Stop Foreign Aid to Tanzania Campaign!!

What is “foreign” about the foreign aid that we get? Kwetu sisi misaada toka nchi mbali mbali sio kitu foreign hata kidogo.

Sasa acheni utani. Kama sii hii misaada hakungekuwa na chochote Tanzania. Kitu pekee non trivial ambacho kimeshafanyika Tanzania bila msaada ni ujenzi wa jengo jiya la BoT! Ni ujenzi wa sehemu ya kuchotea tu!

Ukiondoa barabara za misaada Dar utabaki na njia za TZ11 peke yake! Tuwaeleweshe kidogo wale waliozaliwa hospitalini:

  • Barabara ya Nelson Mandela kajenga Jarumani
  • Barabara toka Dar hadi Moshi kajenga Mwitalia
  • Maji yanayonyweka Rombo kayaleta Jarumani toka Marangu.
  • Salenda Bridge, Kawawa Road, Morogoro Road, kajenga Mjapani.
  • Kitivo cha Uhandisi UDSM, Arusha Technical College, kajenga Jarumani.
  • Watanzania waliosoma nje karibu wote wamesomeshwa kwa msaada
  • Maji safi kidogo mikoani yote ya misaada
  • Kilimo chote cha umwagiliaji ni cha msaada
Na hiyo list bado sana!

Mgonjwa aliye kwenye drip atasemaje mirija ndio imemdhoofisha?
 
Nani aliwasaidia Waswidishi, Wanorwei...?
Wamarekani! Which means you can't ask me "nani aliwasaidia Wamarekani"

I mean, Seriously dude! Are you really sure about this?? Perhaps I need to send you a copy of pre-modern world economy (history) book. Otherwise, you're just making stuff up!!!
 

Mwalimu ni kitu gani ambacho sisi wenyewe tunaweza kukifanya kwa uwezo wetu na fedha zetu wenyewe. Unafikiri misaada ya kigeni??? imetusaidia kuendelea na kiwango cha maendeleo kinaakisi misaada tuliyopokea hadi sasa?
 
Kila ninapofuatilia hii thread kisha nkataka kui_merge na ile ya "wabunge USA wataka kuonana na Zitto;je misaada isitishwe?" hasa katika page kama 10 hivi za mwanzo katika ile thread.Kwakweli napata mawazo yanayokinzana hasa ukizingatia kuwa maoni yanatoka kwa very same people,but ni opposite.Does this imply the human nature of acting/behaving according to the circumstance or its a lack of concistence??
Ushauri wangu ni kuwa kabla ya kuzungumza kuhusu kusitisha misaada ni vema tukajiuliza kama tumeshajijengea mazingira 'bora' ya kutuwezesha kusimama imara na pia kutusongesha mbele.
 
Kaka Mwaky, trust me, njia ipoo. Unajua unapokuwa na shida ndio mara nyingi unapata akili ya kutatua tatizo lako, lakini kama sii hivyo utauacha tu Ubongo wako ulalae kwa sababu kila siku unajua kwamba fulani atalishughulikia hili tatizo. Kwa mfano mimi sasa hivi ndio nina watoto wadogo na ninaishi peke yangu na ndio nimetia akili na najitafutia na kufanya mambo yangu, lakini kabla ya kuanza kuishi peke yangu nilikuwa nategemea wazazi na siishughulishi akili yangu kutafuta, lakini sasa hivi maana yake nisipotafuta mimi , mimi na familia yangu tunakufa njaa, kwa hiyo nitatafuta kila njia ili tu-survive. Na kwa Tanzania Rasilimali zipo na ardi ipo na watu wapo kasoro uongozi (Baba) ndio mbovu. Ila huo uongozi ukipata shida ni kweli utafanya kazi. Na kama misaada ikisitishwa na kweli mambo yakaenda kombo Bongo ndio mwanzo wa watu kuwakataa viongozi ambao watakuwa hawana vision ya kuendeleza Tanzania. na viongozi ndio kweli wataanza kuangalia mikataba ya Madini na kila kitu, kwa sababu ni lazima watumie akili, sasa hivi wanasafirii tuu kuomba misaada we unaona ni akili hiyoo?!
 
Hivi kama huoni mapungufu una sababu gani ya kutafuta suluhisho la matatizo yako? Kama kile tukisema hatuna bomba la maji wafadhili hao, tukisema hatuna madarasa wafadhili hao, tukisema hatuna magari ya mradi wa kujenga mashule na kuchimba visima wafadhili hao; hivi kuna siku tunaweza kuangalia kama tunawahitaji kujenga madarasa au tumeshajiambia mawazoni mwetu kuwa bila ya misaada hiyo hakuna maji wala madarasa? Tuna ulemavu gani sisi wa kushindwa kufikiri?

Wakati JK amekuja US mara ya mwisho alikuja kupokea na misaada ya vitabu vya karibu dola 125,000 (nikikumbuka sawasawa). HIvi kweli mnataka kuniambia Tanzania tunahitaji msaada wa dola 125,000 kununua vitabu?

Alhamisi huko Mpwapwa imefunguliwa kliniki iliyojengwa kwa msaada wa Wamarekani, kweli hatuwezi sisi kujenga hata kliniki moja sisi wenyewe?

HIvi akija mtu kwako nakukuambia anataka kukununulia gunia la mahindi (si kwa sababu hauna uwezo bali kwa sababu anafikiri huna sababu ya kutumia uwezo wako) utakubali gunia hilo la mahindi? Jibu la Watanzania wengi sitoshangaa ni kwua "ndiyo kwa sababu la bure!"!
 
Katika mazingira hayo tunaweza kuomba watuchagulia Rais na wasaidizi wake; Sasa tukiwakaribisha kwa hiari yetu waje watutawale tunaweza kuuita huo ni "ukoloni" au ndiyo "urafiki wa karibu"?

Wakitusaidia kutuchagulia viongozi itakuwa bomba maake hakutakuwa na watu kama Kingunge katika uongozi.
 
Who and how will we plug the hole if your campaign is successful? Unajua mkuu ni lazima uwe na meaningful alternative unapotaka kitu kikubwa kama hiki kifanyike.
 
Wanabodi,
Misaada ni muhimu sana ktk maendeleo ya nchi zetu isipokuwa kosa ni KUTEGEMEA misaada..
Nitawapa mfano mmoja mzuri sana kati yetu sisi wenyewe..Hakuna kati yetu aliyeanza maisha na mokono mtupu kuna mtu ama watu waliojitolea maisha yao kutubeba.
Aidha umepata mkopo (msaada) toka benki ama kwa ndugu yako siku zote malengo ya mkopo huo ni kukuwezesha wewe usimame kwa mguu yako -
Planning ndio kitu muhimu na tatizo la Tanzania ni pale tunapoishi kimaskini yaani kila siku ya maisha yetu tunajipanga msikitini kusubiri sadaka!

Je, kuna mskini ombaomba yeyote yule aliyeweza kuondokana na Umaskini kwa kutegemea sadaka?.. Sas tuseme Tanzania sio maskini anayejipanga msikitini kuisubiri sadaka, tunakopa misaada hii lakini bado ktk maisha ya Kibongo bongo, mtaji tunaokopa unakwenda ktk matanuzi. Ni wangapi kati yetu mliojaribu kusaidia ndugu zenu kwa kutoa mikopo ama misaada na wakaiwasha!..Wengine watafungiwa makanyaboya ktk biashara wanayojaribu... wengine mtaji uliompa ndio haurudi basi fanya la maana hakuna..kesho yupo palepale akiomba tena kwa machozi ati Mungu hakumjalia...Damn!
Nchi nzima imejaa matapeli kiasi kwamba hakuna hata moja linalokwenda kwa sheria..Kila mtu na mzigo wake ndio mfumo unaotembea nchini leo hii toka kwetu sisi wananchi hadi serikali kuu..Utapeli na kila mtu na mzigo wake...
Sasa tunapokuja hapa na kujadili kuhusiana na misaada wakati sisi wenyewe hohehahe hatuna hata moja tunaloweza kulifanya bila Utapeli na maslahi binafsi kuwa mbele sijui kusimamisha hii misaada itatupeleka wapi..Ni uwezo gani tuliokuwa nao ambao kweli mnafikiria tunaweza kujenga hata barabara moja moja!
Jamani hizo barabara za Moshi, Mwanza, Mbeya, Songea zote ni lane moja tu na bado zina hitilafu kibao wakati wa masika. Miaka 50 ya Uhuru tumeshindwa kabisa kukamilisha hata moja acha miradi ya maji safi, lishe, afya na kadhalika...wanakwenda sifiwa kina Mkapa waliojenga a bridge to Nowhere!

Hata Maleysia waliweza kufanikiwa baada ya kupunguza kutegemea misaada. zikajengwa mbinu za kuwawezesha kujijenga kwa mtaji waliopata hata kama ni msaada...Ujumbe ni kwamba hawakurudi tena kuomba msaada baada ya kupata mtaji.. walitumia misaada kujenga misingi bora ya kiuchumi hasa infrastructure na viwanda kulingana na mazingira ya kiuchumi duniani. waliona mbali zaidi ya kufikiria utajiri wa mtu binafsi. Sisi ndio kwanza mtaji wetu tunashindana kujenga maghorofa..
 
wamarekani wakisaidia basi ujue wanahesabu zao tofauti na msaada.
 

Wakati tukiwa occupied under colonialism ulitaka wasafirishe vipi bidhaa(Raw Materials) na manamba wao? Ama wafanyakazi wao?

Kule Iraki sasa zikijengwa barabara ni Chenney/mmarekani amejenga kwasababu ndiye mwenye makampuni ya ujenzi?

Mkuu uhuru bado hatuna hilo liko wazi...Mtu mzima kuendelea kuwa omba omba ni noma....Halafu kwa maoni yangu ni kuwa kabla hatujaendelea kuomba omba, tujiulize kile tulichoomba kimefanya nini..Tukianza kufuatila kwa undani ccm wote makada mtafilisiwa kiaina kwani ni utamaduni ambao kama ulivyoelezea hapo juu ni ugonjwa..Na kwa kweli drip ipo tu na kisiasa ccm ipo mahututi....Na ninakuhakikishia kama hakutakuwa na mabadiliko drip inaweza katwa...Msitudanganye kuwa masikini wananufaika na misaada zaidi ya mafisadi na wale wasiokuwa waaminifu wenye mawazo ya kifisadi.

Ni kivipi tuendelee kukubali kutawaliwa na watu wabaya wasiojali? Mabadiliko ni lazima ndugu yangu hakuna cha kuendelea kupewa misaada kwa kutumia vigezo vya ujenzi wa mkoloni aliyetupa uhuru wa bendera...Sasa ulitaka nani ajenge hivyo vitu na wakati hakujawa na mkakati wowote wa maana wa kuiinua Afrika kiteknoljia?

Ukiritimba unaendelezwa na fikra flani hivi ambazo ni HATARI sana na ni za kitumwa kwa kusema ukweli.
Kama hakuna mapinduzi...Narudia tena...Hatutakwenda mahali.
 
Hatujaanza leo wala hatukuanza jana kupinga misaada isiyo na kikomo….

Risiti zipo!
 
Enzi hizo kabla hujawa compromised na siasa za JPM (Rip).
 

Enzi hizo Kitila ukiwa Mwanafunzi.

Leo uko CCM na akili imebadilika. Sasa umekuwa ni Mdhihili wa Mdhihili wa miaka hii. Issue za hovyo hovyo kama DPW wanakutanguliza wewe kufungua gunia la FUNZA.
 
You can't believe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ludicrous na nchi bado masikini wa kutupwa
 
Majibu yangu yatarudi huko huko Wamarekani. Nchi yoyote utakayouliza jibu lake ni Wamarekani.
Nyani anauliza swali zuri sana, kwa nini Marekani au Uingereza watusaidie? Nani anawasaidia hao? Kwani sis hatuwezi hata kujisaidia? Common: Ardhi, watu, na resource nyingine; sisi tangu siku nenda kale ni kuomba tuuuuuu
 
I can't imagine Tanzania bila hii misaada itakuwaje?
Tumeizoea sana mpaka tunaona kama ni wajibu wao kuendelea kutupa misaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…