than humbled. Pamoja saana buddy!

Me left speechless...I wish I could have that passion kama ya Azimio Jipya na AshaDii (Da Asha)!!!

Anyway, when it comes to Kanumba (RIP), huwa naamua kukaa kimya kwa sababu msimamo wangu haujawahi kuwa mzuri kwa macho ya walio wengi!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Me left speechless...I wish I could have that passion kama ya Azimio Jipya na AshaDii (Da Asha)!!!

Anyway, when it comes to Kanumba (RIP), huwa naamua kukaa kimya kwa sababu msimamo wangu haujawahi kuwa mzuri kwa macho ya walio wengi!!

Babu DC!!
Dark City kwanza nafurahia kuwa uko very clear na objective na msimamo unaokupa wewe utambulisho wako. Kwa kuwa tunajua watu wengi waliopteza hiyo hulka kwenye maisha yao na hivyo huo kuwa udhaifu mkubwa hasa inapokuwa ni kiongozi wa familia au uongozi sehemu yeyote. Ni heshima mtu kutambua na kuisimamia msimamo wake hata kama sio unaotegemewa na waliomzunguka nafikiri pia kuwa ni msingi mkubwa wa afya ya mtu.

Kuwa patience na ku reserve comments kwenye occasion fulani fulani kwangu mimi naona kuwa ni alama ya strength na understanding ambayo mara nyingi inatamkika kama BUSARA!!

Ndio maana mimi kwenye hoja ya Ulimwengu niliamua kulitumia lile neno kwa mtizamo mwingine kabisa na kwa namna yangu simply sikutaka tu lipite hivi hivi. Lakini of course nikipeleka ujumbe mwingine, naamini wenye manufaa kwa jamii. Na nilitegemea nisieleweke!! Lol!

Kilichonishangaza nikuona AshaDii alivyokuwa ameguswa na hoja nzima ya wasanii na alivyoweza kujieeleza kule kwa ulimwengu calmly and artistically ku prove na ku justify anachoamini ! Maana nafikiri mtu mwingine honestly angeweza akalipuka kweli kweli na kupoteza mwelekeo kabisa!

Nafikiri natakiwa niseme .... Pamoja Sanaaa!Lol!!
 
Last edited by a moderator:
Ukorofi gani tena AshaDii (Da Asha)?

Babu DC!!


hahaha! Ngoja nukuache... Nahitaji mchango wako wa topic nimeweka Great Thinkers... Kachangie mzee wangu alafu kesho nitakuja kukujibu. Saizi nenda zangu kulala. lol Usiku mwema DC...
 
hahaha! Ngoja nukuache... Nahitaji mchango wako wa topic nimeweka Great Thinkers... Kachangie mzee wangu alafu kesho nitakuja kukujibu. Saizi nenda zangu kulala. lol Usiku mwema DC...

Vibaya hivyo Da Asha, utamwachaje mwenzio kwenye neutral gear??


Hiyo inahusu nini hadi unataka tuchangie wakati wewe unafaidi ..usingizi..lol!!

Babu DC!!
 
Habari wana JF...

Kifo cha Star maarufu katika Upande wa movies kwa Jina la Steven Kanumba umetikisha taifa kuliko ilivowahi dhaniwa; Nakubali Kanumba was good na wengine wengi wanadiriki kusema he was The Great. Kwa upande wangu nilikua namkubali kweli, sababu nilimuona alivoanza na alipofika. He was no one but was able to change that.... Na nilikua namkubali more because of the way amechangia ku evolve movie Industry nchini kuliko hata movie zake - nitakua ni Muongo nikisema I have watched more than three of his movies ila nilikua namkubali kama ninavokubali na wasanii wengine hapa nchini kwa michango yao katika entertainment Industry. I have been fortunate to meet him once, and I thot him to be so cool nikifananisha na baadhi ya Ma stars nilo wahi habatika kuwaona (Kwa mfano Hemedi; unaweza chafuka nyongo kwa kumsikiliza na kumtazama swagger zake).

Kifo chake kilikua cha kushtua mno! Wapo ambao kweli kazikwa na tumeanza kusahau, Ila believe me you bado thousands of people wana majonzi hadi dakika hii ya hii thread na post hapa. Kuna watu hawawezi angalia movie wakamaliza; Kilio kinaanza upyaaa... Discussion of his death upya... Hadi leo hii huwezi pita mahala mbali mbali ukakosa sikia randomly akiongelewa. Katika Imani zetu za Kiswahili twaweza justify kwa kusema jamaa alikua na nyota kali sana ya kukubalika na kupendwa. Siamini kama sababu tu inasemekana alikua mcheshi na mkarimu ndio sababu pekee... I don't! Nimebahatika kuongea kwa karibu na moja wa mhudumu ambae alikua zamu siku Marehemu Kanumba alipelekwa hapo hospitali akiwa katika gari yake mwenyewe kapelekwa na huyo mdogo wake na kijana mwingine Pamoja na Mama mwenye nyumba wake. Unaambiwa ilipo tambulika kua Kanumba was indeed dead ni ndani ya mda mfupi watu walikuja kwa wingi toka kona mbali mbali ya jiji kutaka kuja hakikisha kama kweli huku wengi wakiwa hawaamini.

Kama Marehemu kutajwa jina yaweza sababisha yeye kushindwa pumzika kwa AMANI - Basi Kanumba bado ana mda mrefu wa yeye kupumzika kwa AMANI hapa karibuni. Ingekua Marehem kafariki kwa njia hio hio kwa kupitia mkono wa Mwanamke mwingine; Kifo chake, jina lake na mijadala kuhusu tukio hilo la kusikitisha lingeanza kupoa sasa. Bahati mbaya saana kwa jinsi mambo yanavoenda ndio kwanza kama ni hadithi badi tupo stage ya Climax.... Na mwisho wake hautabiriki hata kwa wale ambao husoma hadithi zaidi ya 50 kwa mwaka. It is so complicated! For the simple reason kua Mhusika Mkuu katika hilo tukio ni the Late Kanumba na Elizabeth Michael alternatevly known as Lulu.

Utata wa muelekeo wa hii habari nzima ya kusikitisha wa Uhusika wa Lulu unakuja tokana na sababu nyiingi.... Hii yoote inatokana na mhusika kua mtoto/binti mdogo sana ki umri.... binti ambae yeye Marehemu kamuona na twaweza sema mlea toka utoto hadi kupevuka na kua binti. Lakini zaidi sababu ambazo zina nguvu sana ni yeye Lulu alizo zijenga mwenyewe katika macho ya Jamii. Kwamba yeye ni yeye, akiongea katika vyombo vya habari mara nyingi huwa kwa kejeli na kujidai... ni binti ambae katika macho ya tulio wengi twaona ni kama kashindikana. Na yeye alikua akiona ni sifa (I presume) kuandikwa na vyombo vya habari kila siku.... Ana maneno mengi ambayo yanam paint vibaya kama binti. Ingekua huyo huyo Lulu ni binti ambae katika jamii aonekana ni mpole, mstaarabu, adabu na heshima na kutokua na Kashfa; Kitendo cha Marehemu kufariki kusinge mkandamiza saana katika jamii. Jamii ingeuliza maswali kama Jamani Kanumba alikua akifanya nini na yule binti? Yule si mdogo wake? na maneno yafananayo na hayo.

Yule mtoto ana mtihani mkubwa.... Roho yaniuma. Nime observe asilimia zaidi ya 75 yanamlaumu kua ndio chanzo cha kifo cha Steven Kanumba kana kwamba kamuua... Hao watu wakisahau kua huyo binti hajawahi pewa chance ya kukua katika normal child environment based... toka mtoto kazungukwa na mastar, starehe, pesa, wanaume wenye tamaa na wale ambao wapo tayari kumpa lolote ili kuwez mpata.... Wakisahau kua ni mdogo akili haijakomaa. Kama mkubwa tu akipata anakua limbukeni sembuse yeye?

Sijui ataishi maisha gani? sijui kama ana mfadhili wa kumpleka nje akitoka tu... (amini nakwambia yule binti hawezi pita mtaani popote pale Tanzania); Na vile bado ni mdogo... hata akiachiwa huru anatakiwa uangalizi wa 24/7... Kwa maisha alozoea kuishi ya Kujiachia.... na hali atakua mfungwa hata akiachiwa huru; itakua mtihani mkubwa sana kwake kiasi kwamba aweza hata taka poteza maisha yake mwenyewe.... Hata hivo tuone upepo utavoenda.



Nawapa pole Wazazi, Ndugu/Jamaa, Wasanii wote, Wafanyakazi wake na Watanzania wote waloguswa na Kifo cha Marehem Steven Kanumba. May he Rest In Peace.


Nampa pole sana binti Elizabeth Michael kwa doa la maisha lililomkuta; ni kitu ambacho kingeweza mkuta yeyote yule. But in this it is her. Pole zake saana na I pray for her.... Nawapa pole wazazi wake na watu wake wa karibu wote ambao wameguswa na kuumizwa kwa kuhusika kwake katika tukio.



Lengo la hii thread ni kutengeneza kumbu kumbu ya Thread zote ambazo zimeguza hilo tukio La kusikitisha. Kwa wale ambao ni members hawapo, kwa wale ambao watakuja kua members, kwa wale ambao watataka kujikumbushia ama kusoama yote kuhusiana na shughuli nzima waweze pata kwa urahisi badala ya kutafuta randomly. Threads zipo nyingi sana hivo nimejaribu chukua baadhi ya Msingi. Kuna nyingine sijaziona Nitaomba fellow members wajaribu kuweka Links katika posts na nita update.


Tanzanian actor Steven Kanumba reported Dead - Courtesy of Jeryson

Steven Kanumba; Has a very touching story - Courtesy ya Pasco

Madaktari; Hiki ndicho Kilicho muua Kanumba - Courtesy ya Matola

Wabunge Halima Mdee na Easter Bulaya wamefurahi Kanumba Kufa?- Courtesy ya Kamura

TBC1 Wakata matangazo bungeni, wanarusha mazishi ya Kanumba Live - Cortesy ya Wakusoma

Kanumba frustrates JK's Travel Plans - Courtesy of Sijali

Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na mvumbika changa hula mbovu - Cortesy ya Babykailama

Maisha Kitendawili.... Wengi hufa bila kutegua - Courtesy ya The Boss

Kifo Cha Kanumba: Ni uzembe tu! Sio Lulu - Courtesy ya Pasco

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael - Courtesy ya Maseto

Africa Magharibi bado utata, wadhani Kanumba kagongwa na gari - Courtesy ya Misnomer

Speculations behind Kanumba's Death - Courtesy ya Jack Beur

Nyimbo ya Kanumba kabla hajafa ni kama amejitabiria - Cortesy of Hassbaby

Neno la mwisho la Kanumba kwa Mama - Courtesy of Independent Voter

Bungeni Leo; Martha Mlata: Kanumba alitakiwa awe na body guard - Courtesy of Dadio

Filamu ya Kifo cha Kanumba yanaswa kwa siri - Courtesy ya Gumzo

Mod tunaomba utengeneze Jukwaa la Kanumba kuepusha Duplicant - Cortesy of Matope (Lmao hapa)

Kifo cha Kanumba chazua Ushirikina- Courtesy ya Maseto

Kifo cha Kanumba: Wengi kupandishwa Kizimbani - Courtesy ya Allien

Kufa Kufaana; Wasanii Bongo Movies Waanza kuchangisha Pesa- Courtesy ya Ma2mbo

Michango ya Rambi Rambi ya Msiba wa Kanumba watafunwa - Courtesy ya Kimbunga

Kanumba; Holly wood nao walonga - Courtesy ya Alien

Steve Kanumba: Historia; Kazi zake na Mengineyo - Courtesy of Allien

"Nimezaa na Kanumba' - Courtesy of Ngoshwe

Ramli kali.. Nyuma ya pazia kifo cha Kanumba - Courtesy of Bujibuji

Umaarufu wa Kanumba unanitia mashaka - Courtesy of PETER JOHN MLEY



[Lulu Related Thread to the Death of Kanumba]

...........................




"Ujinai" wa Lulu katika "Mauaji" ya Kanumba (R.I.P)- Courtesy of Woman of Substance

Tetesi-UTETEZI WA LULU: Kanumba alitaka kunibaka - Courtesy ya Rutashubanyuma

Je Lulu ana haki juu ya Kifo cha Kanumba? - Courtesy ya MPAMBANAJI.COM

Sakata la Lulu na Kifo cha Kanumba, What does the Law say?- Courtesy ya Majamba Jr.

Police wamuachie Lulu mara moja! - Courtesy of Rutashubanyuma

Ushauri alopewa Lulu na Lady Jaydee 2009 akiwa 14yrs - Courtesy of Independent Voter

Mh. Halima Mdee: Nitamsaidia Lulu kadri niwezavo - Courtesy of Mwitaz

Neno la Leo: Jamii ya walo wema Imsamehe Elizabeth Michael - Courtesy of Majid

Ushauri huu kwa Kanumba na Kifo chake - Courtesy of Kitalolo



The above ndio threads ambazo nimejitahidi ku compile. DISCLAIMER; Nimeweka threads tokana na uhusiano wake na the whole event. Kuweka kwangu hapa sio kwamba all details katika all threads ni valid and verified.


Pamoja Saana.

AshaDii...
Leo ni imetimia miaka 10, toka kifo cha nyota huyu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, na mpaka Leo, sio tuu pengo lake halijazibika, bali hajapatikana star mwingine yoyote wa kuvaa viatu vyake vikamfiti.

RIP Steven Kanumba, tutakukumbuka milele!.
Paskali
 
Back
Top Bottom