Steven Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya,Rufaa Yake Itasikilizwa Kesho

Steven Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya,Rufaa Yake Itasikilizwa Kesho

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Steven Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya........Rufaa Yake Itasikilizwa Kesho


Mahakama ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Bunda kesho.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne wa jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa sababu ya makosa yaliyofanyika kwa vile Wakili wa Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya kuitwa mahakamani.

Jopo la majaji linaloongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk liliahirisha usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo yasirudiwe tena kwa kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.

Warufani wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na Mawakili wa serikali, Obadia Kamea na Angela Msagala.

Wakili wa mjibu rufani wa kwanza wa Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi iahirishwe kwa muda mfupi kutokana na umuhimu wake.

Jopo hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na ombi hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.

“Inasikitisha, haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda wakati tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi tulikuwa tayari kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,”alisema Jaji Mbarouk.

Wakata rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani dhidi ya Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wakili Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa sheria za uchaguzi na kanuni.

Alidai tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana na viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha kura na taarifa ya mwisho ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.
 
Ninadhani ni mtu mchawi pekee anayeweza kuwa na roho za kama namna. Siyou bure. Ester Bulaya aombewe.

Hata mashona nguo yako vingine.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
a7fdc4c021e33d2c4c30e06c3064ec97.jpg
 
Ndiyo shida ya mtu aliyezoea siasa tu

Ova
 
daaa huyu mzee kuna jambo gani ajawafanyia wana Bunda toka enzi za nyerere aisee atupishe anapoteza muda wa watu kufanya maendeleo n kujadili kesi kila siku
 
"Asiyekubali kushindwa si mshindani" Mzee Wasira jipange kujaribu bahati 2020!
 
Back
Top Bottom