Stori ya David Masha: Ajali iliyompa ulemavu wa kudumu, kukubali matokeo na kutokata tamaa

Pole sana mkuu.
 
Pole na hongera sana David, hakika kumtegemea Mungu kuna faida
 
🙏🙏🙏🙏
 
Kuna mpare mmoja school mate wa David amethibitisha hii story ni ya kweli na hata alipooa David mwaka juzi huyu mtu alikuwepo.
 
Hongera sana.
Hakika umekuwa mfano bora unaoishi.
Mungu asimame katika maisha ya familia yako
 
Jamaa ni mpambanaji aisee bila kujali hali yake ila pia nimejifunza pia kuwa na upendo endapo kuna mwanafamilia amepata changamoto. Kwa upendo walioonyesha wanafamilia katika kipindi chote cha changamoto ndio kimempa fursa ya kuweza kujitegemea lakini pia kuleta ahueni kwa wanafamilia baada ya kupata kazi.

Wakati mwingine familia zetu huwa tunachoka kuwahudumia wapendwa wetu na kujikuta ile changamoto inakuwa ya kudumu matokeo yake mnakuwa mnajichangisha maisha yake yote kumbe support ikiwepo hata kama sio fedha inampa nguvu mgonjwa kuweza kujikubali na kusonga mbele

Hakika David ni mpambanaji
 
God is good always.

Unaendeleaje sasa.

Maisha ya kazi na familia yanaendeleaje.
 
Naomba mungu anisamehe sana kwa kuona eti maisha ni magumu sana hali ya kua ni mzima wa viuongo. Hii stori imenifanya nijione naweza kufanya chochote na sitokuja wai kukata tamaa. Zaidi ya hayo nampongeza sana David kwa kupambana na kua mvumilivu. Mwenyezi mungu amzidishie
 
Maisha ni kupambana sio show off. Maana soon watu watamchoka huko mitandaoni
 
Maisha ni fumbo gumu sana.

Mtu utaishia kujiuliza maswali yasiyoisha, "kwa nini sikumsikiza Mwalimu alivyoniambia Jamaa amelewa?", kwa nini sikupanda tu ile Hiace na wale Wadada?", "kwa nini sikuenda tu kwenye mazoezi kama alivyoniambia Jama?" lakini ndio hivyo kilichotokea kimeshatokea.

Kila la kheri Ndugu.
 
Kuna mahali nilipofika kupasoma nilitokwa machozi,hasa kwa yule mama Lyimo,unadhani ni machozi ya furaha,...pole sana ndugu na hongera kea kutokukata tamaa,Mungu atakusaidia zaidi
 
Mimi kiujumla napenda sana stories,hasa ambazo ni true stories lakini hata isipokuwa true ila INA mafunzo hio huwa siiachi inipite,...
Wadau wangu wa Chuga,Manyara na wengine sijui hata ni wa wapi ila tumezoeana kimtindo humu humu😂
Ibra tiger
fyddell
Glenn
goroko77
Meidar
herio
.....Wakuu japo Uzi ni wa mwaka Jana lakini kama hamkupata bahati ya kuupitia njoeni tuongeze somo kwa sisi tumtumainio na kumtegemea Mungu🙏,kuna somo kubwa hapa,
Waalikeni na wengine wajifunze
 
Mimi kiujumla napenda sana stories,hasa ambazo ni true stories lakini hata isipokuwa true ila INA mafunzo hio huwa siiachi inipite,...
Wadau wangu wa Chuga,Manyara na wengine sijui hata ni wa wapi ila tumezoeana kimtindo humu humu
Nafurahi kwa huu wito mkuu, binafsi nilishaupitiaga kitambo sana huu uzi tangia kuanzishwa kwake. Kubwa ni kwamba hakuna muda muafaka wa kujifunza, daima tunajifunza na kuendelea kujifunza kupitia watu mbalimbali maishani.
Tuko pamoja sana ndugu zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…