Stori za Kijiweni!

Iyegu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
6,276
Reaction score
12,404
Kijiweni bhana!
iwe kwenye kahawa,drafti,kwa fundi baiskeli...kwa fundi wa kushona nguo,stori ni kiungo muhimu sana kuliko kitu chochote mahali hapo...mara Simba mara Yanga,Man U mara Chadema mara makinikia...Tshishimbi mara Niyonzima..
Ikiisha hii inakuja ile,siasa mara uchawi[simtaja mshana jr],kila mtu kijiweni ni muongeaji,asipoongea atacheka,akiondoka anaenda kuhadithia..
Kijiweni ni sehemu yenye mambo mengi sana,utasikia hata idadi ya pasi alizopiga Ajibu kwenye mechi..
Ebu ngoja niende kijiweni nitakachosikia nitakuja kuwaambia...
 
Kuna stori huwa hazina mwenyewe, kila kijiwe zina mhusika tofauti... Yaani hata wewe ukiwa wa kwanza kuisimulia kwenye hicho kijiwe unajivisha uhusika mkuu.
Sasa kuna mwana akaja na stori kuwa yeye ana 'kirago' chake Segerea kwa hiyo haogopi kwenda jela, siku pila limetinga maskani na yeye akazolewa. Kufika kituoni wakamkuta kajikojolea...
 
Usiombe mtu akaja na stori za kukutana na majini usiku..
 
Na kwenye vilinge vya wachawi na kwenyewe wanapigaga story?,nyie mnaopitapita huko mtakuwa mnajua mtujuze na sisi tunaofanywa vigoda wakati huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…