NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
kwangu niliona shule siwezi tena maana uwezo wangu wa kujifunza ulikuwa mdogo, walimu darasani walikuwa wanafundisha kwa spidi kubwa kuzidi uwezo wangu, vitabu hakuna, sina hela za kwenda tuishen, n.k.
Form 4 matokeo yalitoka nina division 4 mbaya sana lakini waziri wa elimu wakati huo alibadili matokeo nikapata division 3 nzuri, nadhani kuanzia wakati huo mpaka sasa tushazoea kuona hata wanaofeli wachache, hata shule yangu zamani ilikuwa ina division 4 na 0 nyingi siku hizi zinahesabika, wanafunzi wengi ni division 1 hadi 3,,,,
Kwa upande wangu licha ya kubadilishiwa matokeoa kuwa mazuri mi nilikataa kuendelea na shule maana sikuwa na sifa maana hata sikuweza kufanya hesabu za form 1.
Familia ni kama ilinitelekeza basi ntajijua mwenyewe na mimi nikaona mapema hapa nitafute kazi, nilikuwa na rafiki yangu alikuwa na mjomba fundi seremala nikamuomba anifanyie connection niwe msaidizi, hilo likafanikiwa "mjini ni connection"
Mtu anaweza kusema nilipata zali lakini mimi mhusika nilichoenda kutana nacho mwanzoni ni kama niliingia chumba cha mateso, nilitamani hata kukimbia lakini nikifikiria nyumbani najikaza tu....Kazi ilikuwa ni kazi aisee, asubuhi hadi sometimes usiku ni kazi mtindo moja, sugu zilianza kuota kwenye viganja, nyundo zile nikikosea kulenga msumari najipiga kidole natamani hadi kulia lakini najikaza, kazi nyingine kupiga msasa mbao hadi mikono inachoka natamani kulia lakini najikaza, uncle akanipa ushauri niwe napiga zoezi ndio nikawa nikifika nyumbani naenda uwanja wa karibu nakimbia, push up, kichura, n.k. hii ilinisaidia sana kupunguza ugumu wa kazi
ndani ya mwaka hivu nilianza kuwa mzoefu,.uzuri wa maseremala wengi sio wachoyo, msosi nilikuwa nakula pale pale maana ilikuwa ni karibu na nyumbani kwake, mke wake analeta msosi nami nahesabiwa,, hela nilikuwa napewa nauli tu, posho mara chache sana,,, niliweza kuzoeana na uncle vizuri maana niliheshimu ratiba yake, nilichapa sana kazi na nilimheshimu yeye kama mtu mzima, uzuri uncle hakuwa na vurugu kwahio haikuwa shida.
Baada ya mwaka nilianza kukabidhiwa baadhi ya vikazi vidogo vidogo niwe navifanya ila malipo yalikuwa pasu kwa pasu na wala sikuwa na tatizo maana nilitumia vifaa vyake, ofisi yake, uzoefu wake na brand yake.
Nilipata vihela hela pale nyumbani nikaaga japo haikuwa rahisi maana niliondoka na begi langu tu, nikapata ghetto langu nikiwa na miaka 19....
kiukweli mjomba alikuwa na wateja wengi sana kwa hio suala la pesa kwangu ilikuwa ni uhakika kulaza 5 hadi 20 kwa ile nusu yangu kila siku kwa kazi ndogo ndogo ambazo uncle aliniachia nizifanye.
Nyumbani nikawa nawapelekea vitu vitu na vizawadi nami nikaanza kuthaminiwa, kiukweli nyumbani nilikuwa nimepakumbuka sana hasa mdogo wangu ambae alikuwa ni besti yangu acha tu.
Nilipofika miaka 22 nilikuwa najua vingi sana kwenye useremala hadi uncle akaanza kunipa dili nzito nzito akitingwa na kazi, niliweza kununua pikipiki yangu lakini niliiuza maana kuna ajali chupuchupu ininyofoe miguu..
Kufikia miaka 23 uncle akaniambia nishaiva kama nahisi kuondoka mimi niwe huru tu, wala hawezi kumaindi na pia ni vizuri niwe na ofisi yangu, nilifanya hivyo.
hadi sasa nina ofisi zangu mbili maisha yanaenda ..... nina usafiri wangu nimevunja laana ya familia yetu kutokua na gari 😂😂😂