Wakuu poleni na majukumu..
Nimeagiza gari (Subaru Impreza) na itaingia mwezi wa 11 mwanzoni, hapa majuzi nimepata dharula hivyo hela ya kutolea imepungua.
Nategemea kuweka mambo sawa miezi miwili au mitatu ijayo ndio niitoe.
Ninachotaka kujua, je gari ikikaa pale bandarini inachajiwa kiasi gani kwa mwezi? Je ni baada ya muda gani gari inaweza pigwa mnada? Naombeni majibu yenu ili nijue cha kufanya.
Natanguliza shukrani.
Mkuu nimeona mtu sehemu anazungumzia swala la Custom Bonded Warehouse bora hio gari yako ukaipeleka huko kwenye Custom Bonded warehouse kwa gari ndogo kama yako unalipia $100 kwa mwezi cha msingi tafuta bonded warehouse ili ikifika waipeleke huko maana ikikaa bandarini hio gari yenye CBM 13 itakua 1.5USD x 13 = $13 USD + 2.34 USD Vat = 15.34USD per day kwaio zidisha mara siku utakazoiacha hapo bandarini utapata jawabu
Embu jaribu kuwatafuta watu wa bandari wakupe tathmin kamili manake nasikia ni gharama kuilaza hapo ndio maana mengine watu wanashindwa kuyakomboa na kuishia kupigwa mnada,au pengine wasiliana na mwagizaji anayekuletea gari kwa branch ya nyumbani kama wanaweza kuifanyia clearance alafu associated costs mkalipana baadaeShukrani mkuu ubarikiwe.. Ngoja nifanye huo mchakato kabla gari haijafika!