Tulipoishia muda ule!
Polisi: kwenu wapi?
Mimi: Buguruni?
Polisi: Huyu ulikuwa nae guest.
Mimi: Hapana afande, katoka ktk mizunguko yake, mm simfahamu kabisa!
Polisi: umewezaje kujua majina yake, anapokaa, umri wake? km si mpenzi wako?
Mimi: nilimuhoji alipojiwa na fahamu akanijibu yote hayo.
Polisi: Utakuwa tayari kutupeleka eneo la tukio?
Mimi: (tayari walishanivuruga) Nikatikisa kichwa, kwa alieniona asingeweza kusema kuwa nilikuwa nakataa ama nakubali! Haikueleweka!
Hatimaye nikapewa PF3 pale pale viunga vya Muhimbili!
Kama kuna kitu umejifunza ktk mkasa huu, ama kuna hisia zimekujia, tiririka! Comments zenu zitanifanya nirudi ama nisirudi kumalizia, my life experience!
Karibu tena!
Ilipotimu kama saa 7 usiku, majeruhi wangu, aliekuja kuwa rafiki yangu, japo kwa muda mfupi, alishapatiwa kitanda katika moja ya wodi pale Muhimbili. Mpaka napewa taarifa kuwa amepewa kitanda, sikuwa najuwa kuwa muda tu, walishamchoma sindano (nahisi) ya usingizi. Hivo sikuweza kumuaga, nikaweka nia kwenda kumuona kesho yake asubuhi.
Huku nje napo, wale polisi walikuwa wakinisubiri ili safari ya Ubungo, eneo la tukio, ianze. Ile najitokeza tu, mbele ya macho ya polisi wale, nikaskia sauti ya polisi mmoja akisema: Msamariamwema aliemuokota ndugu yenu ndiye huyu hapa! Ndugu wa manusra wangu wamefika muhimbili, kufuatilia nini kimemkuta mpendwa wao, nikawaangalia haraka haraka kuona aina ya facial expression waliokuja nayo, nikajua wamejawa na mchanganyiko wa taharuki, machungu na shauku!
Mpendwa rafiki yangu, kulikuwa na dada yako mkubwa, dada yako mwingine, mdogo wako na boyfriend wako. Dak 3 za salamu, zilitosha kunipa picha kuwa, wale watu wa jinsia ya kike walishalia sana, nadhani sura zao zilionyesha kuishiwa na machozi. Waliniparamia huku wakiwa na shauku ya kujua hali ya ndugu yao!
Dada mkubwa alikuwa na nguvu ya ziada, alikumbuka kunisalimu, akanishika mkono! Akanipa pole! Akanipa hongera! Akaniomba niseme, hali ya mgonjwa! Nakumbuka nilisema kwa ufupi sana, maneno mawili tu, hajambo, amelazwa!
Baada ya kuskia hivi, ndio ikaja akili, wakaomba tukae chini, dada mkubwa aliomba kujua uhalisia wa tukio zima! Nikiwa na uchovu uliopitiliza, sina hamu ya mahojiano ya tukio lile, niliisi kazi imeanza upya ktk hatua ambayo niliamini naimaliza kazi!
Polisi wetu wakasisitiza tuzungumze kwa ufupi ili safari yetu ianze kwenda eneo la tukio! Wakati naanza kuwasimulia wale wana ndugu kuhusu tukio lililompeleka ndugu yao Muhimbili, kulikuwa na maswali yanachomekewa na wale wadada, hapa na pale, nikawa nayajibu huku lugha yangu ikimaanisha, nimechoka naomba tumalize niondoke hapa!
Ilifika zamu ya Yule mtu wa kiume (nilikuja kujua baadae kuwa ni bf wako) kuuliza swali! Swali lake la kwanza lilikuwa la ajabu, ni swali lililochanganyika na majibu, naomba nimnukuu Yule mtu wako, ewe rafiki yangu:
wewe ni mwanaume, unawezaje kumsaidia mtoto wa kike, usie na uhusiano nae, tena usiku? Nyie mtakuwa mmetoka guest, kwa haraka zenu mwenzio akagongwa na gari! Wewe unamjua huyu binti, acha ujanja bwana mdogo! wakati najaribu kumuelezea kama sio kujitetea, jamaa akanikunja kwa ile style ya kunisimamisha kutoka pale chini nilipokaa! Ghafla Polisi wetu wakashtuka!
Tukutane baada ya ftari!