STOP BARRICK GOLD CAMPAIGN - Wabunge Simameni!

STOP BARRICK GOLD CAMPAIGN - Wabunge Simameni!

Mchakato wa kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa unawanufaisha watanzania unaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali na huyu balozi na ujumbe wakew wako kwenye state of panic kwa taarifa nilizo nazo mpaka sasa.

Hiyo state of panic ni signal kwamba wabunge wamemgomea ombi lake ama ni nini?

Tuombe Mungu CCM wasije wakakutana ili kuwekana sawa. Lakini nina amini kwamba kosa walilolifanya wakati wa Zitto hawawezi kurudia kufanya. Sasa ni zama za kuwahesabu wale ambao wako pamoja na wananchi na wale ambao wako kwa maslahi ya wazungu.
 
Hawa jamaa naambiwa kuwa wpo bize sana huko bungeni na wanakutana na kila mbunge,kinachotisha ni kuwa wanakutana na Mbunge mmoja mmoja sasa huenda huko ndio wanawaahidi kitu ama safari ama kamradi ka maji si unajua tena wabongo na mzungu?

Lazima kupiga kelele this time.

Kama kweli tuna waandishi wa habari(wazalendo) basi nategemea kesho magazeti yote yanaweka front page picha kubwa ya hawa ma lobbyst na wabunge......na headline....MADINI YETU NI KWA MANUFAA YETU
 
Hiyo state of panic ni signal kwamba wabunge wamemgomea ombi lake ama ni nini?.............

............... Sasa ni zama za kuwahesabu wale ambao wako pamoja na wananchi na wale ambao wako kwa maslahi ya wazungu.

Kweli mwaka huu Mwenyezi Mungu ametuonea huruma....hata Mzee wetu wa Mtera...kasema haya...

"Ningeomba kuomba mwongozo wako chini ya ibara namba 68(7) (ya Kanuni za Bunge). Jana tuligawiwa Ripoti ya Bomani, mtu ambaye alijulishwa hapa kwamba ni mtu mashuhuri, na wote waliokuwa katika tume ile ni watu mashuhuri, na ripoti hii ina mambo mengi sana ya muhimu na mimi ninafikiri labda ndiyo pengine wakati muafaka wa nchi yetu kupata sera mpya ya madini.

"Kwa hiyo kutokana na kuomba huo Mwongozo, ningekwenda kwenye ibara namba 37(6), kuomba kwamba ripoti hiyo ili tuifanyie haki ipewe muda wake iwe debated, ili tuweze kutoa maoni yetu na kutoa mapendekezo yetu. Kwa hiyo naomba kutoa hoja chini ya kifungu 37(6) baada ya kupata muongozo wako," alisema Malecela akishangiliwa na wabunge; wa CCM na wa Upinzani.

Tuombe iwe kweli maanake hawa jamaa wa CCM wengi ni kama Kinyonga
 
Napata taarifa kuwa kuna baadhi ya waandishi wameamua kuwauliza kwa kuwapigia simu na imefikia mahali wanajipanga upya kwani wamejikuta wakibanwa sana na waandishi na hata balozi mwenyewe.

Nitawapa nyeti baadae kadiri nitakavyoweza kuzipata.
 
hivi jamani ... mpaka lini, yani nachukia mapaka nakosa raha, hawa wazungu wanatudharau sana, wanatumia njaa zetu, sishangai kuumwa kwa ZITTO sasa,

hivi kwanza anaendeleaje??
 
Jamani tuwaombee wabunge wetu wawe na mshikamano na uzalendo wakati kama huu wa mtihani mkubwa kutoka kwa hawa Wakoloni mamboleo.....na nawaomba wabunge waangalie sana,na waone fundisho kwao, mambo yanaotokea huko kwa wenzetu wa Nigeria.....Tusije tukawa kama wao halafu watu wakaamini kama asemavyo Nyani Ngabu kuwa "waafrika ndivyo tulivyo".....Ndugu wabunge angalieni Mambo yanayotokea Nigeria


Elusive peace in Nigeria's oil Delta

By Andrew Walker
BBC News, Port Harcourt

An effort by the Nigerian government to bring peace to the oil-rich Niger Delta region hangs in the balance even before it has officially begun.
The government of President Umaru Yar'Adua is trying to organise a giant peace summit to end violence by gangs of armed youths that have disrupted oil production and seen it cut by around a quarter............

Last week, an attack by militants close to the Bonny Island Liquefied Natural Gas export terminal killed nine people, including a pregnant woman and four soldiers.................

Losing billions

The government plans to try and get thousands of key decision makers, including militants, to a summit where they hope a solution can be agreed to the problems of the Niger Delta.

Because oil prices are so high, the reduction in the country's oil production is costing it billions of dollars.

Unemployment is rampant.

Any young man on the streets will tell you, as oil militants also do, that oil companies and state governments have cheated the people of development and opportunities.

...The real problem, they say, is the connection between politics and violence.

Corrupt politicians and military officers use armed militants to steal oil and protect their lucrative positions in government.

"Most of what is going on here is sheer criminality," says Anyakwee Nsirimovu, a human rights activist based in Port Harcourt.

"If a state of emergency was declared and all the governors removed and independent-minded people put in, they could end this thing."

Without things like reliable power supplies, transport infrastructure and employment, people will remain dependent on the patronage of corrupt leaders and will be unable to speak out against them, he says.
"Not many people can speak the way I do, because they are afraid. Plenty of people spoke out in the day and were killed at night."

He says the government's intention to get militants to put their arms out of use is "absolute nonsense".

Story from BBC NEWS:
http://news.bbc.co.uk/go/pr/fr/-/1/hi/world/africa/7492870.stm
 
Balozi wa Canada adaiwa kushawishi wabunge kuikataa ripoti ya madini

Na Julius Samuel, Dodoma

BALOZI wa Canada nchini, Janet Siddall, yupo mjini hapa kuwashawishi wabunge ili wakatae mapendekezo ya ya ripoti ya Kamati ya Madini kwa kile anachodai kwamba yakipita yatawakimbiza wawekezaji wa sekta hiyo.

Habari zilizopatikana mjini hapa jana na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge, Balozi huyo alianza kukutana na wabunge mbalimbali wenye ushawishi mkubwa na wale wanaotoka maeneo ya yenye madini ili kuwaeleza madhara ya kupitishwa kwa ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa wabunge hao, Balozi huyo anasema kama ripoti hiyo ikipitishwa itakuwa na madhara makubwa kwa wawekezaji na hivyo watashindwa kuendesha shughuli zao hali itakayowalazimu kufunga shughuli zao nchini.

Balozi huyo aliwaomba wabunge hao waishauri serikali ikutane na makampuni ya madini, ili wajadiliane kuhusu kodi watakazolipa kwenye halmashauri.

Miongoni mwa kodi mpya zinazopendekezwa kwenye ripoti ya kamati hiyo ambayo habari zinasema kwamba imekwisha kupata baraka za Baraza la Mawaziri, ni ongezeko la kodi inayolipwa na makampuni hayo kwa halmashauri kutoka Sh200 milioni kwa mwaka hadi asilimia 20 ya mapato ya madini.

Jana machana Balozi huyo alikutana na wabunge wa Chadema, mbunge wa UDP na baadaye wabunge wa CCM, na ajenda yake ikiwa ni kuwashawishi ama kuibadili ripoti hiyo au kuikataa kabisa kwa kisingizo kuwa itaathiri sekta ya madini kiasi cha kuwalazimisha wawekezaji kuondoka nchini.

Mmoja wa wabunge aliyeshiriki mazungumzo na Balozi huyo ni Zitto Kabwe wa jimbo la Kigoma Kaskaziani (Chadema), ambaye alithibitishia Mwananchi kwamba alikuwa anawashawishi kupinga mapendekezo ya kamati ya madini ambayo iliundwa na Rais mwaka jana na ripoti yake kukabidhiwa kwake Juni mwaka huu.

Kabwe alisema kwamba wabunge wa Chadema walimweleza wazi kwamba hawako tayari kukwamisha ripoti hiyo inayotarajiwa kujadiliwa na Bunge kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 12 unaondelea sasa Dodoma, kwa sababu mapendekezo yake yamezingatia zaidi maslahi ya taifa.

Kadhalika, Kabwe alisema kwamba wamemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania ni nchi huru na aina haki ya kuamua mambo yake kama inavyoona inafaa bila kuingiliwa na mtu yeyote kutoka nje.

Kabwe alisema kwamba walimweleza Balozi huyo kwamba mikataba ya sasa ya makampuni makubwa ya uchimbaji madini ilifikiwa kwa kutumia sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ilitungwa kwa ushauri na ushawishi mkubwa wa Benki ya Dunia hali ambayo haikuzingatia kwa kina maslahi ya taifa.

Alisema sheria hiyo ina upungufu mkubwa katika kutetea maslahi ya taifa ndiyo maana pamoja na Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika, baada ya Afrika Kusini na Ghana, bado madini hayo hayajaweza kusaidia kutokomeza umasikini wa watu wake na wanaofaidi rasilimali hiyo ni makampuni makubwa ya nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Wilson Masilingi, alithibitisha kukutana na Balozi huyo na kujadiliana mambo mbalimbali, likiwamo suala la Darfur na Zimbabwe.

Kadhalika Masilingi alisema kwamba Balozi huyo alimweleza kuhusu ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu iliyoko Kanda ya Ziwa.

Hata hivyo, Masilingi alisema Balozi huyo hakutoa ushawishi wowote kuhusu ripoti ya Kamati ya Madini.

Source: Mwananchi
 
Balozi wa Canada hiyo ndio kazi aliyotumwa kuifanya na Serikali ya Canada?
 
Yaani hii haijakaa vizuri. Balozi anapewa ripoti ya Bomani kabla ya Wabunge( Watanzania) hii tu wabunge wanatakiwa kuizushia sheshe.
 
Mchakato wa kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa unawanufaisha watanzania unaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali na huyu balozi na ujumbe wakew wako kwenye state of panic kwa taarifa nilizo nazo mpaka sasa.


Heshima mbele MK

Tafadhali niambie hii ripoti inatarajiwa kujadiliwa lini bungeni? Nitashangaa sana endapo wabunge wetu watashindwa kutumia nafasi hii muhimu, kwa sababu tu eti wadeal na wazungu!
 
Breaking News ni kwamba Canada wame pull back kwasababu ya resolve...Then sasa wabunge waweke misimamo yao wazi mbele ya wananchi na si kwa kujificha ama kwa magrupu!
Kila mtu alisimama peke yake na kunyanyua kitabu kitakatifu na kuapa kuilinda katiba yetu...Tunataka utaratibu huo huo...Kuwa kila mbunge atowe msimamo wake.
Kwamba wanaisapoti Ripoti ya kamati ya madini ama la.
Na kama la...Then kwanini.
 
Wewe kwenu Komoro? au Tanzania?.Sijakuelwa unaposema kwenu hakuna Madini

Achana nae huyo, ndio hao hao wabaguzi wa majimbo. Hapa tunaongelea masuala nyeti sana ya taifa yeye analeta mzaa.
 
Lawama zote zimwendee msaliti na fisadi namba 1 wa taifa hili, Benjamin William Mkapa. Huyu mtu ametutia hasara kubwa taifa hili makusudi kwa mtazamo wake wa nje zaidi. Kila siku nitasema na nazidi kusema, sekta ya madini ni ugoro mtupu na hii inatudalilisha achilia mbali kutotuleta faida.Niliwahi kufanya kazi kwenye migodi ya dhahabu miaka 5 kama METALLURGIST, sitasahau siku consultant mmoja alikuja nakapewa nifanye naye mradi. Huyo bwana alivyokuwa akilalama kwamba nchi haifaidiki na chochote wakati gharama za uzalishaji ni ndogo kuliko sehemu nyingi duniani($/oz).. Alikuwa akiniuliza , kama nchi haikuwa na wataalamu wa kuingia mikataba , kwa nini isitafute watu hao nje na kuwalipa, badala ya kuingia mikataba ya kujiumiza!...Huyo ni mgeni nasikitika! Kuanzia hapo alinitia doa sana hata kufanya kazi huko migodini...nilijisikia kunyonywa na kudhalilika....hatimaye niliondoka.....lakini kila nikisikia issue ya migodi moyo hunienda mbio na kuanza kumlaani Mkapa na mbumbu wake aliowakokota kuangamiza taifa.

Wabunge tunawaomba msirubuniwe, ili nagalau kama tunaweza pata japo kitu kidogo cha zaiada tupate...maana tuliibiwa ati.....tutakacho recover tutashukuru...Ole wao vibaraka watakaopinga mapendekezo ya tume yenye maslahi ya taifa...tukishindwa kuwafanya lolote....nina uhakika Mungu hatawaacha.
MPAKA KIELEWEKE asante kwa mada hii kwani inagusa sana maslahi ya nchi...Mbunge wangu mtarajiwa TUNDU LISSU tafadhali pigania hili....nakuahidi kukupigia kampeni kwa wananchi wa jimbo letu, japo upeo wa wapiga kura wetu bado tatizo.

Mungu iokoe Tnazania kwenye mikono ya wanyang"anyi. Amen.
 
Uyo balozi ashindwe na alegee!
Watanzania tuamke pls,mgeni hawezi kufanya maamuzi juu ya mstakabari wa nchi yetu bse naamini kwa 100% Maoni ya akina Bomani hayatoki mbinguni lazima watakuwa walifanya comparative analysis.
Aluta Continua......wamekula ya mbuzi lazima waote mapembe
 
Leo asubuhi huko bungeni mzee Malecela ametoa maelezo yake kuwa alipotaka bunge liijadili ripoti hiyo hakuwa anaitega serikali ila alikuwa anataka bunge lipate muda wa kuisoma na kuijadili kwa kina.

Naendelea kufuatilia ushawishi unaendelea ama laa....
 
Back
Top Bottom