Stori: Uko wapi rafiki? Kuna cha kujifunza hapa?

Stori: Uko wapi rafiki? Kuna cha kujifunza hapa?

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Habari zenu wanaJAMII!

Kuna cha kujifunza ktk hii true story!

Ulikuwa umetoka kumaliza Form 6. Ulikuwa unaishi maeneo ya Ubungo, jirani na kituo cha dala dala maarufu BAKWATA, kati kati ya RIVERSIDE na HOSTEL.

Siku moja usiku, ulipata ajali mbaya Mandela rd. Uligongwa na gari iliokuwa ktk mwendo kasi mkubwa, ulikuwa unavuka bara bara ya Mandela, kutoka upande wa Ubungo islamic.

Gari iliokugonga haikusimama, na hatukuweza kusoma number. Uliumia sana, nguo zako zilipasuka, ulikuwa umevaa suruali tight, handbag, saa, viatu vilitupwa mbali mbali!

Ilichukua muda mpaka ulioanza kutoa sauti za kuugulia maumivu (tulihisi umefariki). Wengi waliogopa kukusaidia kwa hofu ya usumbufu wa polisi hapo baadae.

Nikaingiwa na imani. Nikajitolea kukusaidia, angalau ufike hosp! tulisaidiana na vijana wengine kuhakikisha vitu ulivokuwa navyo vinakuwa salama.

Kisha tukalazimisha magari kusimama ili upatiwe msaada, wabongo wenye magari baadhi wagumu, waligoma kusimama, tukapata wazo la kufunga bara bara ya Mandela ule upande wa kuelekea Ubungo.

Ilituwia vigumu kwa nyakati zile za usiku, baadae tulipata STJ ambayo kwa hekima zangu za elimu ya kdt cha 6, na kumsomesha sana, dereva wa STJ, tena usiku wote ule, alinielewa.

Kikubwa nilimueleza kuwa, tuna dada hapa, amegongwa na gari na dereva amekimbia. Nakumbuka dereva wa STJ aliniuliza kama wewe ni majeruhi ama umekufa, nikamuhakikishia kuwa wewe ni majeruhi, akaniuliza: "mbona haongei" Nikamjibu "amepoteza fahamu"!

Alinikubalia ombi langu!
Akafungua mlango, tukakubeba msobemsobe mpk ktk gari. Ghafla watu wote wakatawanyika na kuniacha mm na dereva tu, huku na mm nikionyesha dalili za kuondoka! Dereva kwa ukali: alinikalipia kuwa kama siwezi kwenda na wewe hospitali, basi nikushushe.

Nikaamua kupanda ndani ya gari. Safari Muhimbili. Tukaja mpaka Ubungo mataa, then tukaingia Morogoro rd, tunaitafuta Muhimbili.

Nilishangaa dereva kutokuingia Magomeni police. Nikamkumbusha dereva, kuwa tunatakiwa kuwa na PF3, akiwa kavurugwa akasema: "hii gari ni ya serikali, unajuwa inatakiwa kulala saa ngapi?"

Sikujibu! Moyoni najisemesha "nimelikoroga, nalinywa peke yangu, jela inaniita (akili ilikuwa inawaza kama majeruhi wangu atanifia)"

Njia nzima ulikuwa unaugulia maumivu makali, na hasa maeneo ya kiuno na mguu wa kushoto(Mungu Mkubwa, ulikuwa umeumbika, ulikuwa na mwili wa kabila la wa-Xhosa)!

Nilitumia fursa hiyo kukuuliza majina yako (km cjakosea ni Elizabeth), umri, ndugu zako, mtaa na nyumba unayoishi! Nashukuru mungu ulijaribu kuyajibu!

Tulifika Muhimbili saa 5 usiku, tulipokelewa vizuri tu! wakaleta kitanda cha matairi, wakakubeba mpaka ndani! Nilifanikiwa kuandikisha maelezo machache pale kuhusu wewe! Wakaniomba PF3, nikawajibu sina, hatukupata muda wa kuipitia. Nikaambiwa nikatoe maelezo kituo cha polisi Superstar, nikaenda!

Kurudi - nikakuta ushapelekwa chumba cha x-ray, nikaambiwa mtu wa x-ray amelala, kwa hiyo mgonjwa wangu hawezi kuhudumiwa mpk asubuhi! Nazifahamu sana lugha hz! Nikatoa elfu 5 (ipe jina utakalo).

Muda tena, nikaambiwa nikakununulie dawa ya maumivu, nikaenda! Sifahamu nini kilitokea, lkn ulipigwa x-ray ndani ya dak 5. Wakasema umevunjika mguu. Kuwa hukuwa na madhara makubwa. Wakasema utalazwa na utaendelea kwa matibabu zaidi.

Muda kidogo, kama saa 6.30 walikuja polisi kuandikisha PF3. Nilipenda maswali ya polisi wale. Ilikuwa hv:

Polisi: una uhusiano gn na hy majeruhi?
Mimi: simfahamu!

Polisi: DSM watu hawatoi msaada kwa watu wasiowafahamu, kwa nini kijana umeweza?
Mimi: Huruma yangu tu.

Polisi: Sisi tunaamini wewe ndiye uliemgonga kisha ukajifanya Msamariamwema. Unabisha?
Mimi: Afande mimi sina leseni na wala sijui kuendesha gari.

Polisi: Hatuamini maelezo yako kijana.
Mimi: Naomba mniamini (nilishaingiwa na hofu.)

Polisi: kwenu wapi?
Mimi: Buguruni?

Polisi: Huyu ulikuwa nae guest.
Mimi: Hapana afande, katoka ktk mizunguko yake, mm simfahamu kabisa!

Polisi: umewezaje kujua majina yake, anapokaa, umri wake? km si mpenzi wako?
Mimi: nilimuhoji alipojiwa na fahamu akanijibu yote hayo.

Polisi: Utakuwa tayari kutupeleka eneo la tukio?
Mimi: (tayari walishanivuruga) Nikatikisa kichwa, kwa alieniona asingeweza kusema kuwa nilikuwa nakataa ama nakubali! Haikueleweka!

Hatimaye nikapewa PF3 pale pale viunga vya Muhimbili!

Kama kuna kitu umejifunza ktk mkasa huu, ama kuna hisia zimekujia, tiririka! Comments zenu zitanifanya nirudi ama nisirudi kumalizia, my life experience!



Part II


Tulipoishia muda ule!

Polisi: kwenu wapi?
Mimi: Buguruni?

Polisi: Huyu ulikuwa nae guest.
Mimi: Hapana afande, katoka ktk mizunguko yake, mm simfahamu kabisa!

Polisi: umewezaje kujua majina yake, anapokaa, umri wake? km si mpenzi wako?
Mimi: nilimuhoji alipojiwa na fahamu akanijibu yote hayo.

Polisi: Utakuwa tayari kutupeleka eneo la tukio?
Mimi: (tayari walishanivuruga) Nikatikisa kichwa, kwa alieniona asingeweza kusema kuwa nilikuwa nakataa ama nakubali! Haikueleweka!

Hatimaye nikapewa PF3 pale pale viunga vya Muhimbili!

Kama kuna kitu umejifunza ktk mkasa huu, ama kuna hisia zimekujia, tiririka! Comments zenu zitanifanya nirudi ama nisirudi kumalizia, my life experience!


Karibu tena!
Ilipotimu kama saa 7 usiku, majeruhi wangu, aliekuja kuwa rafiki yangu, japo kwa muda mfupi, alishapatiwa kitanda katika moja ya wodi pale Muhimbili. Mpaka napewa taarifa kuwa amepewa kitanda, sikuwa najuwa kuwa muda tu, walishamchoma sindano (nahisi) ya usingizi. Hivo sikuweza kumuaga, nikaweka nia kwenda kumuona kesho yake asubuhi.


Huku nje napo, wale polisi walikuwa wakinisubiri ili safari ya Ubungo, eneo la tukio, ianze. Ile najitokeza tu, mbele ya macho ya polisi wale, nikaskia sauti ya polisi mmoja akisema: Msamariamwema aliemuokota ndugu yenu ndiye huyu hapa!

Ndugu wa manusra wangu wamefika muhimbili, kufuatilia nini kimemkuta mpendwa wao, nikawaangalia haraka haraka kuona aina ya facial expression waliokuja nayo, nikajua wamejawa na mchanganyiko wa taharuki, machungu na shauku!

Mpendwa rafiki yangu, kulikuwa na dada yako mkubwa, dada yako mwingine, mdogo wako na boyfriend wako. Dak 3 za salamu, zilitosha kunipa picha kuwa, wale watu wa jinsia ya kike walishalia sana, nadhani sura zao zilionyesha kuishiwa na machozi. Waliniparamia huku wakiwa na shauku ya kujua hali ya ndugu yao!

Dada mkubwa alikuwa na nguvu ya ziada, alikumbuka kunisalimu, akanishika mkono! Akanipa pole! Akanipa hongera! Akaniomba niseme, hali ya mgonjwa! Nakumbuka nilisema kwa ufupi sana, maneno mawili tu, "hajambo, amelazwa"!

Baada ya kuskia hivi, ndio ikaja akili, wakaomba tukae chini, dada mkubwa aliomba kujua uhalisia wa tukio zima! Nikiwa na uchovu uliopitiliza, sina hamu ya mahojiano ya tukio lile, niliisi kazi imeanza upya ktk hatua ambayo niliamini naimaliza kazi!


Polisi wetu wakasisitiza tuzungumze kwa ufupi ili safari yetu ianze kwenda eneo la tukio! Wakati naanza kuwasimulia wale wana ndugu kuhusu tukio lililompeleka ndugu yao Muhimbili, kulikuwa na maswali yanachomekewa na wale wadada, hapa na pale, nikawa nayajibu huku lugha yangu ikimaanisha, nimechoka naomba tumalize niondoke hapa!

Ilifika zamu ya Yule mtu wa kiume (nilikuja kujua baadae kuwa ni bf wako) kuuliza swali! Swali lake la kwanza lilikuwa la ajabu, ni swali lililochanganyika na majibu, naomba nimnukuu Yule mtu wako, ewe rafiki yangu:

"wewe ni mwanaume, unawezaje kumsaidia mtoto wa kike, usie na uhusiano nae, tena usiku? Nyie mtakuwa mmetoka guest, kwa haraka zenu mwenzio akagongwa na gari!

Wewe unamjua huyu binti, acha ujanja bwana mdogo!" wakati najaribu kumuelezea kama sio kujitetea, jamaa akanikunja kwa ile style ya kunisimamisha kutoka pale chini nilipokaa! Ghafla Polisi wetu wakashtuka!


Tukutane baada ya ftari!



Part III

Tulipoishia jana:

Polisi wetu wakasisitiza tuzungumze kwa ufupi ili safari yetu ianze kwenda eneo la tukio! Wakati naanza kuwasimulia wale wana ndugu kuhusu tukio lililompeleka ndugu yao Muhimbili, kulikuwa na maswali yanachomekewa na wale wadada, hapa na pale!

Ilifika zamu ya Yule mtu wa kiume kuuliza swali! Swali lake la kwenza lilikuwa la ajabu, ni swali lililochanganyika na majibu, naomba nimnukuu Yule mtu wako rafiki: "wewe ni mwanaume, unawezaje kumsaidia mtoto wa kike, usie na uhusiano nae?

Nyie mtakuwa mmetoka guest, kwa haraka zenu mwenzio akagongwa na gari! Wewe unamjua huyu binti acha ujanja bwana mdogo!" wakati najaribu kujitetea, jamaa akanikunja kwa ile style ya kunisimamisha kutoka pale chini nilipokaa! Ghafla Polisi wetu wakashtuka!

Tukutane baada ya ftari!

Leo tena:

Polisi wale wakaingilia kati purukushani ile, wakanitoa mikononi mwa mbabe-mp***vu Yule! Polisi wakajipa jukumu la kumuelimisha Yule mbabe – mpu**avu, hapa ndio sehemu nyingine nilipowapendea Polisi wale!

Yupo mmoja wa polisi wale alinifurahisha kwa namna alivompiga maswali mkorofi wangu:



  1. Hata kama jamaa anakumegea demu wako, bado lazima umpe hongera kwa kuwa amemjali wakati alikuwa na fursa ya kumtelekeza!
  2. Dsm hatuna watu wa hivi, huyu bwana mdogo hana nia ovu hapa, ndio maana amejitolea muda wake na pesa kumsaidia huyu binti!
  3. "Utakuwa huna akili wewe," alisema mwanausalama mwingine! Unajua gharama ya hela ambayo huyu bwana ametumia mpaka mtu wenu anapata matibabu hapa, eeeeeeh!
  4. Alifoka Mwanausalama yule, akaendelea! Kijana pole, hongera kwa kumsaidia Yule binti, lakini pole kwa kuwa umeanza kulipwa maumivu hapa hapa! Afande tumchukue huyu mpum**vu…..!


Mazungumzo yangu ya nini kilitokea kwa wale jamaa wa manusra wangu, yalifika kikomo kwa kuwa kulikuwa na mada mpya imeingia - kuwasihi wanausalama wale wasiondoke na Yule "mbabe – mpu**avu!"

Aibu na fedheha aliyosababisha Yule bwana ilitukwaza wote pale, hasa mimi ambaye sikuwa nimefikiria kitu kama kile.

Rafiki yangu, Yule dada ako mkubwa ni muungwana sana, aliwaomba wale polisi wanipe fursa, nitaje gharama nilizotumia ili anirudishie. Nilikataa. Dadako alinibembeleza sana, kutaja kiasi ambacho nimegharamia mpaka kufika muda ule. Nilikataa.

Yupo nesi mmoja, alikuwa akishuudia zile vurumai, aliingilia kati mazungumzo yetu na akaanza kumorodheshea dada yako pesa ambazo nilitumia pale hospitali mpaka wewe - manusra wangu ulipopatiwa kitanda!

Alitaja gharama zote tena kwa kiasi kile kile nilichotoa pesa, na kamwambia dada kuwa "sijui kwa huko nyuma walipotoka, ila kwa hapa ametumia pesa hizo kwa ndugu yenu".

Dadako alitoa kiasi cha pesa ambazo sikuweza kujua ni kiasi gani kwa kuwa zilikuwa zimekunjwa ktk muundo wa "msokoto", bado nilikataa! Nilisisitiza hakukuwa na sababu ya kulipana, cha msingi tuweke nguvu ktk afya ya Mgonjwa wetu!

Nakumbuka gharama halisi za pesa nilizotumia kwako, kwa usiku ule hazikufika hata elfu 30, ila ni zaidi ya elfu 20. Pesa ambazo dadako alitaka kunipa zilikuwa ni zaidi ya hata elfu hamsini (nilihisi kwa macho ya usiku ule na namna zile noti zilivosokotwa).

Baada ya kuzikataa pesa, dada aliniomba namba yangu ya simu, bahati mbaya sikuwa na simu (ndio kwanza nilikuwa nimetoka kumaliza A – level, na kipato changu kilitokana na kufundisha tuition wanafunzi wa secondary, maeneo ya mwenge, DSM, nyuma ya NAKIETE PHARMACY, tutiton yetu ilikuwa maarufu kama MAPAMBANO, ama kwa MUSSA au P.Diddy).

Dadako alichoka kabisa, kwake aliniona mimi ni mtu ambae anaitaji kuwa na mawasiliano naye mara kwa mara kuanzia siku ile! Kufika hapo, dadako mkubwa akawa hana namna ya kuwasiliana na mimi.

Akaniuliza ninapoishi nikamjibu – BUGURUNI, akazidi kuchoka kwa kuwa alijua siwezi kumtajia jina la mtaa, na pia namba ya nyumba. Huku kwetu namba za nyumba ni muhimu zaidi kwa serikali, tena serikali ya mtaa kuliko hata sisi wakazi wa nyumba hiyo!

Kwanza hata kichwani haikuwepo, japo najua nyumba ninayokaa, pale juu ya mlango wa nje kuna namba! Kwetu majina ya mitaa ni ya wazee maarufu ama mti mkubwa! Kufupisha mazungumzo yale, dada akanisihi mapema asubuhi kesho yake nifike pale hospitali, bila kukosa, ombi lake lilikuwa ndani ya uwezo wangu!

Kitu kimoja ambacho nilifanya kabla ya kuondoka na wanausalama wale, niliwatajia jamaa zako amana zote ulizokuwa nazo mpaka unapatwa na masaibu yale.

Niliwaambia kuwa, ulikuwa na mkoba (handbag), ulikuwa na saa ya mkononi, ulivaa viatu – mchuchumio, ulikuwa na simu, ulikuwa na herein za dhahabu, ulikuwa na handkerchief.

Tulivikabidhi hivi vitu kwa mama mmoja, msamariamwema aliekuwa anauza duka la dawa pembeni ya Mandela rd, ni mama huyu ambae alipekuwa mkoba wako (kujiridhisha) na kukuta pamoja na vitu vingine, ulikuwa na pesa.

Niliwatajia jamaa zako hizi data, na kuwaomba waende wakaonane na mama huyu, wajitambulishe, wapewe amana zako zote! Na kama kutakuwa na tofauti kati ya vile nilivoeleza na vile watakavyopewa na mama Yule, nilimuahidi dada kuwa, nitakuwa tayari kutoa ushirikiano!

Mpaka kufika saa 8 usiku ule, tayari tulikuwa eneo la tukio, Ubungo, maeneo ya kituo cha dala dala BAKWATA. Wale ndugu wa manusra wangu waliondoka kivyao, hususani baada ya Yule "shemeji" kutibua hali ya hewa!

Hapa maofisa wa polisi hawakuwa na maswali mengi. Walihoji na kutaka kujua vitu vichache sana kama:


  • Hilo gari uliliona kwa macho yako?
  • Lilikuwa la aina gani?
  • Gari lilikuwa linatokea wapi?
  • Huyu manusra wako alikuwa anatoka upande gani na anavuka kwenda upande gani?
  • Wewe na wenzio mlikuwa mmekaa wapi?


Ni maswali ambayo yalikuwa yanajibika. Niliwajibu vizuri, huku nikijua nipo mbali na hatari dhidi ya wanausalama hawa, na kuwa hii ndio ng'we ya mwisho, na mimi nirudi nyumbani, nikajipumzishe.

Walinishukuru wanausalama wale, wakaniomba wanipe lift mpaka Buguruni, baada ya mimi kuwaambia naishi Buguruni. Wakanisihi nisikose kwenda kumjulia hali mgonjwa wangu ifikapo kesho asubuhi, kitu ambacho hata wasingesema, nilishaweka nia!

Niliamka salama, japo na uchovu wa kutolala kwa kutosha. Safari ya Muhimbili ikanihusu. Nilibahatika kuwahi Muhimbili.

Ngojeni kwanza, baadae nitarudi, kuna kionjo cha Mkude Simba hapa e.fm nakiskiliza!

Part V

Walinishukuru wanausalama wale, wakaniomba wanipe lift mpaka Buguruni, baada ya mimi kuwaambia naishi Buguruni. Wakanisihi nisikose kwenda kumjulia hali mgonjwa wangu ifikapo kesho asubuhi, kitu ambacho hata wasingesema, nilishaweka nia!

Niliamka salama, japo na uchovu wa kutolala kwa kutosha. Safari ya Muhimbili ikanihusu. Nilibahatika kuwahi Muhimbili.

Bado nakumbuka rafiki yangu. Nilikuwa wa kwanza kufika pale MNH. Na kwa kuwa ulikuwa ni muda wa kuona wagonjwa, nilipitiliza moja kwa moja hadi wodini. Ilikuwa rahisi kukumbuka. Niliukumbuka mtindo wako wa nywele uliokuwa nao tangu jana yake, siku ya ajali.

Pia nilikukumbuka kwa urahisi, hasa baada ya kuona mguu wako umevishwa POP, lile vijana wa mtaani wanaita ogo (sina uhakika kama sio hogo!). nilifika mpaka kitandani kwako.

Nikakusalimia. Ukaitikia. Ndani ya nafsi ukawa katikati ya hisia kwamba huyu ndiye Msamariamwema aliekuokota ama ni mtu mwingine.
Wakati nikiendelea kukusikiliza, ukielezea namna ulivolala usiku ule wa kwanza ndani ya MNH, ukifafanua na maumivu ulioyaskia usiku ule!

Ghafla kikundi cha wwatu, zaidi ya watano, ukawaona wanaingia. Nilikuona ukitabasamu. Kwa sauti ya chini, sijui ulikuwa ukininong'oneza ama kunielekeza, ukasema: "jamani, dada Yule!" Nilipogeuka na mimi, niliwakumbuka watu wawili. Nilimkumbuka dada yako mkubwa. Nilimkumbuka na Yule rafiki yangu, mwenye makeke mengi. Nakumbuka vizuri, Yule jamaa hakuweza hata kunisalimia, alishindwa.

Rafiki yangu, unakumbuka namna dada yako mkubwa alivonikumbatia kwa furaha, kwa mashamsham tele, na alilitaja jina langu kwa ufasaha (sio slim5) kama vile ni watu tunaofahamiana vzr kwa muda mrefu.

Na mimi nilionyesha kumfurahia dada yako. Alionyesha kushangaa sana kuona nimemudu kuwahi MNH. Pia aliniuliza kuhusu jana, nini kiliendelea kule Ubungo, eneo la tukio, baada ya mimi kuondoka na wale wanausalama. Niliwasimulia yote. Ulionyesha kuguswa sana na simulizi yangu kwa lile jopo la wanafamilia yako na Yule mpenzi wako.

Mungu wangu.
Kumbe rafiki yangu hukuwa na kumbukumbu nzuri ya nini kilikupata usiku wa jana. Dada yako mkubwa alinisaidia kazi hii. Alisimulia vizuri sana namna mfululizo wa matokio ulivokuwa unakufuata usiku wa jana, huku mimi nikitumika kujalizia maelezo. Muda wote huu, Yule mtu wako hakuwa na kauli hata moja. Alikuwa bubu ghafla.

Nakumbuka rafiki yangu, ulivoanza kutoa mfululizo wa maneno, mengi sana, yaani mengi mno, yote yalilenga kuelezea namna unavonishukuru, nilikuona namna ulivoishiwa maneno yenye kumaanisha unanishukuru. Nilikuomba usiendelee sana na shukrani zako, lakini bado ulisisitiza kunishukuru. Nilielewa nini ulimaanisha. Na mimi nilikushukuru sana.

Dada ako nae alitumia muda kidogo kunipamba na sifa mbali mbali, mstaarabu, muungwana, mwenye huruma, mjasiri, mwenye kujitolea, una moyo wa ajabu! Sifa zilikuwa nyingi sana. Nakumbuka. Nilikuwa nampiga kijicho jamaa yako muda wote ambao nilikuwa nasifiwa, nilikosa maelezo ya namna sura yake ilivokuwa ikibadilika badilika.

Alikuja nesi, akatoa maelezo ya pamoja kuhusu hali yako na maendeleo yako. Tulimshukuru sana nesi Yule. Nakumbuka dada yako alimpa na hela ya chai. Nesi Yule nae hakuwa mchoyo, aliwaomba wale wanafamilia yako, warudishe shukrani kwangu, akidai nimefanya kazi kubwa sana. Na mimi nilimrushia mpira yeye mwenyewe nesi kuwa, ndiye anaestahili kupewa sifa zote!

Muda wa kuona wagonjwa ukawa umeisha! Tukakuaga. Ukamuomba dada yako, ahakikishe anakuwa na mawasiliano mazuri na mimi, ikibidi apajue nyumbani ninapoishi (dadako alikujibu, kuwa sina simu). Ulisisitiza kuwa nisijeacha kukuona pale MNH. Nikakuahidi nitaendelea kufuatilia siha yako mpaka utakapotolewa pale hospitali. Ulifurahi. Ukatabasamu rafiki yangu.

Rafiki yangu kuna kosa ukalifanya.
Hukujua kama ni kosa. Baadae nikaja jua lilikuwa kosa kubwa. Wakati tumeshaagana na wewe, tunaondoka kama kikundi cha wanafamilia moja, mimi na wale jamaa zako, ukaniita kwa jina langu (ambalo ulilijua muda mfupi tu, tangu tufike pale kitandani kwako, jina langu halisi lina herufi 4 tu, na ni moja ya majina common sana kwa watanzania wengi, sijui kwa nini)

Kosa la pili. Bila kujijua.
Na mimi nikaitikia wito wako. Nikarudi peke yangu. Huku wale wengine kwenye ile convoy wakiwa wamebutwaa, wanaangalia nini kimetokea. Hawakwenda. Hawakurudi. Walisimama. Wakaona ulivokuwa unaniomba nikuinamie pale kitandani. Na mimi nikatii.

Kosa la tatu. Mara, ukaonekana unaninong'oneza sikioni, huku mkono wako mmoja umeupitisha sehemu ya nyuma ya shingo yangu.

Muda wa ftar.


Part VI
Poleni kwa kusubiri, hatimaye nimerudi:

Rafiki yangu kuna kosa ukalifanya.
Hukujua kama ni kosa. Baadae nikaja jua lilikuwa kosa kubwa. Wakati tumeshaagana na wewe, tunaondoka kama kikundi cha wanafamilia moja, mimi na wale jamaa zako, ukaniita kwa jina langu (ambalo ulilijua muda mfupi tu, tangu tufike pale kitandani kwako, jina langu halisi lina herufi 4 tu, na ni moja ya majina common sana kwa watanzania wengi, sijui kwa nini)

Kosa la pili.
Bila kujijua. Na mimi nikaitikia wito wako. Nikarudi peke yangu. Huku wale wengine kwenye ile convoy wakiwa wamebutwaa, wanaangalia nini kimetokea. Hawakwenda. Hawakurudi. Walisimama. Wakaona ulivokuwa unaniomba nikuinamie pale kitandani. Na mimi nikatii.

Kosa la tatu. Mara, ukaonekana unaninong'oneza sikioni.
Nakukumbuka rafiki yangu, na hapa kama nakuona na mguu wako wenye POP, juu ya kitanda! Umeunyoosha. Nilikuwa katikati ya kukusikiliza na kutokukusikiliza. Nadra sana mimi kuwa ktk hali kama hii. Ni moja ya nyakati ngumu sana kuwahi nipata. Mie. Jf wananijua kama slim5. Mimi. Mwenyewe.

Binafsi sikupenda namna lile jopo la jamaa zako, walivokuwa wakinipa heshima ile mbele ya mpenzi wako. Masifa tele. Tena masifa yanayotaka kwa watu wa jinsia kinzani na ya kwangu. Mbele ya mtu wako. Niliyahisi maumivu ambayo jamaa yako alikuwa akiyahisi.

Ni kama vile wewe rafiki yangu na wale jamaa zako, mlimsahau mtu Yule. Mlisahau nafasi yake. Ni kama hamkutambua uwepo wake pale. Aliumia. Na mimi niliumizwa na picha ile. Kama wa kiume, nilihisi namna gani inaumiza aina ile ya mapito. Ilibidi iwe. Ikawa.

Nikiwa kati kati ya kukusikiliza na kutokukusikiliza, nikaskia ukilisemesha sikio langu. Kwa kuwa nilishakuwa na msongo wa mawazo kichwani, wala sikuelewa. Sikuelewa ulikuwa unasema nini. Niliskia sauti yako ikitoka katika mfumo wa maneno. Sikuelewa maneno yale yalibeba maana gani. Uliponiuliza nimeelewa, nikajibu, ndio.

Pamoja na nyakati ngumu uliokuwa nayo siku ya kwanza pale hospitali, bado uligundua kuwa sisemi kweli. Nakudanganya. Uligundua kuwa nimekubali kukuelewa huku nikiwa sijakuelewa. Uliongeza nguvu ktk mkono wako ulioshika shingo yangu. Nikahisi maumivu. Nikajikaza kisabuni. Nilifundishwa kujikaza penye maumivu, na hasa kama anaeniumiza ni mtoto wa kike. Hakuna mwanaume mkamilifu alie tayari kuonyesha udhaifu wake kwa mtoto wa kike. Nikajikaza. Ukasisitiza sana.

Wakati wote wa hii scenario, wale jamaaa zako pale karibu na mlango wa kutokea wodi hii, walifanya kama kigenge na kuwapisha wengine wenye haraka ya kutoka, watoke. Hawakuwa na sehemu nyingine ya kutazama. Walitutazama sisi. Walintazama mimi. Wakakutazama wewe. Ni kama tulikuwa tunaigiza. Igizo la watu wawili. Mgonjwa kwa upande wake. Msamaria mwema kwa upande wa pili. Kuna kitu kilinipata. Mshangao.

Nilishangaa kuona hujali kitu. Hujali wale jamaa zako, hukujali uwepo wa boyfriend wako mtata rafiki yangu, yote kwa yote rafiki yangu hukujali kwamba pale ni hospitali, kwamba upo ktk kitanda cha hospitali, kwamba wewe ni mgonjwa na mimi ni Mtembezi tu pale hospitali!

Rafiki yangu, nilishangaa kuona hukujali kile kikundi cha watu ulichokisababisha pale mlangoni, watu ambao nilikuwa najua kuwa muda mfupi baada ya kutoka pale, watakuwa maofisini kwao wakiwajibika. Ulikuwa unawachelewesha. Ukasababisha minong'ono kati ya dada zako. Wakawa wanaongea ktk namna ambayo mimi na wewe hatukuweza kuskia kitu. Ni hapa, kwa mara ya kwanza nikamskia jamaa yako mtata akichangia ktk majadiliano yale. Tena alichangia maelezo ya memba wengi ktk kundi lile.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye! Ndio ilivokuja kuwa. Huku mimi na wewe. Kule wanafamilia na mpenzi wako. Mtafaruku. Wakapishana Kiswahili. Dada ako mmoja na shemeji yako, lugha zikagongana. Chanzo, mimi na wewe hatukukijua. Mzozo wa watu wanaogombana huku wanajitahidi makelele ya mzozo wao yasisikike. Hatukuwaelewa.

Rafiki yangu. Mimi sijui. Nakiri mpaka sasa hivi, sijawahi kujua nini kilitokea, sijui nini ulikifanya, nikaanza kuyaskia maneno yanayoeleweka kutoka kinywani mwako. Ulizungumza kwa ufasaha sana, neno kwa neno! Kama si wewe uliefikishwa MNH pasi na fahamu. Macho yako yalionyesha nini ulimaanisha ktk maneno yale.

Kulikuwa na mkazo wa ziada. Niliskia. Nilielewa kila neno. Kuna wakati uliweka nukta lakini bado niliendelea kuskia unachosema. Japo kuna nukta. Akili ikanambia, nazungumza na mgonjwa mwenye uwezo mkubwa wa kujielezea. Sikuamini. Naomba ninukuu ulichokuwa unanambia:



Part VII

Habari wanajamii wenzangu!
WanaJamii kumradhi, nimechelewa kurudi, nilikuwa na ugeni mzito ofisini!

Tuanzie hapa leo:

Rafiki yangu. Mimi sijui. Nakiri mpaka sasa hivi, sijawahi kujua nini kilitokea, sijui nini ulikifanya, nikaanza kuyaskia maneno yanayoeleweka kutoka kinywani mwako. Ulizungumza kwa ufasaha sana, neno kwa neno! Macho yako yalionyesha nini ulimaanisha ktk maneno yale. Kulikuwa na mkazo wa ziada.

Nilielewa kila neno. Kuna wakati uliweka nukta lakini bado niliendelea kuskia unachosema. Japo kuna nukta. Akili ikanambia, nazungumza na mgonjwa mwenye uwezo mkubwa wa kujielezea. Sikuamini. Naomba ninukuu ulichosema:

"Manabii wameondoka na maajabu yao! Mungu ana njia nyingi za kuonyesha maajabu yake sasa! Siamini. Siamini kilichonifika. Hapa wodini kuna bibi ana karedio kadogo hivi, asubuhi amenisikilizisha matangazo! Polisi wameeleza taarifa zangu katika radio. Wamesema kuna binti amegongwa jana usiku na gari ndogo maeneo ya Ubungo, kisha gari haikusimama! Kuna msamaria mwema amemuokota majeruhi huyo, na sasa hivi anaendelea na matibabu Muhimbili! Huyu bibi (ukanionyesha kwa uelekeo wa macho yako) akataka kujua kama ndio mimi, ndio akujia na kale karedio. Binafsi nikawa na maswali mengi sana kichwani, kubwa ni kama kutakuwa na uwezekano wa kumuona mtu huyu, alieokoa uhai wangu. Kumbe ni wewe! Ahsante sana, nimeipata fursa hii."

Yule nesi wetu alishaanza zoezi la kutimua watu. Watoke mle wodini, kwamba muda wa kuwaona wagonjwa umeisha. Kuna kitu sikuwa nimeelewa. Muda wote ambao nesi alikuwa akitimua watu mle wodini, huku akizunguka zunguka ktk vitanda ambavyo wagonjwa bado wanabadilishana salamu, mawazo na jamaa zao, hakujaribu hata kidogo, si tu kusogelea kitanda ulichokuwa wewe, bali pia hata kutupiga macho hakuthubutu! Sikuelewa. Baadae nikahisi labda nguvu ya chai ya dada mkubwa, penye udhia.....!

Rafiki yangu ukaendelea kutiririka. Wakati wote uliokuwa ukitiririka binafsi nilikuwa nafanya tathimini za jumla jumla, namna Muumba alivodhihirisha uwezo wake juu ya mwili wako. Ashukuriwe Mungu. Sikupoteza muda kuangalia maumbile yako ya chini, niliyaona vizuri sana jana yake ktk purukushani za kukupandisha katika ile STJ. Of course, katika lile zoezi, nilitumika kukushika maeneo ya kiuno ili kukupandisha garini, wengine sehemu za juu, wengine miguu, nilikuwa na picha halisi ya maeneo yako ya kiuno na vyote vyenye nasaba na kiuno. Mungu mkubwa.

Black beuty. Zamani ungeitwa maji ya kunde. Siku hizi wameboresha, wanasema rangi ya choclate. Mguu ulikuwa mguu kweli. Sio fito. Kimo cha wastani, wambea wanasema eti si mrefu, si mfupi. Sauti yako hata ingetoka gizani, ilitosha kumuaminisha msikilizaji wako kuwa anaskiliza sauti ya binti, hata kama si mrembo basi yatosha kusema ameumbika!

Ni katika mazingira magumu kama yale ya jana usiku, ndio unaweza kuhitaji kitu cha ziada ili uweze kujua majina, umri, eneo husika la mtu - manusra wa ajali kama ilivokuwa kwako. Kuviskia hivyo vyote ni jambo moja, kuvikariri kichwani ili niweze kuvitumia na kutoa maelezo baadae, lilikuwa jambo jengine. Mimi niliweza. Sauti ya kike hasa (Nimeikumbuka sauti ya Spika)! Ningeshindwa vp wakati kwa sauti yako tu, ilitosha kurahisisha zoezi la kukariri.

"Nakushukuru! Sijui hali ingekuwaje kama sio wewe. Ajali za barabarani, huwa zina changamoto nyingi sana, na hasa katika miji mikubwa kama DSM! Ningeweza kuachwa pale, vibaka wangejipatia riziki yao, watu wangenipita, hakuna wa kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali, tena nyakati za usiku, nadhani ilikuwa ni kifo. Una moyo kaka, una moyo wa ajabu sana.
Nakushukuru sana kwa wema wako, Mungu akubariki sana ndugu yangu!

Nipe namba yako! Haaa – sasa nitawasiliana vipi na wewe? Unakaa wapi? Unafanya kazi gani? (idadi ya maswali iliongezeka zaidi) Daaah, sasa nakuomba fanya kitu kimoja, jitahidi kadri ya uwezo wako usikose kuja mchana wakati watu wanawaletea vyakula wagonjwa, usikose! Naomba ujue kitu kimoja, hao woote uliowaona wamentembelea hapa asubuhi hii, hamna mwenye nafasi ya kuja hapa mchana, watakuja saa 10, ni dada mkubwa tu ndiye atakaekuja mchana kuleta chakula. Mtakuwa wawili tu, wewe na dada! Si utakuja? Ni lazima uje, nataka uje mchana, kwangu ni muhimu sana wewe kuja hapa mchana. Leo"

Kwa kawaida binadamu huwa hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, huwa inatokea mara chache sana. Kwa mfano, katika kubishana, huwa si rahisi wanaobishana wakawa wananong'ona, ni ngumu sana. Ndio ilivokuwa pale ktk kitanda chako, ilibidi tuanzishe mazungumzo rasmi. hatukuweza kunong'ona! Ukaniachia. Nilijikuta nikijimuvuzisha huku nikikuonyesha kuwa sijaridhika, nilitamani baada ya kuniachia, sasa unikumbatie kabisa, zamu yako kuniskiliza! Niskilize huku umenikumbatia! Haikuwezekana.

Maswali yako yote yalipata majibu hasi kutoka kwangu isipokuwa lile la unaishi wapi na lingine la unafanya kazi gani. Uso umeumbwa na haya. Nilijishtukia kubaki mahali pale – wodini, watu wachache sana, kama wawili ama watatu, huku wengi wakiwa wametimuliwa na Yule "nesi wetu" wengine waliobaki ni wagonjwa kama wewe. Nikakuomba tufupishe mazungumzo, kwamba ntakuja tuongee jioni, muda umefika na mimi niondoke, niwahi kibaruani kwangu, kwamba na wewe unaitaji kupumzika!

Nilikukatalia wazo lako la mimi kuja mchana, nililisisitiza kuja jioni. Muda wa mchana, nisingeweza kuja Muhimbili kukuona, kwa aina ya kibarua changu, huo ulikuwa muda wa kazi nyingi. Nilikueleza kuwa, ili niwahi Muhimbili kwa kutokea Mwenge, ilibidi nitoke mwenge walau sa5 asubuhi, na mpaka narudi tena ofisini itakuwa ni zaidi ya saa 8, hii itakuwa ngumu na hasa kukiwa na ukweli kuwa asubuhi nilianzia Muhimbili, na hivo kuchelewa kuingia kibaruani.

Wazo la kupoteza masaa kama matatu kwa safari yangu ya Mwenge – Muhimbili, ulilipinga kwa hoja kuwa, dada ako mkubwa, ofisi zake zipo maeneo ya Mbezi beach, na unao uwezo wa kuweka utaratibu na dada ako akanipitia mimi Mwenge, tukaja wote Muhimbili. Bado sikulikubali wazo hili. Akili yangu ilishahamia ktk aina ya kibarua changu, kwamba ukiwepo unaingiza – usipokuwepo na lako halipo, wewe hukulijua hilo! Nikajikuta natoa sauti ya juu kidogo kumuaga Yule "nesi wetu" na kumshukuru sana. Hatimaye nikatoka pale wodini kwa maelezo kuwa nitapanga na dada ako.

Tukiwa na jamaa zako, tunatembea kuelekea nje ya MNH, nilipata fursa nyingine ya kuwa karibu na "mtu wako." Nadhani kuna seminar alipewa, sijui na nani, mimi sifahamu. Nilimuona akiniongelesha. Safari hii kwa utulivu sana. Aliongea mithili ya mtu anaetaka msikilizaji wake, ajue kuwa yeye ana vitu vinavofanana na hekima, busara ama ustaarabu. Alijitahidi. Aliongea sana, maelezo yake yalionyesha kuwa anajutia vile ambavyo vimetokea baina yake na mimi.

Alitumia muda mwingi wa matembezi yale, kunishawishi niamini kuwa anajutia kile kitendo chake cha kutumia nguvu ya ziada katika namna ambayo baadae alijiona kuwa ni mpum***u. Hakutaka kusema samahani, nilishaelewa kuwa amemaanisha samahani. mkubwa hakosei. Sinaga kinyongo. Ndio kwanza nikamsifia kuwa anajua kupenda. Akacheka. Nikamsisitizia kuwa anajua kupenda, kiasi yuko tayari kupigana na mtu asiemjua, tena usiku, bila kujali huyo mtu ana silaha ama laa! Akaonyesha kufedheheka. Nilielewa kwa nini moyoni mwake mbegu ya chuki ilichipua. Chuki kwa Msamariamwema aliemsaidia mpenzi wake. Mwanaume akifanikiwa kummiliki kiumbe wa mfano wako, huwa kuna artificial intelligence inaji-install kichwani mwake! Wivu!

Dada ako aliingilia mazungumzo kati yangu na mbaya wangu. Alitaka kujua naelekea wapi. Nikamjibu mwenge. akaniomba tuzungumze kwa dakika chache, kabla hatujaachana, kwa sababu anataka kwenda Ubungo kufuatilia vile vitu vyako - mdogo wake, vitu nilivowatajia jana usiku, manusra wangu wa ajali. Aliitumia fursa hiyo vizuri na kuniuliza mambo mengi sana. Aliniuliza kuhusu wazazi wangu, aliniuliza kuhusu ninapoishi, naishije? Na kina nani?, aliniuliza kuhusu shule, aliniuliza kuhusu kibarua ninachofanya, kisha akaniuliza kuhusu wewe. Akaniuliza kuhusu mahusiano, akaniuliza kuhusu wewe, manusra wangu wa ajali! kuhusu wewe, kuna kitu akanambia. Kwanza alisita. Kisha akasema:

beb v
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hebu malizia kuandika basi au kibodi yako imeisha wino nikuazime yangu?
 
Wewe malizia ndiy tutiririke,isije mgonjwa alikufa then sisi tucomments eti congrats she must be your wife wakati kumbe maskini ya Mungu mgonjwa mwenyewe alitangulia mbele ya haki na wewe uliswekwa lupango kwa kuwa walihisi wewe ndiye aliemgonga na gari yako ama ya rafiki yako.Malizia kwanza ndiyo tuje tukiwa full
 
I guess ndo umetolewa nje kwa dhamana...!!!


Endelea...
 
Kama unamtafuta si ni vyema ukaenda radio One... Otherwise kama ni stori ya kweli basi pole na hongera..
 
bonge la love story, hao polisi marafiki zako nini? aya malizia basi, matangazo na wimbo umeisha, karibu msimulizi.
 
Back
Top Bottom