Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Katika ukanda mmoja wa Kusini wa Bara la Asia, palikuwa na mfalme mmoja ambae alitawala himaya yake kwa weledi na ufanisi mkubwa mno. Mfalme huyo alikuwa akipenda sana haki na utiifu mno, kiasi kwamba aliwaadhibu vikali mno wale wote walioenda kinyume na sheria na taratibu za himaya yake.
Mfalme huyo alifuga mbwa wakali sana, mbwa hao alikuwa akiwatumia kuwapa adhabu watu wote waliokuwa wakienda kinyume na maagizo yake au kukaidi amri za falme yake. Mfalme alikuwa anawakamata watu wenye makosa na kuwatupa kwenye banda la mbwa hao wakali, mbwa hao walikuwa wakila nyama za watu wote waliokuwa wakitupwa mule bila kuwa hata na huruma.
Siku moja mmoja wa watumishi wa karibu sana wa mfalme alimkosea mfalme, mfalme alichukia sana na kutoa amri mtumishi huyo akamatwe na atupwe kwenye banda la mbwa wale wa adhabu. Lakini kabla ya agizo hilo kutendeka, mtumishi yule alisema "ewe bwana wangu, nimeweza kukutumikia kwa takribani miaka 10 na wala sikuwahi kukutwa na hatia yoyote Ile.
Basi kama ikikupendeza naomba unipe nafasi ya siku 10 tu niweze kuvuta pumzi yangu ya mwisho kabla ya kifo changu". Basi mfalme akalikubali ombi lake na akapewa siku kumi za kuishi kabla ya kuuwawa.
Basi mtumishi yule akaamua kuzitumia siku zile kumi kwa kuwa mfanyakaz wa mbwa wale wa mfalme wa mauaji. Akawa akisafisha banda na kuwapa huduma zote mbwa wale, hata baada ya siku 10 kupita mfalme aliweza kumkamata mtumishi yule na kumtupa kwenye banda lile la mbwa lakini cha kushangaza mbwa wale hata hawakumla wakaishia tu kumnusa nusa na kumramba ramba kisha wakamuacha.
Mfalme alishtuka sana na tukio hili na kupigwa na butwaa, akauliza kwa sauti kubwa "hiki ni nini, mbona hawamli" ndipo yule mtumishi akamjibu mfalme na kumwanbia "niliweza kukutumikia kwa miaka kumi lakini hukuweza kuona umuhimu wangu kiasi kwamba ukaruhusu kosa langu moja kukusahaulisha yale yote mema niliyowahi kukutendea, lakini mbwa hawa niliweza kuwatumikia kwa siku 10 tu lakini waliweza kukumbuka wema wangu kwao niliowatendea na ndio maana hawakuweza kunidhuru"
SOMO: Mfadhili mwanadamu kwa miaka mitatu atakusahau ndani ya siku tatu, mfadhili mbwa kwa siku tatu atakukumbuka kwa miaka mitatu
Wako katika kalamu Amani Dimile

Upvote
0