Stori ya David Masha: Ajali iliyompa ulemavu wa kudumu, kukubali matokeo na kutokata tamaa

Hongera sana!
 
ASANTE Mungu, asante sana David kwa simulizi ya kusisimia hakika tumejifunza mengi, Allah azidi kuwabariki, nimependa jinsi ulivyoiweka story yako ili tujifunze!
Binafsi nilianza kumsikia habari yako kipindi umeoa, nikavutiwa mno na wewe!
Dah safi sana David!
 
Hongera sana kwa David. Niliona stori yake inaweza kuwa na manufaa kwa wengi ndiyo maana niliichukua toka ukurasa wake wa Instagram na kuweka hapa ili isomeke vema kwa kila mmoja, na kwa mtiririko usio na vikwazo. Niliihariri kwa kiwango changu kutokana na urefu wake.

Davie ni mpambanaji. Mungu aendelee kumbariki sana. Ni simulizi za namna hii ambazo zinatupa mwanga na kutuonesha njia maishani.
 
Hadithi ya David inanikumbusha Sana hadithi ya yule Binti yetu Wakonta ambaye naye alipata ajali ya Kugongwa na Gari na Mwanafunzi mwenzake siku ya Graduation Yao pale Korogwe Girls Secondary na aka paralyise kutoka Shingoni hadi nyayoni.
Poleni Sana na Pongezini Sana Kwa Ushujaa wenu.
 
Dah! We jamaa mpambanaji! Umeniliza vibaya mno kwa story yako hasa kwenye mama wa kukulipia ada ya chuo, mdada wa connection ya hadi kupata mkopo n.k! Hongera sana tena sana na pole kwa yote ulopitia! Mafunzo ni mengi mnooo kwenye story hii lakini pia akina Dada Idda naamin tumebakiza wachache! She deserves the high rank respect[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
AISee nimepata mafunzo hapa na tena funzo kubwa la kutokata tamaa hata kama unapita mazingira au hali gani ngumu hupaswi kukata tamaa pambana na songa mbele

ila nakushauri mdogo wangu mcharo haya uliyoyaweka hapa yangeamia kwenye kitabu yaani ukataengeneza kitabu cha historia ya maisha yako nadhani ungepata hela pia na vilevile ungejisajiri kule AMAZON kuweka hii makala yako uliyandika hapa ungeingiza pesa pia haya ni maoni tu na ushauri mdogo wangu pole sana Mungu anaweza ukimwomba na kumtegemea
 
The story of change hii kaka hongera na pole kwa yote uliyopitia kweli God is good all the time
 
Ahsante Mungu Kwa Kunibariki Hali Niliyonayo Sasa japo kuna muda Nilijiona si Kitu Chochote kumbe kuna watu wanapitia Mengi mazito zaidi yangu na hawaachi kukushukuru.
 
Yaaani hiii story imenitoa machozi, jamani
Mungu ni wetu sote,
 
Safi sana ndugu David, hayo mambo hamna anaelewa.
Wengine tulipiga mzinga hapo Dar na askari hawa wa defender walikuja sehemu ya tukio fasta ni kwamba hela ilipigwa usiku huo ni nyingi mno in terms of cash pound. wakapiga kila kitu mpk gari iliyopata ajali.
Hii tuliikuta kituoni inauzwa chuma chakavu.
Cha kushangaza wamechukua PF3 fire kwamba walikuta maiti mbili nje ya ajali tupelekwe mochwari tukaandikiwa tukapelekwa MOI
Yule daktari alikua muadilifu sana ndio alitupima akagoma akaona mbona wazima .
Wao wametubwaga wameondoka.
Daktari kaweka dripu na kukaa pale anatuskilizia mpk siku ya pili tunaamka.
Huko Sewa haji,sijui kibasila mi nshakaa sana tu.
Na kuna wodi kipindi cha kukata miguu boda hawa mi nilikua pale.
Nimeona sana hiyo.
Na nilikoswakoswa maana kimguu kiliteguka katika ajali.
Ebo jamaa wakataka kikatwe.
Kumbe kuna jamaa pale ana deal la kutengeneza magongo enzi hizo.
Unalimwa mguu fundi seremala yuko hapo na futi anakupima size.anaenda kulitengeneza
Ilikua kulilipia 70-laki.
We unaskilizia maumivu
Badae gongo hilo hapo,wazazi wako wanapewa mzigo kulipa bill.
Nilipiga kelele sio ya dunia hii.
Sa hii ningekua kilema.
Huyu jamaa naskitika kakosa miguu ashukuru uzima.
Kusema ukweli mguu wangu ulipona
Kichwani nimeathirika ingawa hujui ukiniona..
Kilichopotea si mbaya natafuta tu.
 
Mungu aendelee kukutunza na wote walioshiriki vyema katika mapito yako,, hongera kwa kumpata Jessica
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…